Serikali kutumia magari ya kawaida kwa shughuli zake imeishia wapi?

Majighu2015

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
2,936
3,958
Wadau,

Kama mnakumbuka katika serikali iliyopita ya Rais Kikwete, Waziri Mkuu wa kipindi hicho Mh. Pinda alianzisha mchakato wa Serikali kuanza kubana matumizi na kuanza kutumia magari ya kawaida kama RAV 4 n.k ambazo zina gharama ndogo za kutumia na ulaji mafuta pia. Kwa sasa Serikali inatumia sana magari aina ya Nissan, V8, Prado, land cruiser ambazo gharama zake za kuziendesha ni kubwa.

Hili swala sijui limeishia wapi na kama Serikali ya sasa italiona hili na wakiamua kubadilisha hizi gari zilizopo kwa sasa wataweza ku-save fedha ya kutosha ambayo ingeweza kutumika katika shughuli nyingine za kimaendeleo.

Wadau mna mawazo gani kuhusu hili swala?
 
Mkuu aliwashangaa maEngineer kwenda kukagua miradi na maV8 badala ya pick ups, ngoja tusubiri huenda tukafika huko, Mkuu seems to be seriousoo! Ikechukwu
 
Kama tutaamua kutumia magari gharama nafuu itachukua mda kwakua tayari tunayo magari yaliyopo sasa ambayo ni ya gharama kubwa kiuendeshaji lkn pia bado mpya na sijui km tuliagana yauzwe ili tununue hayo gharama nafuu itawezekana.
 
Nilitegemea SANA Kwenye bajeti ya mwaka huu kuona MABADILIKO makubwa Kwenye matumizi ya Magari lkn ikawa KIMYA .
 
Hivi mnajua barabara za Tanzania au mnasikia tu. Na unaposema yanagharama kubwa kuendesha umesha kokotoa kujua tofauti ya running cost za gari kama RAV 4 au Landcruiser V8. Umewahi kupeleka gari dogo service Toyota ukaona ina cost shs ngapi? Msilinganishe na service za uchochoroni, standard service za gari kwa authorised dealer ni expensive hata kama gari ni dogo.

Hapa mnaongea kwa hisia za kimasikini na roho ya kwanini. Umewahi
 
Mkuu aliwashangaa maEngineer kwenda kukagua miradi na maV8 badala ya pick ups, ngoja tusubiri huenda tukafika huko, Mkuu seems to be seriousoo! Ikechukwu
Ngoja tusubiri tuone..Ila haya magari ni shidaa tu
 
Hivi mnajua barabara za Tanzania au mnasikia tu. Na unaposema yanagharama kubwa kuendesha umesha kokotoa kujua tofauti ya running cost za gari kama RAV 4 au Landcruiser V8. Umewahi kupeleka gari dogo service Toyota ukaona ina cost shs ngapi? Msilinganishe na service za uchochoroni, standard service za gari kwa authorised dealer ni expensive hata kama gari ni dogo.

Hapa mnaongea kwa hisia za kimasikini na roho ya kwanini. Umewahi
Mkuu nchi za wenzetu hawatumii gari kama za kwetu. Serikali zao zinajua gharama za kuendesha magari ya aina tuliyo nayo. Usifananishe V8 na Rav4 kwenye maitanance na ulaji wa mafuta. Barabara inayopita v8 na Rav4 inapita. Halafu hawa wakubwa wenye haya magari unakuta mds mwingi sana wapo kwenye lami tu.
 
Issue sio ulaji wa mafuta. Kuna issue za uwezo wa gari pia.
Unaweza ukabana matumizi ya mafuta, lakini ukasahau kwamba, uwezo wa kubeba abiria, uwezo wa kustahimili (durability) ni vigezo pia. RAV 4 ina Sifa pungufu ya hizo ukilinganisha na Land Cruiser (Prado, V8 n.k.)
 
Kama tutaamua kutumia magari gharama nafuu itachukua mda kwakua tayari tunayo magari yaliyopo sasa ambayo ni ya gharama kubwa kiuendeshaji lkn pia bado mpya na sijui km tuliagana yauzwe ili tununue hayo gharama nafuu itawezekana.
yanauzwa kunawanunuzi wengi sana kitaaa,,tena magari yao mazuri coz yanaagizwa km 1
 
Back
Top Bottom