Hebu soma tena,,,serikali ya jamuhuri ya muungano wa tanzania,,,it means ni serikali ya shirikisho wa nchi,zaidi ya moja,iwe mbili au tatu ndio ikaitwa muungano,sasa sisi tuna serikali mbili ambazo zilijipatia uhuru mwaka 1961 ambayo tanganyika na zanzbar 1964,na ndipo zikaungana,baada ya muungano ilikuwa tunaita hivi Jamuhuri ya muungano wa tanganyika na zanzibar.
Baada ya hapo ilitumika technic ya kuimeza zanzbar ndani ya muungano na kuiyuwa tanganyika na kuita tanzania tukapakiwa na serikali ya muungano ambayo ni tanganyika kuita tanzania na ikabakia zanzbar, Ni sawa zaire kiuta congo, tanganyika/tanzania.
sasa watanganyika ikiwa nyinyi munataka kuwa serikali moja hilo haliwezikani kwa upande wa zanzibar,kwani sisi ni taifa kamili tuna serikali yetu,na kila kitu chetu,haya ni maamuzi yetu,na hatuko tayari kuuza utaifa wetu kwa kujimbambika jina la ubatizo la tanganyika ambalo ni tanzania,sisi ni wazanzbari sasa inafika miaka 500 zanzibar ipo.
Sasa ikiwa wewe umependezewa na jina la tanzania jite mtanzania,lakini sisi wazanzbari tunafahamu kuwa tanzania ni ile tanganyika kilichobadilika ni jina tu,kwanza muungano hatuna,kwani mshiki wa muungano amekufa,ni sawa na ndoa mke kufa kubakia mume,hakuna ndoa tena.
Pia katika makubaliano ya muungano,rais wa zanzbar ndio anatakiwa awe makamo wa rais wa muungano kwa sababu yeye amechaguliwa na wanachi wa zanzibar kwa hiyo naweza kuwakilisha wazanzbari katika muungano,sasa jiulize Doctor Bilal amechaguliwa kichama ndio kawa makamo wa rais wa muungano vipi anaiwakilisha zanzibar ? Wakati hakuchaguliwa na wanachi ?
Kwa kweli vile vizingiti vya muungano ambavyo vilivyofanya muungano uwepo havipo na muungano umekufa,sasa muungano hakuna,uliokuwepo ni muungano wa chama tu,ASP na TANU ambayo ni ccm.
hii symbol ukiangalia ni ile ile ambayo ikitumika kwa serikali ya tanganyika leo tunaambiwa tanzania,sasa jiulize tanganyika sio hii tanzania ?
Nembo hii ndio ilikuwa ikitumika kwa tanganyika sasa inatumika kama ni ya tanzania,ni sawa zaire kuita congo,utapeli tu,nani alosema tanganyika haipo ? Ipo tanganyika,rasilimali kama migodi,almasi,mafuta na gasi,sio ya muungano sasa jiulizeni yanasimamiwa na serikali ipi ? Na pesa hizo za umma zinakwenda wapi au wanagawana viongozi ? Amkeni nyinyi.
hii nembo sasa imekuwa ya tanzania,jiulize huu sio usanii ?
View attachment 32914 na hii ndio ilivyokuwa baada tu ya muungano tukitambulika kimataifa angalia hiyo ramani ...Balozi zetu zilikuwa zikiandikwa jamhuri ya muungano wa tanganyika na zanzibar.
Sisi wazanzibar tunasema tena hatutaki hatutaki muungano,kwa sababu hauna jema kwetu,hauna fadhila,unatudhulumu sisi,na nyinyi watanganyika kama munaona ni mzigo kwenu basi bora iwe end.