Serikali kuichukulia hatua kali kampuni ya Halotel ikishindwa kutekeleza mkataba

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,563
21,665
1.jpg

Serikali imesema itachukua hatua kali kwa kampuni ya Halotel kama itashindwa kutekeleza makubaliano ya mkataba wa kusambaza huduma za simu na mtandao katika ofisi za Serikali katika kila Wilaya nchini kote.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa wilayani Maswa wakati akizungumza na watendaji wa sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mkoani Simiyu na kusisitiza kutoa ushirikiano unaostahili kwa kampuni hiyo.

“Makubaliano yetu kati ya Serikali na Halotel ni kuunganisha ofisi za Umma kwa mtandao zikiwemo shule tatu katika kila Wilaya, Hospitali, Mahakama na Ofisi za Polisi ili kuwezesha mkakati wa mawasiliano vijijini kutekelezeka”, amesema Prof. Mbarawa.

Waziri Prof. Mbarawa ameeleza kuwa ifikapo mwaka 2017 kila eneo hapa nchini litakuwa na huduma ya mawasiliano ya mtandao na kuwezesha wananchi wote kunufaika na huduma hizo.

Katika hatua nyingine Prof. Mbarawa amekagua Ujenzi wa Barabara ya Lamadi-Bariadi KM 71.8 na Bariadi-Maswa KM 49.7 na kuwapongeza makandarasi wanaojenga barabara hizo kwa kazi nzuri wanayofanya.

“Nawapongeza kwa kazi nzuri mnayoifanya, hakikisheni kazi yenu inauwiana na thamani ya fedha na kuhakikisheni wafanyakazi wazawa wanapewa kipaumbele katika kazi wanazoziweza na kupewa mikataba stahiki ya kazi wanazozifanya”,
amesititiza Prof. Mbarawa.

Aidha, Waziri Prof. Mbarawa amemuagiza mkandarasi anaejenga barabara ya Maswa-Mwigumbi KM 50.3 kuhakikisha nyumba zinazojengwa kwa ajili ya mkandarasi zinajengwa kwa ubora ili zitumike kwa muda mrefu.

“Nakuagiza Meneja wa TANROADS, hakikisha nyumba hizi baada ya mradi wa barabara kukamilika unazikabidhi kwa jeshi la polisi ili waweze kuzitumia kwa ajili ya makazi na ofisi”, amesema Prof. Mbarawa.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Bw. Eraston Mbwilo amemwomba Waziri Prof. Mbarawa kuelekeza nguvu za ujenzi wa ofisi na nyumba za watumishi katika mkoa huo.

Katika hatua nyingine, Mkuu wa Wilaya ya Maswa Bi. Rosemary Kirigini amemuomba Waziri Prof. Mbarawa kuwawezesha Wakala wa Majengo nchini (TBA) kukamilisha mradi wa Ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo unaojengwa sasa kwa miaka mitano ili kuipunguzia Wilaya hiyo adha ya kutumia jengo chakavu ambalo si salama hasa kipindi cha mvua.

Waziri Prof. Mbarawa pia amekagua Kiwanja wa Ndege kilichopo Mkoa wa Shinyanga na ofisi za Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) kiwanjani hapo na kusisitiza kuwa Serikali iko katika hatua za kuboresha uwanja huo kuwa wa kisasa ili kuvutia mashirika mengi ya ndege kutumiwa kiwanja hicho.

Waziri Prof. Mbarawa yupo kwenye ziara ya kukagua miradi ya ujenzi kwenye sekta za barabara, nyumba, viwanja vya ndege na mkongo wa taifa wa mawasiliano katika mikoa ya kanda ya ziwa ambapo ametembelea Wilaya za Busega, Bariadi na Maswa mkoani Simiyu.
 
asimamie Inavyotakiwa ili wasikiuke mkataba ila waanze kufanya mchakato wa kufufua TTCL baadala ya kukomaa tu na makampuni ya kigeni
 
You second me.

