Serikali kupitia Waziri Mwijage wamjibu Dangote: He is not aware with the pre existing laws!

Namshangaa waziri Mwijage kwa kutokuelewa ushauri wa Dangote - tena wa bureee. Dangote lazima anawafahamu wawekezaji ambao wamwemwendea wakitaka kujua experience yake ya kuwekeza TZ na vile vile wakaonyesha kusita kwao kuwekeza TZ. Hata kama matamshi ya serekali yanakuwa matamu kiasi gani, wawekezaji binafsi wanataka kupata experience ya mwenzao aliyeko on the ground. Kwa hiyo tahadhari ya Dangote siyo ya ku- brush aside eti kuwa hajui sheria za TZ
 
Kwani ni lazima akaongelee Uingereza.

Kwani alishindwa kuonana na Waziri husika akampatia huo ushauri?

Tatizo la wenye mapesa ni kuwa na dharau na wenye mamlaka,hili ni tatizo kubwa ktk Afrika.

Kwa hiyo ameenda kutushitaki kwa Bwana Mkubwa?

Ama kweli vita ya uchumi hata wale uliowatengenezea mazingira mazuri wanaweza kukuzunguka.

Kuna kitu si bure,why the financial times and not the citizen/The East Africa/The guardian?

Next time time hakuna haja ya kumjibu,ni kumuita aeleze yote anayodhani ni muhimu kwa yeye na sio yeye kujifanya wakala wa wawekezaji.
 
Waziri badala ya kwenda kumjibu huko huko anatujibu sisi sasa atasikiaje na hao aliowaambia kimataifa wamesikia alichosema waziri.Jamani to act professional.Dogote sijui nani ,he is smart yeye kaongelea kimataifa Je kulikuwa hakuna Waziri au mtanzania aliyekuwa kwenye huo mkutano naye amjibu.Najiuliza tu la sivyo jamaa anasema kweli sisi tunasemea huku nchini wananchi wa kawaida watusikie kwa ajili ya kura.Jitadhmini Jamani
 
Wewe ndio hujaelewa...naamini kama mwekezaji pindi unapopata shida yoyote milango ya majadiliano na Serikali iko wazi sana na hiyo ni moja ya mazingira bora ya uwekezaji Hasa Nchini Tanzania.

Pamoja na kuwa sheria za Rasilimali zimebadilika lakii siamini kwamba zimeigeuza Tanzania kuwa Rigid dhidi ya wawekezaji.

Dangote ameenda mbali kutoa generalised comment ambayo inaweza kuathiri uwekezaji...ni vyema akatambua kuwa alichokitenda sio uungwana especially kwa yeye ambaye ni mwekezaji anayependelewa.

Sera zetu za uwekezaji ziko wazi na zinatabirika na hata hivyo tuna wajibu wa kuzirekebisha muda wowote pindi tunapoona mikataba haiko sawa na tunapoteza badala ya kufaidika.
Ikumbukwe wanaolilia mikataba yenye maslahi kwa pande mbili ni wananchi wanyonge wasio na huduma za afya na wala sio kwa maslahi ya Magufuli.

Uwekezaji unatakiwa kuwa na sera za kitaifa,yani tutakazokubaliana wote zisiwe sera za Rais aliepo madarakani maana itakuwa kila anaeingia anakuja na mambo yake hili ni tatizo kwa wawekezaji wakubwa aina ya DANGOTE ambao wanawekeza miradi ambayo kuanza kupata faida inaweza kuwachukua miaka hadi kumi baada ya kuwekeza.

Watu aina ya DANGOTE mnakosea sana nyie wapigadebe wa serikali hii na uongozi wa awamu hii kuwachukulia kama wapiga dili maana tatizo ndio linapoanzia kufikiri kila mfanyabiashara ni mpiga dili.mtu kama Dangote anachoangalia cha kwanza ni SOKO,soko lilikuwepo na bado lipo.

