Serikali iweke sheria ya usafirishaji wanyama wa kuchinja

uchumi2018

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2018
Posts
2,085
Reaction score
2,996
Habari zenu wanajukwaa.
Niende moja kwa moja kwenye hoja.
Juzi tuliona kwenye vyombo vya habari
kuhusu mizoga ya ng'ombe 15 waliokuwa
wamepelekwa tegeta Dar es salaam ili
kutengenezwa na hivyo kuwauzia watu kama kitoweleo.

Tumemsikia meya wa manispaa ya kinondoni
akilaani kitendo hiki cha wachinjaji wasio waaminifu
kujaribu kwalisha walaji wa nyama vibudu.
Mimi najaribu kuangalia jambo hili kwa jichola tatu,tujiulize ni nini chanzo
cha wanyama hawa kufa wakiwa wanasafirishwa? Kama umesafiri njia ya kati utakuwa
umeyaona magari yamepakia mifugo misiri ya mazao ya biashara yasiyo na uhai.
Naamini hii ni sababu mojawapo inayosababisha,maana wanakuwa wamebanana
na hata akichoka hawezi kulala na akilala anakanyagwa na wenzake waliosimama.

Rai yangu ni kuwa umefika wakati serikali
iweke sharia madhubuti ya kusafirishaviumbe hai,ihusishe muda wa kukaa
kwenye chombo cha usafiri,upatikanaji wa maji nachakula cha mifugo husika
kutegemeana na umbali wa safari.kinyume na hapo,hali hii haitaisha.

Hakuna mfanya biashara atakayenunua wanyama na kuwasafirisha
wakafa mara tu baada ya kuwafikisha akawatupa,tena kwa kuingia
gharama ya kuwazika na mengineyo badala yake atatafuta waharifu
watakaoendelea kutulisha vibudu.

Ni vyema serikali isimamie usafirishaji wa wanyama hawa
wafikishwe wakiwa katika hali nzuri naamini
hatutashuhudia uhalifu wa namna hii na hata ikitoke itakuwa ni nadra.
 
Bora umeongea maana hili suala hata Mimi hua Lima niumiza sana
Kuna watu hawajali kabisa wanyama
Wana waona kama si viumbe hai
Ifike wakati sasa serikali isimamie
 
Ni kweli kabisa mkuu,yaani unakuta
wanyama hata hewa unaona kabisa
hawapati vya kutosha kutokana na mbanano.
 
Afadhali mizoga ya ng'ombe ni michache sana kuliko mizoga ya hawa kuku wa kisasa,kiukweli mungu atatusamehe tu maana kama watu wana roho ngumu ya kuua watu na kuweka maiti kwenye viroba ataona huruma kukulisha mzoga?
Mtu anakung'oa kucha bila ganzi huku anakuangalia usoni mchana kweupe bila huruma,je atashindwa kukulisha mzoga?
 
Ingekuwa machinjio yoote yanamilikiwa na Serikali haya yasingetokea, badala yake wamiliki ni wa binafsi na wasijali AFYA zetu kabisa. Nenda manjio ya pale Kimara Suka uone vituko vya pale.
 
Waafrika akili hawana mpaka kila kitu wawekewe sheria? Hata kujua kuwa ukipakia wanyama kama hivo si vizuri?

Mimi naamini machinjio yote wanachinja nyama maiti. Kwa tamaa

Serikali sio itunge sheria ambazo kila siku zinatungwa hatuoni utekelezaji wake

Serikali itangaze kuwa nyama si salama mpaka itakapojirizisha. Ikifanye hivo hata kwa wiki wananchi wakigoma watajirekebisha

Lakin serikali hii inayojali kodi sio maisha ya watu haiwezi kuchukua hatua yoyote.
 
Mkuu
Waafrika akili hawana mpaka kila kitu wawekewe sheria? Hata kujua kuwa ukipakia wanyama kama hivo si vizuri?
siamini kama issue ni uafrika,maana nchi kama marekani
kuna watu wanakutwa na kesi za kukiuka haki za wanyama
pamoja na kwamba kuna sharia za kuwalinda wanyama.
Nadhani hapa issue ni ukatili na kutaka kupata faida
iliyopitiliza,ndo maana tunaiomba serikali isimamie jambo hili.
 
Ni aibu kutoa mfano wa marekan? Haki za wanyama zipi zinavunjwa marekani ukizitaja zitasaidia
 
Kufuga wanyama ambao huna huwezo wa kuwapa matunzo
ni mojawapo.Na wapo wanaohukumiwa na wanafungwa
au mkuu ukisikia marekani unadhani ni nusu ya mbinguni?
 
Ndo maana zamani mm nakumbuka tulikua tunapakia kwenye mabehewa yaliyotenganishwa yaan na kamba tunaongezea ngo'mbe anafika anakokwenda salama ila hii ya kutumia magari siku hizi dah ??kweli serikali iingiliea kati maana hawa jamaa wanatesa sana viumbe hivi
 
Kufuga wanyama ambao huna huwezo wa kuwapa matunzo
ni mojawapo.Na wapo wanaohukumiwa na wanafungwa
au mkuu ukisikia marekani unadhani ni nusu ya mbinguni?

Iyo sheria ndio inatakiwa tena sio kwenye kula ni matunzo ya mnyama. Uone maajabu ya marekani wamepitiliza kutoka kwenye matunzo ya binadamu mpaka ya wanyama. Hao watu utawafikia kwa njia gani? Na umeona sheria zao zinavofanya kazi mpaka watu wanafungwa kwa wanyama kwa kuwatimizia haki zao. Hapa afrika imetokea wapi kama hiyo?
 
Ingekuwa machinjio yoote yanamilikiwa na Serikali haya yasingetokea, badala yake wamiliki ni wa binafsi na wasijali AFYA zetu kabisa. Nenda manjio ya pale Kimara Suka uone vituko vya pale.
Mwamba yamefungwa long tym kupisha ujenz labda ya kuelekea golan kama yapo active
 
Wanyama wakisafirishwa na kufikishwa kwa muda muafaka wanafika salama...

Tatizo labda linaweza kua kwenye vizuizi vya ukaguzi... ucheleweshwaji au uzembe wa makusudi unaweza kutokea...

Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom