Serikali Kufupisha Miaka Ya Kusoma; Kupatia Chakula | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali Kufupisha Miaka Ya Kusoma; Kupatia Chakula

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by X-PASTER, Jun 3, 2011.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Jun 3, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160


  Serikali imesema iko katika mchakato wa kuandaa Sera Mpya Elimu itakayofupisha muda wa kusoma.

  Sera hiyo mpya inapendekeaza muda wa kusoma kwa shule za awali kuwa wa kipindi cha mwaka mmoja wakati wa shule ya za msingi utakuwa wa miaka sita badala ya saba.

  Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua kongamano la wiki ya Elimu na kuzindua Shahada ya Uzamili ya Elimu katika Shule Kuu ya Elimu, Chuo Kikuu cha Dares Salaam, ambalo limeenda sambamba na maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa chuo hicho alisema, “Tuko katika mchakato wa kuandaa sera hii ambayo katika elimu ya shule ya awali mwanafunzi atakuwa anasoma kwa kipindi cha mwaka mmoja yaani akiwa na miaka mitano,atakapofika umri wa miaka sita ataanza elimu ya darasa la kwanza kwa muda wa miaka sita.”

  Akizungumzi a kuhusu maendeleo ya elimu , katika kipindi hicho cha miaka 50 Waziri Mulugo alisema Tanzania imepiga hatua nzuri na kuna mafanikio, ambayo, ubora wa elimu , idadi ya walimu imeongezeka pamoja na wanafunzi.

  Alisema serikali inaendelea kuzifanyia kazi changamoto zilizopo katika shule, zikiwemo kuongeza idadi ya walimu na vifaa vya maabara.

  Waziri Mulugo aliipongeza shule hiyo kwa kuanzisha shahada hiyo kwa kuwa itawezesha watu wengi waishio Dar es Salaam na Pwani kupata muda wa kujiendeleza kielimu wakati wakiendelea na kazi.

  Mhadhiri wa shule hiyo Profesa Justinian Galabawa alisema ni muhimu kwa walimu kujieleza kiujuzi ili waweze kuwa na taaluma bora kama ilivyo katika nchi za Cuba na Korea, “ Walimu wanatakiwa kukubali kujifunza kuliko wanafunzi, pia watakiwa kupatiwa elimu ya kuweza kuwa mameneja ili waweze kumenejimenti rasilimali za shule” (habari imeandikwa na Magreth Kinabo- Maelezo via FullShangwe blog).

  Na kutoka Selina Wilson/gazeti Uhuru: Serikali inaandaa mpango maalumu utakaowezesha wanafunzi wote wa shule za msingi nchini kupatiwa chakula cha mchana shuleni.

  Mpango huo unatarajiwa kuingizwa kwenye bajeti ya mwaka ujao wa fedha wa 2012/2013, ili kuziwezesha halmashauri kuanza utekelezaji.

  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa akitoa taarifa kwa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii jana alisema hatua hiyo inatokana na mafanikio yaliyopatikana katika halmashauri 16 zinazotekeleza mpango wa kuwapatia wanafunzi chakula cha mchana shuleni, unaofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP).

  Dk. Kawambwa alisema kupitia mpango huo, halmashauri zote zitalazimika kuingiza mpango huo kwenye bajeti zake ili kuwawezesha wanafunzi kupata chakula cha mchana. “Mei 29, mwaka huu, tulishirikiana na mke wa rais, Mama Salma Kikwete, kwenye matembezi ya hisani yaliyoandaliwa na WFP kuchangisha fedha za chakula cha wanafunzi. Walipanga kupata sh. milioni 200 lakini zilipatikana sh. milioni 230,” alisema.

  Alisema takwimu zinaonyesha katika halmashauri 16 zinazotoa chakula cha mchana, tatizo la utoro limepungua kwa kiasi kikubwa na uelewa wa wanafunzi umeongezeka.


  wavuti
   
 2. N

  NZURI PESA JF-Expert Member

  #2
  Jun 4, 2011
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 4,034
  Likes Received: 1,248
  Trophy Points: 280
  Usisikie ndg yangu ukisikia chakula shuleni utafikiri kweli!kumbe uji nusu kikombe mara 1 kwa wiki!
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Jun 4, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,321
  Likes Received: 22,167
  Trophy Points: 280
  hizi ni akili au kinyesi?
   
Loading...