Cha pili ni malighafi na nishati,swala la nishati alihakikishiwa ipo ya kutosha hasa gesi lakini kilichokuja kutokea ni kinyume kabisa.na kumbuka huyu mtu ana uzoefu wa kuwekeza katika nchi mbalimbali kwahiyo anayoyasema yawe changamoto ya kutusaidia kutatua matatizo yaliyopo katika sekta hiyo na sio kuanza kubishana nae.
 
Huyo aliingia nchini kwa kuunga unga na feva za waliopita.. atulie aheshimu ya awamu hii na kuelewa sionya wapiga madili kumpa vya mkato mkato kama zamani.
kama kawaida yako mzee wa pointless...Jitahidi ujibu hoja apo sio siasa za majibu mepesi mepesi...
 
mi naona hao wawekezaji waondoke ili tuone sasa hizo kodi mtakusanya kwa kina nani....
kila mtu akiamua kulima mboga zake, akasaga mwenyewe unga wake, nguo asinunue mpya sijui mtapata wapi hela nyie mafisi
Na ruzuku ya CHADEMA itatoka wapi? Au mkuu una hadithi ile unakata mtawi uku umeukalia.
 
Sheria za uwekezaji hazijabadilishwa sioni sababu ya yeye kulalamika ukizingatia tangu anafanya investment zake sheria ni zile zile angelalamika before ya ku invest sawa.
Ndio hapo sasa inavyoonekana sheria zinafuatwa kikamilifu hamna loophole anaanza kulalamika
 
Dangote lazima afahamu kwamba katika uwekezaji kuna changamoto na lazima kuji - tune juu ya namna ya kukabiliana nazo (risk bearing). Anapaswa kufahamu kwamba mambo ya jana si ya leo na hivyo ajipange namna ya kwenda na wakati.
 
Sio jambo zuri kwa dangote kutuharibia promo Tz kuhusu wawekezaji huko kwenye media. Na yeye kama public figure katika uwekezaji africa inawagusa na kuwaogopesha hata wawekezaji wengine.

Ila kama hilo 16% interest ya kampuni inachukuliwa na serikali basi hakuna budi serikali iyapokee, ichunguze kwenye uwekezaji wa wengine kuna changamoto kama hayo ili waweze kuyafanyia kazi. Ila naye achunguzwe kama anaficha faida halisi anayoipata.

Uwekezaji ni zaidi ya serikali kupata kodi na tozo zingine, bali ajira, kipato, uchumi na maendelo ya nchi yanakuwa.
Iyo 16% si ilikuwepo au mheshimiwa rais kabadilisha kwenye utawala wake?

Uyu jamaa tapeli tu
 
Huyo Mwijage naye ni wale wale...mtu Kiswahili hajui na Kiingereza hajui. Kwa kweli tumetoka kapa awamu hii. Dangote is not aware with..., duh!
Umemuona kaongea ivyo au gazeti ndio limeendika kiingereza kibovu?
 
Huyo aliingia nchini kwa kuunga unga na feva za waliopita.. atulie aheshimu ya awamu hii na kuelewa sionya wapiga madili kumpa vya mkato mkato kama zamani.
Akili ndogo ,kama yako,haiwezi kuelewa akili kubwa!

Dangote ameshauri vizuri. Kwa hizi sera na utamaduni ambao tumeanza kutumia,tutakwama tu! Ni suala la muda tu! Mtatafuta vibwagizo vingine. Tatizo ni kwamba,nchi yetu na wananchi wote,tutalipa gharama ya ujinga wenu!
 
Kitendo cha Dangote kuisema Tanzania kuwa ina sera mbovu za uwekezaji kwenye huo mkutano wa watu wenye pesa zao AMETUJERUHI VIBAYA SANA wenye akili wanaelewa matokeo tutayaona.
 
