Serikali kuanza kutoa kinga ya VVU mwakani

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,699
Reaction score
2,260
SERIKALI inatarajia mwakani, kuanza kutoa dawa za kujikinga na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU), ikiwa ni mkakati za kuwazuia watu kutopata maradhi hayo.

Dawa hiyo ni Truvada na utaratibu huo utakuwa wa majaribio na utahusisha watu 12,000 wanaojidunga dawa za kulevya, machangudoa na wanaofanya mapenzi ya jinsia moja. Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndugulile alisema: “Hii ni tiba kama kinga na tutawapima kwanza wote 12,000 na wale wasiokuwa na maambukizi ya VVU ndiyo tutawapa dawa ambao tunajua wanaendelea na ngono zembe, kisha tutafuatilia mienendo yao kwa mwaka mmoja na ikibidi kuongeza iwe miaka miwili.”

Watu hao watakaofanyiwa utafiti huo wa majaribio ni kutoka mikoa ya Njombe, Kagera, Iringa, Mwanza, Mbeya na Dar es Salaam. Dk Ndugulile alisema kutakuwa na timu ya wataalamu ya kufuatilia mienendo yao na afya zao wote watakaokuwa kwenye majaribio hayo. Alisema timu hizo zitagawanywa katika kanda tatu ikiwemo Kanda ya Ziwa.

Alisema dawa hizo watakuwa wakipewa kila mwezi. Vidonge hivyo serikali haijanunua, bali imepata taasisi za Presidents Emergency Plan for Aids Relief (PEPFAR) na Global Fund. “Hizi dawa ni katika mkakati wa kidunia wa kuzuia maambukizi mapya na sisi tumepewa na taasisi hiyo ya Marekani ya PEPFAR na Global Fund,” alieleza Dk Ndugulile.

Dk Ndugulile alisema wanakamilisha taratibu za kuanza kwa majaribio hayo ikiwemo kupata vibali, hivyo hawajajua rasmi lini wataanza kazi hiyo isipokuwa itakuwa mwakani. Sasa hivi nchi nyingi zinatumia Truvada kama kinga dhidi ya maambukizi mapya ya Virusi Vya Ukimwi na miongoni mwao ni pamoja na Kenya, Uganda, Peru na Marekani.

Kwa mujibu wa mtandao wa Truvada.com, utumiaji wa dawa hizo ambao umeidhinishwa na Shirika la Afya Duniani(WHO) una mafanikio makubwa, unaweza kuleta madhara kama ya matatizo ya figo, kuwepo asidi ya lactic nyingi, maumivu ya tumbo, maumivu ya misuli.

Athari nyingine ni kuhema kwa kasi au kasi ya kuhema kuwa chini, kutapika, mapigo ya moyo kuwa katika hali isiyo ya kawaida, tatizo la ini, kichwa kuuma na kupungua uzito. Dawa hiyo ya Truvada imeingizwa nchini mwaka 2013 na imekuwa ikitumika kwenye tiba kama sehemu ya dawa za kufubaza Virusi Vya Ukimwi (ARVs). Inakadiriwa watu milioni 1.4 wanaishi na VVU nchini na maambukizi mapya yameonekana kupungua kila mwaka.

Takwimu zilizotolewa na Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) zinaonesha mwaka 2013 maambukizi hayo mapya yalikuwa kwa watu 72,000, mwaka uliofuata yalikuwa watu 69,603 na mwaka 2015 yameshuka na kuwa watu 48,000. Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Tacaids, Dk Jerome Kamwela amesema katika semina ya wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ukimwi kadiri dawa za kufubaza virusi vya Ukimwi (ARVs) zinavyoongezeka, vifo vitokanavyo na Ukimwi vinapungua.

Alisema hali ya maambukizi kwa Tanzania ni asilimia 5.3 huku Manyara na Tanga kwa Tanzania Bara, kiwango cha maambukizi kikiwa chini zaidi na Zanzibar, Pemba kipo chini. Makundi yaliyo hatarini zaidi kwa maambukizi na asilimia yao kwa wastani wa kitaifa yakiwa kwenye mabano ni makahaba (26), wanaume wanaofanya mapenzi ya jinsia moja (22.2) na wanaojidunga dawa za kulevya (15). Mengine yaliyo hatarini ni madereva wa malori ya masafa marefu, wafungwa na wafanyakazi wanaohama kufuata ajira.

