Serikali kuhujumu wananchi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali kuhujumu wananchi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zhule, May 28, 2010.

 1. Z

  Zhule JF-Expert Member

  #1
  May 28, 2010
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 354
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Saudia Arabia wametamka wazi kwamba viwanda vyao vingi vinakosa malighafi kutokana na kukosa ardhi kwa ajili ya kilimo.

  Strategy yao ni kuja Tanzania kumilikishwa ardhi walime wasafirishe kwao. tayari wanafanya hivyo kwa mazao ya chakula na mafuta ya kupikia kule Ethiopia. Hali kadhalika China kila mwaka watu Milioni 60 wanazaliwa.

  Kila mwaka zaidi ya 400,000Ha za ardhi kwa ajili ya kilimo inatumika kujenga majengo mapya. Wameongeza juhudi kutumia sayansi na teknolojia ili ardhi kidogo izalishe zaidi. Hata hivyo ndani ya miaka 35-50 wanahitaji additional source of land kwa ajili ya kuzalisha chakula. Tayari wameanza kule msumbiji kuzalisha mbegu.

  Trend hii itakuwa hivyo kwa nchi nyingi tu kwani hatutegemei ardhi au mipaka ya nchi kuongezeka bali ni kupungua tu with time. Manufactured goods hatuwezi ku-export kwa sababu ya gharama za umeme, usafirishaji na ukosefu wa technologia na ubunifu. halikadhalika madini, gesi, mafuta hatuwezi kuchimba kwa sababu hatuna mitaji.Tatizo la wakulima wetu kwa muda limekuwa ni ukosefu wa masoko. Hili limesababisha hata mabenki kutowakopa ki urahisi kwa sababu mkulima hana uwakika wa kuuza.Dola inapanda kila siku kwa sababu tunahitaji dola ku-import goods wakati vitu tunavyouza nje vinapungua kila siku.

  Hatumtegemei msaudia kuongeza dola kwa sababu kila kitu mbolea, matrekta irrigation equipments, bank acounts n.k atatoka nazo huko kwao. Kwa nini basi wakulima wetu wasiwe source ya malighali za viwandani na chakula huko Saudia, china, iran na nchi zingine zitakazo hitaji badala ya wao wenyewe walime wasafirishe kwenda kwao?

  Africa na Tanzania in particular kwa nini tusi-export agricultural goods for the time being iwe ni -strategy ya serikali zetu wao watupe vifaa vya viwandani sisi tuwape malighali na chakula, this is would be win-win contract yes! Hii kilimo kwanza haina kipengele cha masoko? Mambo yanayovuka mipaka ya nchi kama hili la soko liko nje ya uwezo wa wakulima, lipo ndani ya serikali.

  Serikali inafahamu vyema kwamba hata raia na vifaa vya kichina, Saudia, India kujaa humu nchini si kwa sababu ya juhudi za wafanyabiashara na viwanda vya nchi hizo bali ni kwa sababu ya serikali zao kuwekeana mikatapa na sisi kununua kwao au wao kuchukua natural resources zetu na kutupa mikopo nafuu au misaada. Je serikali linakwepa jukumu lake muhimu kwa wakulima/wananchi wake?

  Lipi lililo bora wapewe pembejeo milele huku wakikosa soko au wapewe soko la uhakika mabenki yawakopeshe wajitegemee? Huku si CCM au serikali kuhujumu wananchi wake?
   
Loading...