Serikali pamoja na vyombo vingine vya haki za binadamu vimekuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu juu ya kuondoa aina zote za kunyanyapaa wagonjwa wa ukimwi.
Kuwatenga wagonjwa wa ukimwi kwa jinsi yeyote ile ni aina ya unyanyapaji ulio mbaya zaidi kuliko aina zingine zote.
Lakini wakati serikali na vyombo vingine vya haki za binadamu vinafanya jitihada za kuondoa aina zote za unyanyapaji kwa wagonjwa wa ukimwi, serikaki hiyo hiyo ndio kinara wa unyanyapaaji.
Mimi ni moja wa watoa huduma kwa wagonjwa wa ukimwi. Hospitali zote ziwe za serikali au binafsi zina vituo maalum za kutolea huduma za matibabu zinazojulikana kama CTC yaani "care and treatment center".
Ugonjwa wa ukimwi hauambukizwi kwa njia ya hewa wala kugusana kwa hiyo kuwatenga wagonjwa hawa na wagonjwa wengine wanaopata matibabu kwa kuwajengea mabanda yao pembeni ni moja ya aina ya unyanyapaji uliokubuhu.Ugonjwa wowote alionao mgonjwa ni siri yake na daktari wake.
Kuwajengea mabanda yao (CTC) wagonjwa wa ukimwi ni moja ya njia ya kuwanyanyapa.
Wanapokuwa wamekusanyika pamoja wanapewa huduma, jamii nyingine moja kwa moja wanakuwa wametambua kuwa wale wote wanaumwa ukimwi.
Hapa siri ya ugonjwa wa mhusika unakuwa umetangazwa kwa asili mia moja.Hali hii ya kuwatangazia siri ya ugonjwa alionao mhusika imeleta changamoto zifuatazo katika kupambana na mambukizi ya ukimwi:
Kwanza wagonywa wengi wanasita kwenda kupima afya zao.Wagonjwa wengi huhama vituo vilivyoko jirani na nyumbani kwake kwa kuhofia kuonwa na watu wanaomfahamu.
Inakuwa nafuu kwake kwenda mbali wasikomjua kupata huduma.
Baadhi ya wagonjwa wamekuwa wakitumia fedha kununua dawa za ARV kinyemela kwa sababu hawataki ugonjwa wao ujulikane na watu wengine kwa kutengwa kwenye mabanda ya CTC.
Rai yangu kwa mamlaka zinazohusika na mipango hii hasa wizara ya afya iweke utaratibu ambao wagonjwa wote wenye kisonono, malaria, nimonia, ukimwi nk.wapate huduma kwa kuchangywa pamoja.Daktari pekee ndiye abebe dhamana ya kujua SIRI za magojwa kwa wagonjwa wake wote.