Badala ya kufufua TTCL waziri bila aibu anataka kuuza nchi kwa wavietnam kusambaza ndani ya offisi za serikali kazi ifanywe na kampuni ya nje sio shirika letu sijaelewa mimi
Bado upuuzo unaendelea Hii Nchi!!
 
Badala ya kufufua TTCL waziri bila aibu anataka kuuza nchi kwa wavietnam kusambaza ndani ya offisi za serikali kazi ifanywe na kampuni ya nje sio shirika letu sijaelewa mimi
Wewe unaakili sana. Hapo ni kukabidhi nchi kwa wageni.
 
Badala ya kufufua TTCL waziri bila aibu anataka kuuza nchi kwa wavietnam kusambaza ndani ya offisi za serikali kazi ifanywe na kampuni ya nje sio shirika letu sijaelewa mimi
Halotel.
Mzee wa Msoga huyo kaka.
Kampuni imekuja faster kuliko halafu ulishawahi kuona mtu anafanya finishing ya ghorofa kuanzia juu kuja chini ndiyo hawa jamaa. Wameanzia vijijini ndiyo wakawa wanakuja mijini
 
“Makubaliano yetu kati ya Serikali na Halotel ni kuunganisha ofisi za Umma kwa mtandao zikiwemo shule tatu katika kila Wilaya, Hospitali, Mahakama na Ofisi za Polisi ili kuwezesha mkakati wa mawasiliano vijijini kutekelezeka”,amesema Prof. Mbarawa.
 
Sasa wote waanzie mjini cc wavijijini ni nani atatujali? Huna akili
 
Badala ya kufufua TTCL waziri bila aibu anataka kuuza nchi kwa wavietnam kusambaza ndani ya offisi za serikali kazi ifanywe na kampuni ya nje sio shirika letu sijaelewa mimi
Kumbe anaijua!? Wemefika tu juzi na wameshalamba kamkataba na serikali!
Kwa vile hapa jukwaani kuna thread hata za mwaka 2008 basi basi nyie wekeni kumbukumbu za hawa jamaa na tutaambiana hapahapa Inshallah!
 
Dah hii nchi bana, hiyo tender ya kusambaza mawasiliano ilitangazwa lini na halotel walishinda lini? yani matumaini yanakuja afu yanakata tena. JPM ataweza kweli kutumbua jipu la Msoga kweli? Serikali itakua inawalipa kiasi gani hao halotel kwa mwezi kwenye hiyo package? Na vipi kuhusu TTCL kama wameweza kuwagawia makampuni ya simu inakuwaje washindwe kuunganisha ofisi za serikali. Daaaah am tireed kwakweli.
 
Sasa wote waanzie mjini cc wavijijini ni nani atatujali? Huna akili
Kibiashara zaidi mijini ndiyo kuna matumizi makubwa ya wanaotumia mawasiliano haya, so tulivyozoea ni kwamba wengi huanzia mijini then vijijini. Hapo ujiuluze huyu mvietinam gani mwenye jeuri hii hapa duniani.
Connect the dots.
Asante mwenyewe akili timamu.

Wako ktk utiifu, Asiye na Akili
 
“Makubaliano yetu kati ya Serikali na Halotel ni kuunganisha ofisi za Umma kwa mtandao zikiwemo shule tatu katika kila Wilaya, Hospitali, Mahakama na Ofisi za Polisi ili kuwezesha mkakati wa mawasiliano vijijini kutekelezeka”,amesema Prof. Mbarawa.
hivi Voda, tigo, zantel, airtel achilia mbali TTCL kweli hiyo miaka yote waliyokuwepo walishindwa kuingia huo mkataba!?
 
kwa mara ya kwanza mbarawa kachemka yani baada ya kuipa ulaji TTCL unatumika kuwabeba wavetinam waingize mawasiliano kwenye majengo ya serikali,?? aliyetuloga watz kafa tumebaki kama manyumbu tu.
 