Chanzo: HabariLeo
 
Kwa hiyo wanapewa Kinga alafu wanaambiwa wakajamiiane na Wenye Virusi? Huh!...

Nani atakubali?
 
Taarifa ina ukakasi, mara mseme mtafunga mashoga mara mnawapa dawa halafu mnawafuatilia, Tufuate lipi? Kwa hiyo wasipopata maambukizi mtaruhusu ushoga?
 
Mmmmhh.. mbona hizo side effects za hiyo dawa ni kheri madhara ya VVU kabisa... Maana wenye UKIMWI siku hizi ndio wana afya ukiwaona physically kuliko watu wazima..!!
 
Taratibu watu wameanza kuchukua nafasi ya panya katika utafiti wa dawa.
 
Mapenzi jinsia mmoja kipaumbele!rais si alikataa musaada .sheria yetu walipaswa washitakiwa nini tena kimeikuta serikali. matamko yote yale mwe
 
Hiyo population sample wanayotumia ni kuhamasisha upuuzi.

Upuuzi mkubwa sana, ndio maana wasomi tunaonekana ni hovyo kuliko ambao hawajasoma.
 
Yaani machangudoa wanapewa halafu wizara inahakikisha wanafanya ngono zembe kuona kama dawa inafanya kazi
Wizara kuhakikisha machagudoa hao wanafanya ngono zembe haiwezi kuwa kweli kwani ni unethical na linaweza kupelekea wizara kuburuzwa mahakamani.

Study design lazima ikidhi matakwa ya medical ethics. Kwa mfano katika utafiti huo:
1. Kabla ya utafiti kila chagudoa atadodoswa ni mara ngapi kwa wiki, mwezi na mwaka amefanya ngono zembe. Machagudoa waliofanya ngono zembe zaidi ya mara kumi kwa wiki ndiyo watakaofaulu kuingia kwenye huo utafiti na watapewa dawa hiyo kama wako HIV negative.

2. Baada ya mwaka mmoja hao machagudoa walioanzishiwa hizo dawa watadodoswa tena idadi ya ngono zembe walizofanya kwa wiki, mwezi na mwaka mzima. Wale ambao hawakufanya ngono zembe zaidi ya kumi kwa wiki will be dropped from the study. Wale walioendelea na tabia hiyo ya ngono zembe ya zaidi ya kumi kwa wiki watapimwa HIV status kujua kiwango cha maambukizi.

3. Control group ni machagudoa HIV negative wanaofanya ngono zembe zaidi ya 10 kwa wiki ambao hawakupewa dawa hiyo ya kinga.

Hivyo utafiti hautaingilia namna yo yote tabia ya machagudoa hawa ya namna wanavyofanya ngono.

My take: Kwa kuwa dawa hii inajulikana kutibu virusi vya HIV, utafiti huu hauna kipya kisichojulikana. It is obvious utapunguza kidogo kiwango cha maambukizi at the risk of possible serious side effects some of which could be fatal. Hivyo utafiti huu haufai. Tunachotaka ni utafiti wa chanjo (vaccine) dhidi ya virusi hivi. Kinga inayohitajika ni ya chanjo to booster one's immunity to prevent these viruses from penetrating into one's cells kama ilivyo kwa magonjwa ya virusi vya surua. Kuwaua virusi hawa baada ya kuingia kwenye cells za mtu (after infection) kwa kutumia dawa, tena dawa yenyewe ni ya kutumia milele, si kinga hata kidogo. Halafu dawa iwe na side effects kibao ambazo zinaweza kupelekea kifo. Dawa hizi ziachwe zitumiwe na wale tu ambao wameanza kuonyesha upungufu wa kinga katika miili yao. Wale ambao hawana upungufu wo wote wa kinga zao hata kama wana virusi hivyo siyo ethical kupewa dawa hizo hatari. There many who have this virus in their bodies which has done no harm to their immunities for over ten years.

Wizara ya afya iachane na misaada ya namna hii ya wazungu kutufanya guine pigs wa tafiti zao.
 
SERIKALI inatarajia mwakani, kuanza kutoa dawa za kujikinga na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU), ikiwa ni mkakati za kuwazuia watu kutopata maradhi hayo.

