Serikali kubadili sheria ya kununua Dowans | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali kubadili sheria ya kununua Dowans

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by fangfangjt, Mar 14, 2011.

 1. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  Serikali leo inaanza mchakato wa kubadilisha sheria ya ununuyi ya umma,ili kuruhusu mazingira ya kununua bidhaa au mitambo iliotumika . Kwa sheria ya 2004, serikali hairuhusiwi kununua bidhaa iliyotumika. Habari hizi zimethibitishwa na waziri wa fedha Mustafa Mkullo. Kamati ya bunge ya fedha itaita wadau ili kujadilh marekebisho hayo. Mwenye kiti wa kamati hiyo ya bunge Dk Aadallah Kigoda alithibitisha kuwa mjadala huo utaanza leo

  source mwananchi

  HABARI KAMILI

  SERIKALI leo inaanza mchakato wa kubadilisha Sheria ya Manunuzi ya Umma, ili kuruhusu mazingira ya kununua bidhaa au mitambo iliyotumika, Mwananchi limebaini.

  Chini ya sheria ya mwaka 2004, inayotumika kwa sasa, Serikali hairuhusiwi kununua bidhaa au mitambo ambayo tayari imetumika.

  Sheria ikibadilishwa, itatoa nafasi kwa Serikali kununua mitambo ya Dowans katika kipindi hiki ambacho taifa, linakabiliwa na upungufu mkubwa wa umeme huku wananchi wakishinikiza mitambo ya Dowans iwashwe ili kupunguza ukubwa tatizo hilo.

  Habari zilizolifikia gazeti hili na kuthibitishwa na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, zilisema tayari Serikali imekwishalijadili kwa kina suala hilo na leo itaanza kujadiliwa na Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi.

  Kamati hiyo italijadili na baadaye kupata maoni kutoka kwa wadau mbalimbali kabla ya kuwasilisha bungeni mswada kuhusu kubadili sheria hiyo.
  Mswada huo unatarajiwa kuwasilishwa katika mkutano ujao wa Bunge unaoatarjiwa kufanyija mwezi ujao.

  "Wiki hii kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi, itaita wadau ili kuyajadili marekebisho ya sheria ya manunuzi," alisema Mkulo.

  "Jambo hili si la siri. Litajadiliwa kwa uwazi na ninyi waandishi wa habari ni miongoni mwa wadau muhimu. Kwa hivyo waambie na wenzako… Katika mjadala huo, ripoti ya Serikali itasomwa na wadau mtapewa nafasi kuijadili," alisisitiza.

  Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari serikalini, tayari mawaziri wote wamepewa dokezo kuhusu mkakati huo wa Serikali katika kushughulikia suala hilo ambalo Mkulo alisema ni siri.

  "Hilo ni ‘confidential' (siri)," alisema Mkulo alipotakiwa na Mwananchi kufafanua kuhusu maelezo yaliyo katika waraka uliotumwa kwa mawaziri wote.

  Badala yake, waziri alilishauri Mwananchi kuwasiliana na Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah, ili aeleze ni lini suala hilo litajadiliwa.

  Mwananchi lilishindwa kumpata Dk Kashilila, ili kutoa maelezo hayo.
  Hata hivyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi, Dk Abdallah Kigoda, alithibitisha kuwa mjadala huo utaanza leo.

  Kwa mujibu wa Dk Kigoda, mjadala wa leo utawahusu wajumbe wa kamati pekee yao.
  
"Tunakutana kesho (leo) Ubungo Plaza (jijini Dar es Salaam). Mkutano huo utawahusu wabunge tu," alisema Kigoda.

  Habari zilisema hatua ya Serikali kutaka kubadili sheria ya manunuzi ya umma, inalenga katika kuifanya iwe huru kukunua kitu kilichotumika haya taifa linapokumbwa na majanga au mambo ya dharura.

  Sheria ya sasa inayoizua Serikali kutonunua bidhaa au vitu viilivyotumika ilitafsiriwa katika sheria ya manunuzi ya Benki ya Dunia (WB), inayolenga kuepuka mazingira ya ufisadi.

  Lakini, kwa hapa nchini, inadaiwa kuwa sheria hiyo imekuwa kikwazo cha kupata suluhisho la muda mfupi la kutatua tatizo la umeme nchini.

  Hii inatokana na mijadala na mivutano iliyoibuka hivi karibuni kuhusu taifa kushindwa kufanya maamuzi ya haraka, katika kutatua tatizo la umeme.

  Viongozui wa Serikali, wasomi, wanasiasa na wadau wengine, ni miongoni watu walitoa maoni yao kuhusu ugumu wa sheria hiyo.

  Mwishoni mwa mwezi uliopita, Rais Jakaya Kikwete, alisema Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), iko mbioni kununua mitambo itakayokuwa suluhisho la kudumu la tatizo la umeme.

  Alisema hata hivyo, mpango huo ni wa muda mrefu kwa sababu utekelezaji wake hauwezi kuwa wa mara moja.

  Alisema kwa kawaida, hakuna mitambo inayokuwa kwenye soko tayari kununuliwa na kwamba kinachofanyika ni kuagiza ili itengenezwe, jambo ambalo litachukua miezi kadhaa kabla haijatengenezwa, kusafirishwa kuja nchini, kufungwa na kuanza kutumika.

