Serikali kuufunga uwanja wa Taifa!

Deo Corleone

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2011
Posts
17,048
Reaction score
13,495
NI KUTOKANAa NA TABIA YA KIJINGA YA MASHABIKI KUHARIBU VITI. PIA WATAANGALIA ADHABU YA TIMU KUCHEZA BILA MASHABIKI KAMA ITAFAA.
TFF WAMEKUBALI KULIPA FIDIA YA UHARIBIFU ULIOTOKEA KATIKA MECHI YA KANDAMBILI NA AL AHLY.
CHANZO:TBC TAIFA.
 
Wafunge tu ,ubaki wa kuhudhuria sherehe za kitaifa tu.
 
Kama hospitali hakuna dawa,watoto wanakaa chini, kanuni zimechukua wiki tatu ukifungwa uwanja kitauma nini zaidi!!!??????

Hata ubomolewe kabisa!!!!
 
Safi sana kila timu itafute uwanja wake na uwanja wa taifa usubiri mambo ya kitaifa tu hata nchi za wenzetu zinafanya hivyo, hatuwezi kuwachekea mashabiki vichaa
 
NI KUTOKANAa NA TABIA YA KIJINGA YA MASHABIKI KUHARIBU VITI. PIA WATAANGALIA ADHABU YA TIMU KUCHEZA BILA MASHABIKI KAMA ITAFAA.
TFF WAMEKUBALI KULIPA FIDIA YA UHARIBIFU ULIOTOKEA KATIKA MECHI YA KANDAMBILI NA AL AHLY.
CHANZO:TBC TAIFA.

kazi kwao magoti fc na mkia fc
 
Kama hospitali hakuna dawa,watoto wanakaa chini, kanuni zimechukua wiki tatu ukifungwa uwanja kitauma nini zaidi!!!??????

Hata ubomolewe kabisa!!!!

Unaonesha wazi kuwa wewe ni mmoja ya wanaoharibu uwanja.

Nani alikwambia hospitali hakuna dawa? Kikwete katunyanyua toka miaka 48 (life expectancy) mpaka 62 kwa miaka 8 tu. Wakati wa nyerere hata 40 ilikuwa muhali.
 
Unaobesha wazi kuwa wewe ni mmoja ya wanaoharibu uwanja.

Nani alikwambia hospitali hakuna dawa? Kikwete katunyanyua toka miala 48 (life expectancy) mpaka 62 kwa miaka 8 tu. Wakati wa nyerere hata 40 ilikuwa muhali.

Kuna masuala ya kubishana sio haya!!!!!!!!
Kaa dukani uza hapo bi mkubwa sie watu wa field tunayaona na kuumia zaid ya maneno ya mdomoni!!!!!!!!
 
Sawa ichezee taifa stars tuu

tatizo litabaki palepale kwasababu hata ikicheza timu ya taifa wanaoenda mpirani ni wale wale.
hivi wale waliojisaidia kwenye masinki ya kunawia mikono si ilikuwa timu ya taifa?
 
askari police wawe wanatizama mashabiki na si muda wote wanatizama mechi.
 
Ni jambo jema, washabiki wa soka hawana uzalendo,
 
Simba, Yanga na timu zingine zijenge viwanja vyao
 
Kuna masuala ya kubishana sio haya!!!!!!!!
Kaa dukani uza hapo bi mkubwa sie watu wa field tunayaona na kuumia zaid ya maneno ya mdomoni!!!!!!!!

Tatizo lenu mna compare na wakati upi? wakati leo hii kila nyanja ya afya tuko mbele kuliko wakati wowote ule, sisemi tumefika au tumefikia tunapostahili, lakini kumbuka uozo uliowachwa na Nyerere, Mwinyi na Mkapa kwa miaka 44, Wametuwacha hohe hahe, leo at least tumepata japo matumaini kwa kupunguza vifo vya watoto na kina mama na kutupaisha "life expectancy" yetu kuliko wakati wowote wa kabla ya Kikwete. Hiyo pekee ni achievement kubwa sana.

Jee, unajuwa kuwa tunaweza leo kutatuwa matatizo mengi kiafya kuliko wakati wowote ule wa kabla ya Kikwete?
 
Bora ufungwe maana kila siku uharibifu tu halafu hakuna adhabu itolewayo kwa wale wanaoleta uharibifu.Zaidi ya yote mamilioni yanayopatikana haifahamiki yanakopelekwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…