Mmetuharibia nchi na hata kile kidogo kilichokuwepo mnataka kukikimbiza, hivi mnataka sisi tuishije kwenye hii nchi?
mnataka tuwe kama zimbabwe ndio mfurahie?
naanza amini kuwa mapato yamepungua san ahadi aibu mnaona kuyatangaza
Ulizoea kuishi kwa kudanganywa na pipi kama mtoto mdogo. Pole sana.
 
Dar es Salaam. The minister for Industries, Trade and Investment Charles Mwijage has defended the government against accusations made by Mr Aliko Dangote that President John Magufuli’s policies scare away investors.

Mr Mwijage told The Citizen on Monday that the government’s investment policies are clear, transparent and aimed at ensuring that the government also benefits from the country’s resources.

In an article published by the Financial Times on Monday Mr Dangote, a major investor in Tanzania, was quoted as saying that the government has pursued policies that seek to “seize a majority share of assets.”

“They have scared quite a lot of investors and scaring investors is not a good thing to do,” Mr Dangote told the Financial Times Africa Summit in London on Monday, according to Financial Times.

Dangote, who own a $600 million (Sh1.3 trillion) cement factory in Mtwara, specifically mentioned a “backdoor plan” by the government to take up to 16 per cent of an investor assets for free.

But Mr Mwijage clarified that the “free carried interest” is a requirement for companies operating in the extractive industry that had existed in Tanzanian laws even before the recent review of laws.

“Investors in the extractive industry are obliged to seize16 per cent free carried interests to the government to ensure the country benefits from the natural resources,” Mr Mwijage said, adding; “I really expect Mr Dangote as one of major shareholders in the country to be conversant with our laws. Once a company comes and invest in the extractive sector, the government shares should not be less than 16 free carried interests. This is not wrong at all as the natural resources are ours,” Mr Mwijage told The Citizen in an interview with The Citizen.

Even as he insisted that the government will make sure that all investors in the country are abiding by the country’s laws, Mr Mwijage said he did not believe that Mr Dangote would be the one to castigate the country’s investment climate in the negative manner.

This, Mr Mwijage noted, was due to the “special attention” in which the Nigerian investor receives from the Tanzania government in his Dangote Cement factory.

“Dangote has not had any problems here. Whenever he encounters any difficulties the whole government rushes to his help. You remember when he had issues last year we were all available to help his cement factory,” Mr Mwijage noted.

In the Financial Times article, Mr Dangote was quoted as advising President Magufuli to “have a look at” his policies.

Chanzo:Citizen.

My Take :Kweli Dangote kakosa shukrani kwani kati ya investors waliowahi kupigiwa debe waziwazi na Magufuli basi ni Dangote tu...

Nimeamini kuwa nchi hii itajengwa na watanzania Wazalendo wengine wote ni wachumaji tu kwa manufaa yao.

I may agree with Hon Mwijage that probably Dangote was not conversant with pre existed Tanzania laws simply because in 2015 Dangote comments about Tanzania were as follows:
Serekali kwanini tuna endekeza rohooo ya kuomba kwani watanzania tuashindwa kuwekeza waache waondoke watazania milion hamsini atushindi North korea wemeweza je?
tuondoe hiyo mawazo ya kila kitu wazungu tu DANGOTE kahongwa ndio maana kasema hayo kwani yeye kaongezewa hiyo asilia 16 kwenye uwekezaji wake au anajitia loud speaker ya wachimba madini wenye hila au ana hisa huko ACACIA?
Watanzania tuamke tuache kutegemea kila kitu Mzungu tu Hata sisi tuna weza?
huku Congo wanako safirisha madini kila kukicha kuna wawekezaji? ENOUGH IS ENOUGH CARRY ON MR MAGUFULI SISI TUKO NYUMA YAKO
 
Nianze kwa kusema kuwa mwekezaji hawezi kuwa Dangote pekee!

