Serikali kuwabana makocha na wachezaji wa kigeni

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
1580814604901.png

Serikali imesema itaendelea kuwabana wafanyakazi na wachezaji wote ili walipe kodi stahiki na Serikali iweze kupata mapato yake.

Akijibu swali la Mbunge Bungeni leo Januari 4, 2020 Naibu Waziri wa Fedha Dk. Ashantu Kijaji amesema katika kipindi cha 2017/18, Serikali imekusanya Sh 1.7 bilioni ambazo zimetokana na malipo ya kodi ya ajira kutoka kwa makocha na wachezaji wa kigeni wanaofanya kazi hapa nchini.

Nkamia amesema ulipaji kodi kwa kada hiyo hauna mpangilio maalumu na kuwa Serikali inapoteza fedha nyingi.

Akimjibu Mbunge huyo, Dk. Kijaji amesema, kwa mujibu wa Sheria ya Kodi ya Mapato ya Mwaka 2004, Kifungu cha Saba (7), kila mtu anayepata mapato yatokanayo na ajira ndani ya Tanzania anawajibika kulipa kodi ya mapato kulingana na kipato chake.

Amesema suala kujua nani anastahili kulipa kodi no jukumu la mwajiri ambaye ndiye anatakiwa kutoa taarifa ana wafanyakazi wangapi na wanatakiwa kulipa kodi kiasi gani.

Awali Mbunge wa jimbo la Chemba Juma Nkamia alihoji Serikali imekusanya kiasi gani cha kodi kutoka kwa makocha na wachezaji wa kigeni wanaofanya kazi nchini katika kipindi hicho.
 
Back
Top Bottom