Serikali izuie uingizaji wa Bodaboda

Clemence Baraka

JF-Expert Member
Sep 4, 2012
1,694
650
Ni ukweli usiopingika kwamba pikipiki za badaboda zimekua nyingi sana wakati vilevile maafa yanazidi kuwa makubwa.

Kwa mawazo yangu naona ni wakati sasa serikali izuie uingizaji wa pikipiki hizo lakini iruhusu tu sparepart zake.

Endapo hali itaendelea kwa spidi hii baadae kutakua na kilio kikubwa kwa kuwa barabara zetu hazitamudu wingi wake na maafa yataongezeka mara dufu.
 
Ni ukweli usiopingika kwamba pikipiki za badaboda zimekua nyingi sana wakati vilevile maafa yanazidi kuwa makubwa. Kwa mawazo yangu naona ni wakati sasa serikali izuie uingizaji wa pikipiki hizo lakini iruhusu tu sparepart zake. Endapo hali itaendelea kwa spidi hii baadae kutakua na kilio kikubwa kwa kuwa barabara zetu hazitamudu wingi wake na maafa yataongezeka mara dufu.
Ndo maendeleo mkuu, ziletwe tuu unajua hawa bodaboda wangekuwa wanajishughulisha na nini? Letaaaa zimwagweeeeee
 
Kwa Ajira Gani Tuzuie Bodaboda?Je Wakizuia Wana Malengo Gani Na Vijana Hao Juu Ya Kuwapa Ajira?Uhalifu Utazuilikaje Kwa Mfano? Ni Maswali Machache Tu Kati Ya Mia Yakujiuliza Juu Ya Hoja Uliyoitoa.Bodaboda Zinalipiwa Kodi Hamna Serikali Kichaa Yoyote Duniani Inayoweza Kuzuia Chanzo Cha Mapato Yake.
 
Wapelekwe shule tu hawa dereva bodaboda na kuwe na maadil na kanuni za kuwa dereva bodaboda maana wengi wao bangi tu
 
Kwa Ajira Gani Tuzuie Bodaboda?Je Wakizuia Wana Malengo Gani Na Vijana Hao Juu Ya Kuwapa Ajira?Uhalifu Utazuilikaje Kwa Mfano? Ni Maswali Machache Tu Kati Ya Mia Yakujiuliza Juu Ya Hoja Uliyoitoa.Bodaboda Zinalipiwa Kodi Hamna Serikali Kichaa Yoyote Duniani Inayoweza Kuzuia Chanzo Cha Mapato Yake.
Wasiwasi wangu ni uwezo wa barabara zetu.
 
Wasiwasi wangu ni uwezo wa barabara zetu.
kodi ambayo serekali inakusanya wakati hizo pikipiki zingia nchini itumike kujenga barabara.kua na vyomba vingi vya usafiri barabarani ni dalili kuwa watu wanajishulisha kutafuta kipato (kuwahi kazini au kupiga boda boda) sasa unapozuia kuingizwa kwa pikipiki unakua unabomoa sio kujenga
 
Nadhani kungefanyika maboresho ya miundombinu ukizingatia kuwa ajali nyingi zinatokea kwenye barabara ambako bodaboda zina share na magari, lakini pia elimu kwa waendesha bodaboda ni muhimu sana ikiwa ni pamoja na mamlaka husika kama askari wa usalama barabarani kuwabana vilivyo pale wanapokiuka sheria kama vile kuendesha chombo cha moto bila leseni pamoja na mwendo kasi, nk
 
Tena zichomwe moto kabisa kama vipodozi bandia! Teh! (Mawe!) kwani kabla ya hii biashara ajira zilikuwepo?? Yani kila leo ni vifo na majeruhi wa bodaboda.,why wawe wao kila siku??hivi wao wanaruhusiwa kuvunja sheria?? Mataa hayawahusu??khaa! Mpita kwa miguu ukivuka barabara especially kwenye barabara ya foleni ghafla unaweza ukakumbana na libodaboda mbele pembeni ya barabara,!!ni viroba tu! ZIFUNGIWE TU wanatumalizia ndugu,jamaa na rafiki zetu!! Mmfyuuuu boda!! Loh!
 
Hebu jiulize bila bodaboda itakuwaje kuhusu uhalifu
Bodaboda zimeanza lini, na kabla ya hapo maisha yalikuwa aje? Sidhani kama zikisitishwa ndio itakuwa mwisho wa dunia. Wakigeukia uhalifu sheria zitachukua mkondo wake.
 
Kwa ufupi zisizuiliwe kabisa ila tu zizuiliwe kuingia main road na sikwamba haiwezekani inawezakana maana zina saidia nje ya mji hasa kufika watu wanapo ishi bodaboda wamefanya dar hata nje ya mji kuonekane town maana kufika huko ndani sijui ingekuwaje watu wangekuwa wanaukanyaga mguu zaidi ya nusu km.

Zisizuiliwe ila zisiingie barabara za lami maana majanga yanaongezeka
 
Back
Top Bottom