17.-(1) Kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kwenda kokote katika Jamhuri ya Muungano na kuishi katika sehemu yoyote, kutoka nje ya nchi na kuingia, na pia haki ya kutoshurutishwa kuhama au kufukuzwa kutoka katika Jamhuri ya Muungano.
(2) Kitendochochote cha halali au sheria yoyote yenye madhumuni ya -
(a) kupunguza uhuru wa mtu kwenda atakako na kumweka chini ya ulinzi au kifungoni;
au
(b) kuweka mipaka kwa matumizi ya uhuru wa mtu kwenda anakotaka ili-
(i) kutekeleza hukumu au amri ya mahakama;
au
(ii) kumlazimisha mtu kutimiza kwanza wajibu wowote anaotakiwa na sheria nyingine
kuutimiza; au
(iii) kulinda manufaa ya umma kwa jumla au kuhifadhi maslahi fulani mahususi au maslahi ya sehemu fulani ya umma,
kitendo hicho hakitahesabiwa au sheria hiyo haitahesabiwa kuwa ni haramu au ni kinyume cha ibara hii.