Serikali Kuanzisha Tuzo za Mitandao ya Kijamii kwa Wanahabari


MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
40,028
Likes
5,490
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
40,028 5,490 280
Serikali Kuanzisha Tuzo za Mitandao ya Kijamii kwa Wanahabari
Mwandishi wa habari wa mtandao huu, Denis Mtima (kushoto) akikabidhiwa kadi ya kujiunga na mfuko wa hiari wa mwanachama wa PSPF na Waziri Nape Nnauye.Nape akimkabidhi mwanadada mwandishi wa habari, kadi ya ATM ya NMB.…Akisisitiza jambo fulani kwa wanahabari.…Akizungumza jambo.Mwakilishi wa wadhamini wa semina hiyo ambaye ni Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Vicky Bishubo, akizungumza jambo kwenye hafla hiyo.Mkurugenzi wa mfuko wa hiari wa mwanachama wa PSPf, Adam Mayingu ambao nao walikuwa wadhamini wa semina hiyo, akizungumza jambo.Vicky Bishubo akimkabidhi Nape zawadi iliyokuwa imeandaliwa kutoka NMB.Taswira ilivyoonekana katika semina hiyo.

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, amesema serikali inatarajia kuanzisha Tuzo za Umahiri kwa waandishi wa habari wa mitandao ya kijamii (blogs na website) kuanzia mwakani 2017.

Hayo ameyasema jana wakati akifunga semina kwa mtandao wa wamiliki wa mitandao ya kijamii na wanahabari nchini Tanzania maarufu kama Tanzania Bloggers Network (TBN).

Wakati huohuo alikabidhi kadi za ATM za NMB za kutolea fedha kwa wanahabari waliofungua akaunti zao za ‘Chap Chap Account’ na za kujiunga na mfuko wa hiari wa pensheni wa mwanachama (PSPF) jijini Dar es Salaam.

Semina hiyo ilikuwa ya siku mbili ambayo ililenga juu ya uendeshaji mitandao ya kijamii, namna ya kuzingatia maadili na namna ya kunufaika na mitandao hiyo kwa waendeshaji.

Akizungumza katika hafla hiyo, Nape alisema serikali inaitambua mitandao ya kijamii (blogs na website) kuwa vyombo vya habari nchini kwani vina nguvu kubwa katika kupasha habari kwa jamii hata kuliko magazeti.

Alisema katika uchaguzi mkuu wa urais wa 2015 mitandao ya kijamii ndiyo iliyokuwa ikitumiwa kwani iliaminika kuwa ndiyo ingeweza kufikisha taarifa za matukio kwa urahisi na ilisaidia kwa kiasi kikubwa hata kupatikana kwa viongozi.

Na Denis Mtima/GPL
 
mende msafi

mende msafi

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2016
Messages
1,095
Likes
2,026
Points
280
mende msafi

mende msafi

JF-Expert Member
Joined Aug 27, 2016
1,095 2,026 280
huyu si ni yule malaika ambaye magufuli alisema anatamani ashuke ili kufungia mitandao ya kijamii?...sasa malaika kaja na njia bora ya kudhoofiaha mitandao hii....blogers wataanza kuandika samaki ili wapate tuzo ya malaika
 

Forum statistics

Threads 1,274,988
Members 490,865
Posts 30,529,728