Tumeshuhudia huo unaouita ni uwekezaji kuwa ni laana kwa Taifa...yaani kati ya mifano yote ya wawekezaji uliyoitoa hakuna asiye na sifa mbaya ya kulalamikiwa na watanzania.

Huo uwekezaji unaousifia kwa miongo zaidi ya miwili umeshindwa kutuondoa kwenye lindi la umasikini wa kutupwa lakini at the same time wawekezaji hao wamepiga hela ya kufa mtu na kutuachia mazingira mabovu yaliyochafuka na kuharibika.

Cha kushangaza uwekezaji huu wa kihuni unafanywa kwa Tanzania tu sio US au UK ...kule pamoja na masharti mengi husikii wakilialia.

Kwanza nashukuru na niweze kukupongeza kwa kujaribu kuwa walau na mawazo huru..

Ndugu yangu binafsi sijaona tatizo kwa wawekezaji ila nimeona tatizo kwetu, muwekezaji ni mfanya biashara anayehitaji faidi nyingi akipata urahisi, tumewapa wawekezaji urahisi nao wameutumia wametupiga. Jambo hili linahitaji akili kudeal nalo ili muwekezaji apate na mhusika mwenye ardhi apate, ndio maana tunakaa nao mezani kwanza na lugha ya sasa wanaita win win... Kuliwa kupo lakini kidogo na sio walivyokuwa wanatula na hata huko US na UK wanaliwa lakini kidogo nao pia wananufaika..
 
Kusema Dangote amewekeza mtaji wa $600m bila kufahamu sheria za nchi ni kuushangaza ulimwengu na kuonyesha sheria zetu ni popo, hazieleweki na hubadilika bila kuzingatia uwekezaji.

Mambo mengine si vema kukurupuka na kujibu kwa sababu wewe ni waziri husika. Gazeti tunalojibu ni Financial Times si Tanzania Daima.

Kilichopo ni kwamba investors wengi hukurupuka kuja nchini bila kujua au kujali sheria zilizoko zinasemaje. Sasa serikali inapoanza ku-enforce hizo sheria ndiyo investor anakurupuka.

Huwa tunadhani vilaza wa sheria wako serikalini tu lakini ukitembelea idara za sheria za wawekezaji huko nako kuna vilaza wa ajabu. Kwa nini attorneys wa Dangote hawakumweleza sheria zote atakazokumbana nazo.

Likishakuwa jambo la kisheriahata kama wewe ni upnzani huwezi kuipiga serkiali eti tu kwa sababu unaichukia.

Dangote akumbushwe sheria zilizopo na asikimbilie kulialia. Hata kwao Nigeria kuna sheria na anaziheshimu.

Na nyinyi mnaopiga kelele humu kama mnadhani Dangite kaonewa pelekeni bill of ammendment bungeni inayom-favour Dangote na si kubwatuka humu mitandaoni.

But Mr Mwijage clarified that the “free carried interest” is a requirement for companies operating in the extractive industry that had existed in Tanzanian laws even before the recent review of laws.
 
Kwani kiwanda kikiwa na thamani kubwa hakiwezi kuongia nchini kwa kuungaunga?
Mseme ninyi ndio mlimtapeli! yaani kwa akili zenu hela yote hiyo halafu mtu aje awekeze kimagumashi kweli!! Acheni ujuha CCM!
 
mumemuelewa Dangote?
hajazungumzia Kiwanda chake cha siment
na wala mwijage hakutakiwa kumjibu km Waziri wa Viwanda na Biashara
yeye kasema ni sera za Nchi (tafsiri yangu inataka kudhulumu hata huo uwekezaji kwani inataka 16%, hapo mtu ukikwama wanataifisha au kuchukua mali zote)
kuna wawekezaji wa almas wamenyang'anya almas /Kimberley
Acacia wamenyeng'anywa makanikia
kuna wawekezaji katika Mbuga za wanyama wamewekeza katika vitalu nk
Sera ndizo zinazolalamikiwa
 
Back
Top Bottom