  Rais Kikwete hakutamka lolote kuhusu pendekezo la baadhi ya wadau wanaoshinikiza kuwashwa kwa mitambo ya Dowans, ambayo ingeweza kuzalisha megawati 120 na kupunguza tatizo la mgao wa umeme.

  Lakini mwanzoni mwa mwezi huu, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alisema watu binafsi wanaweza kununua mitambo ya Dowans na kuiuzia Tanesco umeme.

  Alisema hiyo inatokana na sheria ya manunuzi ya umma, inayoizuia Serikali kununua kitu chochote ambacho tayari kimetumika.

  "Mitambo ya kufua umeme ya Dowans si lazima inunuliwe na Serikali ila kwa vile ipo tayari nchini inaweza kununuliwa na mwekezaji binafsi na ikafua umeme utakaosaidia kuondokana na mgao," alisema Pinda kwenye mahojiano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Machi Mosi mwaka huu.

  Aliongeza, "ndiyo maana kuna mazungumzo yanayoendelea hivi sasa na pande zote zinazohusika, ili kuangalia taratibu za kisheria na kuona nini cha kufanyika kwa haraka kupata megawati 160 za umeme zilizopungua kwenye gridi ya taifa…"

Mitambo ya Dowans, inayofua umeme kwa kutumia gesi asilia, ina uwezo wa kuzalisha megawati 100. Iliwahi kufanyakazi, lakini mkataba wake na Tanesco ulikatishwa na kuzua mgogoro wa kibiashara.

  

Mgogoro huo ulifikishwa katika Mahakama ya Usuluhishi ya Kimataifa, ambayo iliamua kuwa Tanesco ilivunja isivyo halali mkataba wake na Dowans.

  Hatua hiyo ililazimisha mahakama hiyo kuiamuru Tanesco iilipe Dowans Sh 94 bilioni, fedha ambazo Watanzania wataka zisilipwe.

  Taarifa zilisema Serikali kupitia jopo la wanasheria wake linashughulikia shauri la kutaka fedha hizo zisilipwe.

  Hata hivyo, taarifa zinasema kwamba Dowans ipo tayari kuiuzia Serikali mitambo yake.

  
Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI) lilitoa tamko kuwa tatizo la mgawo linatishia kuua viwanda vingi.
  Liliitaka Serikali kuzungumza na Dowans ili mitambo yake, iwashwe pamoja na kuiamuru IPTL kuzalisha umeme kwa kiwango cha juu.

  Kwa sasa inazalisha megawati 10 tu wakati mitambo yao ina uwezo wa kuzalisha megawati 100.

  Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Dar es Salaam, nacho kiliunga mkono taarifa ya Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini ya kutaka mitambo ya Dowans na IPTL, izalishe umeme ili kumaliza tatizo la nishati hiyo.

  Taarifa ya kamati hiyo inayoongozwa na January Makamba, ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli, ilisema Serikali inapoteza makusanyo ya kodi yanayofikia Sh 4 bilioni kila siku kutokana na tatizo hilo la umeme.

  Taarifa hiyo pia ilisema pato la taifa linashuka kwa asilimia tano, huku viwanda vikielekea kufungwa na kuongezeka kwa kasi ya mfumuko wa bei.

  Kwa pamoja, mambo hayo yamesababisha maisha ya wananchi kuwa magumu na kuibua malalamiko dhidi ya Serikali.
  Serikali ilisitisha mkataba wake na Dowans Agosti mwaka 2008 kwa madai ya kukiukwa kwa taratibu za kurithisha mkataba wa uzalishaji umeme wa dharura kutoka kampuni tata ya Richmond Development LLC ya Marekani.

  Richmond ndiyo iliyokuwa imeshinda zabuni ya awali ya kuzalisha umeme wa dharura baada ya nchi kukumbwa na tatizo kubwa la ukame mwaka 2006, lakini baada ya kushindwa kutekeleza agizo hilo katika muda wa makubaliano, iliirithisha Dowans kazi hiyo.

  Habari ambazo hazijathibitishwa zinaeleza kwamba Dowans ipo tayari kuuza mitambo yake kwa bei ya kati ya Sh60 bilioni na Sh90 bilioni. Wataalamu wanasema ina uwezo wa kufanya kazi kwa miaka 25.

  http://www.mwananchi.co.tz/habari/4-habari-za-kitaifa/10054-serikali-kubadili-sheria-ya-kununua-dowans
   
 2. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #2
  Mar 14, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  sasa kwa nini waitoe tender? tunaweza kupata mitambo bora zaidi na kwa bei nafuu zaidi. Inavyoonekana serikali imedhamiria kununua mitambo ya Dowans (kutokana na shinikizo fulani, ndio maana kila kikundi kinataka iwe hivyo), bila kujali matatizo ambayo Dowans/Richmond yameleta kwa Taifa letu mpaka leo hii. Hii inaipunguzia serikali uwezo wa kupata mitambo kwa bei nzuri , maana Dowans wanajua kabisa lazima serikali itanunua mitambo yao hata kama ikiwalalia kwenye bei.
  kama hii ndio njia ya serikali kulipa madeni ya Dowans ( kama hapo mwisho wa report kunavyosema kwa bei ya Sh 60-90 bil) basi tumeliwa....ni bora watangaze tender makampuni ya bid, kama Dowans mitambo yao ni bei nzuri basi Tanesco inunue, kuliko Taifa liingie kwenye hasara nyengine,

  hiyo mitambo haichelewi kuharibika baada ya miaka 3, tutamfunga RA na Al Adawi?
   
Loading...