Serikali kuu ya Marekani yafungwa

Serikali kuu ya Marekani yafungwa

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2012
Posts
12,320
Reaction score
11,345
Serikali kuu ya Marekani imefungwa huku zikiwa zimebaki zaidi ya saa moja tu, zilihitajika kura zaidi ya 60% lakini kura zilizopigwa ni 49% tu, wabunge wa Democratic wameshindwa kuafikiana ...Rais wa Marekani Donald Trump aliakhirisha safari yake ya kwenda mapumzikoni huko Florida akisubiri baraza la seneti kuidhinisha mswaada wa muda wa matumizi ya fedha.

Rais Trump alipangiwa Jumamosi kuhudhuria harambee ya chakula cha usiku kuadhimisha mwaka mmoja wa urais wake lakini huku kukiwa na wasi wasi wa kuidhinishwa mswaada wa matumizi ya fedha na bunge, maafisa wa White House walisema rais ataendelea kuwepo Washington akisubiri suluhisho la bajeti ili kuepuka serikali kuu kufungwa.


Mkurugenzi wa ofisi ya utawala na bajeti Mick Mulvaney alisema Ijumaa nafasi ya kufungwa kwa serikali kuu ilikuwa “nusu kwa nusu” baada ya nafasi ya ushindi wa uungaji mkono wa kutosha kutoka Democrat kwa hatua iliyoonekana kupunguza makali ya kufungwa kwa serikali kuu.

“Tulikuwa tuna endesha shughuli chini ya kama asilimia 30 ya kufungwa kwa serikali kuu hadi Alhamis, ninafikiri hali imeongezeka hivi sasa” Mulvaney aliwaambia waandishi wa habari huko White House. “Tulikuwa na mkutano wetu kiasi cha nusu saa iliyopita, mkutano kwa njia ya simu na idara mbali mbali ili kuwaambia waanze kutekeleza mipango yao ya sera katika hatua ijayo ya kujiandaa na ukosefu wa fedha wakati serikali kuu inafungwa”.

Mkurugenzi wa bunge katika White House, Marc Short aliwaambia waandishi wa habari kwamba Rais Trump alipiga simu Ijumaa ili kujaribu kuzungumzia suala hilo lakini hakusema rais alimpigia nani. “Tunajaribu kuhakikisha serikali inaendelea kuwa wazi” alisema Short.


Mswaada uliopitishwa na bunge utaisaidia serikali kuwa wazi na kuendesha shughuli zake hadi Februari 16 lakini baraza la seneti lilimaliza siku bila ya upigaji kura hatua ambayo ingepelekea kuwasilisha hatua za muda za matumizi ofisini kwa rais.

Katika ujumbe alioandika Rais Trump Ijumaa asubuhi alikiri kwamba kura za Democrat zinahitajika kupitisha hatua hiyo lakini alipendekeza madai ya wademocrat ya kulinda suala la uhamiaji yataweza kuchelewesha fursa ya kupitisha mswaada huo na kupelekea serikali kuu kufungwa.

Madhara yatakayopatikana mojawapo ni zaidi ya wafanyakazi wa serikali 850,000 kurudi nyumbani na kutolipwa mishahara, pia huduma nyingi kufungwa hadi hapo suala hili litakapomalizika ama kupatiwa ufumbuzi.

MY TAKE: Tunajifunza nini kwa mabunge ya afrika haswa yenye wabunge wengi wa CHAMA TAWALA? Na pia marais wa afrika haswa wale wanaominya demokrasia na kuingilia mihimili ya kibunge wanajifunza nini ?

capitol_hill_4.jpg
 
Hakuna la kujifunza...hapo ni style yao na haituhusu
 
Baada ya tisho la kufungwa nini kinafuata?

Na je ikifungwa kunakuwa na madhara gani
 
Back
Top Bottom