GwaB
JF-Expert Member
- Mar 19, 2014
- 5,223
- 7,083
Kamati iliyoundwa kuchunguza chanzo cha ajali ya kupinduka chombo cha MV Nyerere inaweza kuwa imeishaanza kazi yake tangu ilipotangazwa au kama nilivyosoma kwenye makala moja inaanza kazi yake leo. Pamoja na kamati hiyo kuwa na kazi ya kumulika chanzo cha ajali, nafikiri itakuwa vyema kama watajaribu kusikiliza maoni na ushauri wa watu mbali mbali ambao kila mmoja kwa uelewa wake au uzoefu ametoa maoni kuhusu kile kinachopaswa kufanyika.
Tanzania tumebarikiwa kuwa na maziwa matatu yanayotuzunguka na kuwa na idadi kubwa ya wananchi ambao usafiri wa majini ndio namna ya kuishi, ndio namna ya kusafiri. Ajali iliyotokea kwenye visiwa vya ukara ni sehemu ndogo tu ya kiashiria cha uhitaji mkubwa wa vyombo vya usafiri majini vyenye hadhi, uwezo mkubwa wa kupakia abiria na mizigo yao lakini licha ya kuwa usalama viwe maridadi.
Kwa bahati mbaya sana ununuzi wa meli au vivuko vyetu vingi unajikita kwenye kubana matumizi zaidi kuliko kuangalia ubora wa vyombo vyenyewe. vyombo vyetu vingi ni chakavu na vifinyu kulingana na idadi kubwa ya watu wenye uhitaji wa kusafiri majini bila kuhusisha utalii ambao ni mada nyingine ya kuongelea siku zijazo.
Naishauri sasa serikali yetu kuanzia sasa ifanye juhudi za kuwekeza kwenye usafiri wa majini kama ilivyofanya kwenye kampuni ya ndege, kwa kujenga meli kubwa zenye uwezo wa kubeba abiria kati ya laki tano hadi million moja katika maziwa ya Victoria na Tanganyika. Bei ukilinganisha na faida itakayopatikana katika uwekezaji huu ni ndogo na itaongeza rasilimali za nchi.
Hizi ndizo bei za meli nyingi zinazojengwa duniani na tukijipanga vizuri tuna uwezo wa kuua ndege wawili kwa wakati mmoja, kwa maana ya usafiri majini na biashara ya utalii. Usafirishaji mizigo pamoja na uvuvi vinaweza kanzishiwa vitengo tofauti na bila shaka mada ya siku nyingine. Meli kubwa ikiishajengwa ni kama hoteli inayoelea majini ambapo uhai wake ni miaka hadi mia moja.
Tanzania tuziongezee thamani rasilimali zetu kwa kuwekeza zaidi na kuifanya Tanzania moja ya sehemu ya kuvutia sana duniani na salama.