View attachment 323673
Serikali imesema itachukua hatua kali kwa kampuni ya Halotel kama itashindwa kutekeleza makubaliano ya mkataba wa kusambaza huduma za simu na mtandao katika ofisi za Serikali katika kila Wilaya nchini kote.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa wilayani Maswa wakati akizungumza na watendaji wa sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mkoani Simiyu na kusisitiza kutoa ushirikiano unaostahili kwa kampuni hiyo.

“Makubaliano yetu kati ya Serikali na Halotel ni kuunganisha ofisi za Umma kwa mtandao zikiwemo shule tatu katika kila Wilaya, Hospitali, Mahakama na Ofisi za Polisi ili kuwezesha mkakati wa mawasiliano vijijini kutekelezeka”, amesema Prof. Mbarawa.

Waziri Prof. Mbarawa ameeleza kuwa ifikapo mwaka 2017 kila eneo hapa nchini litakuwa na huduma ya mawasiliano ya mtandao na kuwezesha wananchi wote kunufaika na huduma hizo.

Katika hatua nyingine Prof. Mbarawa amekagua Ujenzi wa Barabara ya Lamadi-Bariadi KM 71.8 na Bariadi-Maswa KM 49.7 na kuwapongeza makandarasi wanaojenga barabara hizo kwa kazi nzuri wanayofanya.

“Nawapongeza kwa kazi nzuri mnayoifanya, hakikisheni kazi yenu inauwiana na thamani ya fedha na kuhakikisheni wafanyakazi wazawa wanapewa kipaumbele katika kazi wanazoziweza na kupewa mikataba stahiki ya kazi wanazozifanya”,
amesititiza Prof. Mbarawa.

Aidha, Waziri Prof. Mbarawa amemuagiza mkandarasi anaejenga barabara ya Maswa-Mwigumbi KM 50.3 kuhakikisha nyumba zinazojengwa kwa ajili ya mkandarasi zinajengwa kwa ubora ili zitumike kwa muda mrefu.

“Nakuagiza Meneja wa TANROADS, hakikisha nyumba hizi baada ya mradi wa barabara kukamilika unazikabidhi kwa jeshi la polisi ili waweze kuzitumia kwa ajili ya makazi na ofisi”, amesema Prof. Mbarawa.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Bw. Eraston Mbwilo amemwomba Waziri Prof. Mbarawa kuelekeza nguvu za ujenzi wa ofisi na nyumba za watumishi katika mkoa huo.

Katika hatua nyingine, Mkuu wa Wilaya ya Maswa Bi. Rosemary Kirigini amemuomba Waziri Prof. Mbarawa kuwawezesha Wakala wa Majengo nchini (TBA) kukamilisha mradi wa Ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo unaojengwa sasa kwa miaka mitano ili kuipunguzia Wilaya hiyo adha ya kutumia jengo chakavu ambalo si salama hasa kipindi cha mvua.

Waziri Prof. Mbarawa pia amekagua Kiwanja wa Ndege kilichopo Mkoa wa Shinyanga na ofisi za Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) kiwanjani hapo na kusisitiza kuwa Serikali iko katika hatua za kuboresha uwanja huo kuwa wa kisasa ili kuvutia mashirika mengi ya ndege kutumiwa kiwanja hicho.

Waziri Prof. Mbarawa yupo kwenye ziara ya kukagua miradi ya ujenzi kwenye sekta za barabara, nyumba, viwanja vya ndege na mkongo wa taifa wa mawasiliano katika mikoa ya kanda ya ziwa ambapo ametembelea Wilaya za Busega, Bariadi na Maswa mkoani Simiyu.
Nina wasiwasi sana na uwekezaji wa wachina Tanzania! Hawa jamaa hawaheshimu kabisa utawala wa sheria utafikiri waliambiwa Tanzania ni coloni lao
 
Hivi halotel huyu ni jipu gani hili linaloanza kupanatrate kirahisi na kukubalika ndani ya serikali ya Magu huku TTCL ikichechemea??
 
Back
Top Bottom