Serikali kuunda Mamlaka Kuu ya Mapato ya Taifa

Serikali kuunda Mamlaka Kuu ya Mapato ya Taifa

singidadodoma

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2013
Posts
4,394
Reaction score
1,538
SERIKALI inatarajia kuunda Mamlaka Kuu ya Mapato ya Taifa nje ya Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) iliyopo sasa, kuondokana na malalamiko ya kero za kodi kwa wananchi wenye kipato cha chini.

Aidha, TRA imefuta kodi elekezi kwa bidhaa zinazoingizwa nchini kwa msamaha wa kodi hususani zinazotoka China, hivyo wafanyabiashara waliokuwa wakinufaika na fursa hiyo, watatakiwa kuanza kulipa kodi.

Hayo yalielezwa jijini Dar es Salaam jana na Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari. Akizungumzia mamlaka mpya itakayoanzishwa, alisema hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali kusaidia wananchi wa kipato cha chini, kumudu kulipa kiwango cha kodi kinachowekwa na mamlaka hiyo.

“Napenda kuwaambia umma wa Watanzania kwamba Serikali ya Awamu ya Tano inawajali watu wake na ndiyo maana imeona kuwa kuna haja ya kuunda mamlaka moja ya utozaji wa kodi itakayojumuisha taasisi zote zinazohusika na kukusanya mapato nje ya kodi na ushuru ili kuondokana na malalamiko mengi ya wananchi juu ya utozaji wa kodi hasa katika halmashauri zetu,” alisema Kidata.

Kamishna Kidata alisema katika dunia, hakuna serikali ambayo imechaguliwa na wananchi ikaamua kuwakandamiza wananchi wake . “Hivyo basi kwa sasa serikali ipo katika mchakato wa kuunda mamlaka hiyo ambayo itasaidia kuweka viwango vya kodi ambavyo wananchi wa hali ya chini watamudu kulipa kutokana na biashara au kazi wanazozifanya,” alisema.

Kamishna huyo alisema mamlaka yake kwa kushirikiana na mamlaka nyingine, zinazokusanya kodi katika halmashauri nchini, watahakikisha wanapatia ufumbuzi kero ya kodi kwa wananchi wa hali ya chini kwa kupata muafaka, ambao utasaidia pande zote mbili bila kukandamiza upande wowote ama Serikali au mwananchi wa kawaida.

Ingawa TRA imekuwa na rekodi nzuri ya ukusanyaji wa kodi, kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuhusu kodi zinazodaiwa kuwa za kero. Akizungumzia kufutwa kwa kodi elekezi kwa bidhaa zinazoingizwa nchini kwa msamaha wa kodi, Kaimu Kamishna Kidata alisema awali, kulikuwa na punguzo la kodi kwa wafanyabiashara wanaoagiza na kuingiza bidhaa kutoka China kwa kupunguziwa sehemu ya kodi.

“Tumeamua kuondoa kodi elekezi kwa sababu haina faida kwa taifa letu kwani inawanyima wafanyabiashara wengine ambao hawaagizi bidhaa kutoka China, fursa ya kushindana kibiashara.
 
Serikali ipo kwenye mpango wa kuunda Mamlaka ya Mapato Kuu ya Taifa nje ya Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) iliyopo kwa sasa ili kuondokana na malalamiko ya kero za kodi kwa wananchi wenye kipato cha chini.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Kaimu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Alphayo Kidata alipokuwa akifafanua kuhusu juhudi za Serikali katika kuwasaidia wananchi wa kipato cha chini kuweza kumudu kulipa kiwango cha kodi kinachowekwa na na Mamlaka hiyo.

“ Napenda kuwambia umma wa watanzania kwamba Serikali ya Awamu ya tano inawajali watu wake na ndio maana imeona kuwa kuna haja ya kuunda Mamlaka moja ya utozaji wa kodi itakayojumuisha taasisi zote zinazohusika na kukusanya mapato nje ya kodi na ushuru ili kuondokana na malalamiko mengi ya wananchi juu ya utozaji wa kodi hasa katika Halmashauri zetu”Alisema Kidata.

Kamishna Kidata amesema kuwa katika dunia hii hakuna Serikali ambayo imechaguliwa na wananchi ikaamua tu kuwakandamiza wananchi wake katika jambo lolote lile hivyo basi kwa sasaserikali ipo katika mchakato wa kuunda Mamlaka hiyo ambayo itasaidia kuweka viwango vya kodi ambavyo wananchi wa hali ya chini watamudu kulipa kutokana na biashara au kazi wanazozifanya.

Kamishna huyo ameongeza kuwa Mamlaka yake kwa kushirikiana na mamlaka nyingine zinazokusanya kodi katika Halmashauri nchini watahakikisha wanalipatia ufumbuzi suala la kero ya kodi kwa wananchi wa hali ya chini kwa kupata muafaka ambao utasaidia pande zote mbili bila kukandamiza upande wowote iwe Serikali ama mwananchi wa kawaida.

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekuwa na rekodi nzuri ya ukusanyaji wa kodi ila kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuhusu kodi ambazo zimekuwa kero na hazina tija.

Hivyo Serikali imejipanga kuiongezea nguvu Mamlaka hiyo kwa kuipa uwezo wa kukusanya na mapato ambayo hayatokani na kodi toka katika wizara, mashirika, taasisi za serikali na Halmashauri zote nchini.
 
