bibikuku
JF-Expert Member
- Feb 16, 2011
- 832
- 495
WAZIRI wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka amesema leo ataeleza mafanikio ya Serikali katika kutoa ajira kwa vijana ikiwa ni siku moja baada ya Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa kusema tatizo hilo ni bomu linalosubiri kulipuka na kuliomba Kanisa Katoliki liisaidie kutafuta ufumbuzi.
Juzi, akitoa salamu katika sherehe za uzinduzi wa Jimbo Jipya la Kanisa Katoliki la Ifakara, Morogoro, Lowassa alisema: Nawaomba maaskofu katika miradi yenu mlipe kipaumbele suala la tatizo la ajira kwa vijana... wengi wanaohitimu elimu ya sekondari na vyuo wanakabiliwa na tatizo kubwa la ajira. Hili kama tulivyosema ni bomu linalosubiri kulipuka...
Akizungumza na Mwananchi jana kuhusu tatizo hilo la ajira, Waziri Kabaka alisema leo atoa takwimu za ajira zilitolewa na Serikali kwa vijana na kueleza kile ambacho Serikali imekifanya na kuendelea kufanya katika kushughulikia tatizo la ajira nchini.
MY TAKE; Mapambano aliyoyasema Lowassa kuwa yuko tayari na fit huenda ndio yanaanza sasa