barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,916
Serikali ya Tanzania ipo ktk mkakati wa kununua ndege kwa matumizi na safari za viongozi wa serikali ndani na nje ya nchi.
Ndege hiyo aina ya Embraer 190(E190) yenye hadhi ya VIP inatazamiwa kununuliwa toka nchi ya Morroco na Serikali ya Tanzania kupitia Wakala wa Ndege za Serikali (Tanzania Government Flight Agency)
Kama ndege hiyo itanunuliwa,basi itafanya TGFA kuwa na ndege 5 ikiwemo ile Gulfstream 550 iliyozua balaa.Juzi ktk ziara yake uwanja wa ndege inasemwa Dr Harison Mwakyembe alifanya ukaguzi kuangalia ubora wa ndege hiyo ambapo aliruka nayo toka Dar-Zanzibar-K'njaro-Dar.
Wakati haya yanatokea,inasemwa kuwa shirika la ndege Tanzania bado lipo taabani na linamiriki ndege moja tu aina ya DH8 inayofanya safari zake ktk mikoa ya Tabora,Kigoma,Mtwara na Hahaya-Commoro