Dawa hiyo ni Truvada na utaratibu huo utakuwa wa majaribio na utahusisha watu 12,000 wanaojidunga dawa za kulevya, machangudoa na wanaofanya mapenzi ya jinsia moja. Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndugulile alisema: “Hii ni tiba kama kinga na tutawapima kwanza wote 12,000 na wale wasiokuwa na maambukizi ya VVU ndiyo tutawapa dawa ambao tunajua wanaendelea na ngono zembe, kisha tutafuatilia mienendo yao kwa mwaka mmoja na ikibidi kuongeza iwe miaka miwili.”

Watu hao watakaofanyiwa utafiti huo wa majaribio ni kutoka mikoa ya Njombe, Kagera, Iringa, Mwanza, Mbeya na Dar es Salaam. Dk Ndugulile alisema kutakuwa na timu ya wataalamu ya kufuatilia mienendo yao na afya zao wote watakaokuwa kwenye majaribio hayo. Alisema timu hizo zitagawanywa katika kanda tatu ikiwemo Kanda ya Ziwa.

Alisema dawa hizo watakuwa wakipewa kila mwezi. Vidonge hivyo serikali haijanunua, bali imepata taasisi za Presidents Emergency Plan for Aids Relief (PEPFAR) na Global Fund. “Hizi dawa ni katika mkakati wa kidunia wa kuzuia maambukizi mapya na sisi tumepewa na taasisi hiyo ya Marekani ya PEPFAR na Global Fund,” alieleza Dk Ndugulile.

Dk Ndugulile alisema wanakamilisha taratibu za kuanza kwa majaribio hayo ikiwemo kupata vibali, hivyo hawajajua rasmi lini wataanza kazi hiyo isipokuwa itakuwa mwakani. Sasa hivi nchi nyingi zinatumia Truvada kama kinga dhidi ya maambukizi mapya ya Virusi Vya Ukimwi na miongoni mwao ni pamoja na Kenya, Uganda, Peru na Marekani.

Kwa mujibu wa mtandao wa Truvada.com, utumiaji wa dawa hizo ambao umeidhinishwa na Shirika la Afya Duniani(WHO) una mafanikio makubwa, unaweza kuleta madhara kama ya matatizo ya figo, kuwepo asidi ya lactic nyingi, maumivu ya tumbo, maumivu ya misuli.

Athari nyingine ni kuhema kwa kasi au kasi ya kuhema kuwa chini, kutapika, mapigo ya moyo kuwa katika hali isiyo ya kawaida, tatizo la ini, kichwa kuuma na kupungua uzito. Dawa hiyo ya Truvada imeingizwa nchini mwaka 2013 na imekuwa ikitumika kwenye tiba kama sehemu ya dawa za kufubaza Virusi Vya Ukimwi (ARVs). Inakadiriwa watu milioni 1.4 wanaishi na VVU nchini na maambukizi mapya yameonekana kupungua kila mwaka.

Takwimu zilizotolewa na Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) zinaonesha mwaka 2013 maambukizi hayo mapya yalikuwa kwa watu 72,000, mwaka uliofuata yalikuwa watu 69,603 na mwaka 2015 yameshuka na kuwa watu 48,000. Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Tacaids, Dk Jerome Kamwela amesema katika semina ya wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ukimwi kadiri dawa za kufubaza virusi vya Ukimwi (ARVs) zinavyoongezeka, vifo vitokanavyo na Ukimwi vinapungua.

Alisema hali ya maambukizi kwa Tanzania ni asilimia 5.3 huku Manyara na Tanga kwa Tanzania Bara, kiwango cha maambukizi kikiwa chini zaidi na Zanzibar, Pemba kipo chini. Makundi yaliyo hatarini zaidi kwa maambukizi na asilimia yao kwa wastani wa kitaifa yakiwa kwenye mabano ni makahaba (26), wanaume wanaofanya mapenzi ya jinsia moja (22.2) na wanaojidunga dawa za kulevya (15). Mengine yaliyo hatarini ni madereva wa malori ya masafa marefu, wafungwa na wafanyakazi wanaohama kufuata ajira.

Chanzo: HabariLeo
wanaanza na mikoa ya ngno hahaaaa
 
Hii Truvada nimeisikia karibu miaka 10 iliyopita,
hamna jipya jamaa wanatufanyia test tu,
usikute hii inafanya kazi kama PrePs na PEP
 
Hii si sawa waafrika tunatimika kama wanyama wamajaribio si sawa kabisa.
 
Back
Top Bottom