Inasikitisha kuona karne 21 bidhaa kutoka China zinamisamaha ya kodi!
 
Magufuli saidia nchi yetu, sijui watawala waliopita walikuwa na nia gani kwa nchi yetu mweeee
 
Angeeleza pia kwa nini mafuta, ememe n.k zina mlolongo wa makodi. kwani hizo nazo si kero? Usanii tu hamna issue
 
Kwa serikali hii tutasonga tu safi sana uongozi wa jpm tupo pamoja na wewe.
 
Itakuwa poa sana
Naona baada ya miaka 2 bajeti yetu haitakuwa tegemezi tena
 
SERIKALI inatarajia kuunda Mamlaka Kuu ya Mapato ya Taifa nje ya Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) iliyopo sasa, kuondokana na malalamiko ya kero za kodi kwa wananchi wenye kipato cha chini.

Aidha, TRA imefuta kodi elekezi kwa bidhaa zinazoingizwa nchini kwa msamaha wa kodi hususani zinazotoka China, hivyo wafanyabiashara waliokuwa wakinufaika na fursa hiyo, watatakiwa kuanza kulipa kodi.

Hayo yalielezwa jijini Dar es Salaam jana na Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari. Akizungumzia mamlaka mpya itakayoanzishwa, alisema hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali kusaidia wananchi wa kipato cha chini, kumudu kulipa kiwango cha kodi kinachowekwa na mamlaka hiyo.

“Napenda kuwaambia umma wa Watanzania kwamba Serikali ya Awamu ya Tano inawajali watu wake na ndiyo maana imeona kuwa kuna haja ya kuunda mamlaka moja ya utozaji wa kodi itakayojumuisha taasisi zote zinazohusika na kukusanya mapato nje ya kodi na ushuru ili kuondokana na malalamiko mengi ya wananchi juu ya utozaji wa kodi hasa katika halmashauri zetu,” alisema Kidata.

Kamishna Kidata alisema katika dunia, hakuna serikali ambayo imechaguliwa na wananchi ikaamua kuwakandamiza wananchi wake . “Hivyo basi kwa sasa serikali ipo katika mchakato wa kuunda mamlaka hiyo ambayo itasaidia kuweka viwango vya kodi ambavyo wananchi wa hali ya chini watamudu kulipa kutokana na biashara au kazi wanazozifanya,” alisema.

Kamishna huyo alisema mamlaka yake kwa kushirikiana na mamlaka nyingine, zinazokusanya kodi katika halmashauri nchini, watahakikisha wanapatia ufumbuzi kero ya kodi kwa wananchi wa hali ya chini kwa kupata muafaka, ambao utasaidia pande zote mbili bila kukandamiza upande wowote ama Serikali au mwananchi wa kawaida.

Ingawa TRA imekuwa na rekodi nzuri ya ukusanyaji wa kodi, kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuhusu kodi zinazodaiwa kuwa za kero. Akizungumzia kufutwa kwa kodi elekezi kwa bidhaa zinazoingizwa nchini kwa msamaha wa kodi, Kaimu Kamishna Kidata alisema awali, kulikuwa na punguzo la kodi kwa wafanyabiashara wanaoagiza na kuingiza bidhaa kutoka China kwa kupunguziwa sehemu ya kodi.

“Tumeamua kuondoa kodi elekezi kwa sababu haina faida kwa taifa letu kwani inawanyima wafanyabiashara wengine ambao hawaagizi bidhaa kutoka China, fursa ya kushindana kibiashara.
Excuse me bwana Kamishna! Labd a sikukuelewa vizuri .Umesema hakuna serikali inayochaguliwa na wananchi na baadae ikawakandamiza wananchi wake! Are you sure? Ile serikali ya awamu ya nne ilitufanyia nini kama sio kutukandamiza!
 
Unajua awamu ya Kikwete haikuwa na ubunifu wowote.
ubunifu ulikuwepo mzee kila mtu na tumbo lake yaani amna hata MRADI mmoja wa serika ya awamu ya 4 HAUKUFANYWA DILI daraja la kigamboni bei imeongezwa kuto 160B mpaka 260B , mabehewa , BOMBA la ges japo watu hawasemi ukweli , kinyerezi Ina II mabarabara ndio usiseme tena
 
Mamlaka kuu na mamlaka iliyopo vitakuwa na utofauti gani?

Na bado sijaelewa kwanini haiwezekani kushughulikia matatizo ya kodi kwa makundi maalumu kwa kutumia mamlaka iliyopo mpaka kiundwe chombo kingine?
 
Itakuwa poa sana
Naona baada ya miaka 2 bajeti yetu haitakuwa tegemezi tena
ata miaka mia moja kwa serikali hii na chama hiki hiki tutaendelea kuwa tegemezi kwa sababu taifa bado linamahitaji mengi acha ufinyu wako wa kufikiri huo
 
hii ndo serikali ya wananchi sio kama ile serikali ya viongozi chini ya mswahili
 
Inasikitisha kuona karne 21 bidhaa kutoka China zinamisamaha ya kodi!
Pia inasikitisha kuona karne ya 21 mtu mzima Kama wewe bado haujui ya kwamba "zina misamaha" ni maneno mawili katika sentensi na sio "zinamisamaha" Kama ulivyoainisha hapo juu.
 
Naona nchi ilikuwa ishauzwa kwa mchina. Sijui JK alipewa nini na hao jamaa.
 
Back
Top Bottom