Serikali kubomoa 'Maisha Plus'Kipawa

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,834
155,782
SERIKALI imewataka familia tatu zenye wakazi zaidi ya 30 wanoishi katika shule ya msingi Kipawa 'Maisha Plus'kuondoka katika kipindi cha siku sita zilizobaki kabla ya bomoa bomoa kuanza.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Miundombinu kupitia kwa Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kwa vyombo vya habari jana ilisema kuwa watu wanaishi au kufanya shughuli zao katika majengo ya shule hiyo wahakikishe kuwa wanahama na kuondoa mali zao zote.

"Serikali itavunja majengo yote ya iliyokuwa Shule ya Msingi Kipawa katika kipindi cha siku saba (7) kutokea kutolewa taarifa hii kwa lengo la kuruhusu upanuzi wa kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere" ilisema taarifa hiyo.


Watu wanaoishi katika shule hiyo ni wale ambao nyumba zao zilibomoka wakati wakisubiri fidia kupewa hifadhi na Mkuu wa Mkoa wa zamani wa Dar es Salaam, Bw. Abbas Kandoro makazi yaliyopewa jina la Maisha Plus.

Awali katika shule hiyo ziliishi familia 22 lakini baadaye nyingine 19 walichukua fidia zao na kuondoka,waliobaki ni wale wanaogomea fidia hiyo iliyolipwa kwa sheria ya mwaka 1967 wakati wao wakitaka malipo kwa sheria ya mwaka 1999.

Katika taarifa hiyo pia ilisema kuwa baada ya muda huo kupita Serikali haitawajibika na madhara au hasara itakayotokea kwa mtu yoyote atakayekaidi taarifa hiyo au kuathirika na ubomoaji wa shule hiyo.

Mwenyekiti wa watu 342 wanaogoma kuondoka Kipawa wakitafa malipo zaidi, Bw. Magnus Mulisa alisema Serikali haipaswi kuvunja shule hiyo kwa sababu haijamalizana na wakazi wa Kipawa.

Alisema mbali ya madai yao lakini bado Manispaa ya Ilala haijajenga shule mbadala katika maeneo waliyopangiwa kuhama ya Pugu Mwakanga, Majohe na Chanika.
CHANZO : MAJIRA
 
Back
Top Bottom