Serikali kuipa ruzuku Benki ya Wanawake

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
SERIKALI imeahidi kuisaidia Benki ya Wanawake Tanzania (TWB), Sh bilioni mbili kila mwaka kama ruzuku, ili benki hiyo kuweza kuwafikia wanawake wengi wajasiriamali waweze kunufaika na mikopo inayotolewa na benki hiyo.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alipofanya ziara na Naibu Waziri Khamis Kingwangalla katika benki hiyo.
Waziri Ummy ameipongeza benki hiyo kwa kuwa na utaratibu mzuri wa kutoa huduma za kibenki hasa kwa akinamama, ambao ni wajasiriamali wadogo na wa kati waliosahaulika kwa muda mrefu katika kuwezeshwa na kupewa kipaumbele kwa wanawake kumiliki mali.
Alisema serikali kupitia wizara yake inaandaa mkakati mzuri wa kuipa nguvu benki hiyo ili iwe na matawi mengi ya kutoa huduma za kibenki hasa katika mikoa, wilaya na vijiji waweze kunufaika na mikopo katika benki hiyo.
Waziri huyo ameshauri kinamama na kinababa kote nchini kuchangamkia fursa hii ya benki ya wanawake kujikwamua kutoka kwenye umaskini.
Amezitaka taasisi za serikali na mashirika ya umma kufungua akaunti kwenye benki hiyo kwa kupitishia mishahara ya wafanyakazi wake ili kuiwezesha benki hiyo ya kizalendo kuweza kupiga hatua.
Ameahidi kutoa ushirikiano wa karibu kuisaidia benki hiyo mtaji ambao utaiwezesha benki kuweza kukabiliana na soko la ushindani kwenye taasisi za fedha.
Pia amepongeza juhudi za mikopo mbalimbali inayotolewa na benki hiyo ikiwepo viwanja vyenye hati ambapo akinamama wanaweza kutumia viwanja hivyo kama dhamana, wanaweza wakajenga nyumba na kuepukana na makazi holela.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Margaret Chacha, amesema ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa serikali inaonesha kuwa benki hiyo imepata hati safi ya hesabu na uendeshaji wa biashara kwa ujumla.
Ripoti hiyo pia iliainisha kwamba mwaka wa hesabu wa 2014, benki hiyo ilifanikiwa kutengeneza faida ya Sh milioni 141.
Mafanikio hayo yalichangiwa na ukuaji wa benki hasa kwa kupanua masoko yake ya mikoani, lakini pia kukuza na kuboresha huduma za benki kupitia mitandao ya Tehama.
Alisema ili kujiendesha kama benki kamili ya biashara, benki hiyo inahitaji kuongeza mtaji wake kufikia kiwango cha zaidi ya Sh bilioni 15 kilichoainishwa na Benki kuu ya Tanzania (BoT).
Mwanahisa mkuu wa benki ni serikali ya Tanzania kupitia ofisi ya msajili wa hazina, imekuwa ikiongeza mtaji wake mwaka hadi mwaka.
 
Another taxpayer's money wasted, we are braced for more tax burden in the near future. We are doomed.
 
Back
Top Bottom