kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,423
- 13,935
Uuguzi ni taaluma muhimu sana kwenye afya, lakini Wauguzi wana manung'uniko ya chinichini ambayo ni hatari sana kuendelea kuwa nayo mioyoni mwao. Manesi wana shida zifuatazo ambazo zinawaondolea morali yao ya kuwahudumia wagonjwa:
1. Uongozi: Hakuna sifa na/wala vigezo vinavyofahamika vya kuupata uongozi kwenye nursing. Kwasasa unatumika urafiki, undugu, ukanda na udini kupata uongozi kwenye nursing. Hii inasababisha uuguzi kupoteza dira. Think tank ya uuguzi ina shida nyingi, imekosa dira wala mwelekeo kabisa.
2. Elimu: Elimu ya wauguzi haielezeki, utakuta wako waliosoma digrii hiyohiyo kwa miaka 2, 3 na wengine 4.
3. Specialties: Wauguzi wote wamerundikana sehemu moja, eti kila muuguzi anajuwa na anaweza kufanya kila kitu kwa kiwango kilekile. Hii inawaletea shida kwenye ufanisi wa kazi na mgawanyo wa kazi za kitaaluma na utoaji huduma uliotukuka kwa wagonjwa.
4. Scheme of Service: Kutokana na mkanganyiko wao wa idadi ya muda wa kusoma na kuhitimu kozi, na mkanganyiko wa majukumu yao inasababisha iwe vigumu kuwapangia scheme of service kwa urahisi.
5. Ubaguzi wa wahitimu: Viongozi wa wauguzi hawawapendi manesi wenye digree za moja kwa moja waliopitia form 6 moja kwa moja kwenye nafasi mbalimbali za uongozi eti hawana uzoefu hata baada ya miaka 24 ya kuwepo kwa wahitimu wa aina hiyo nchini. Asilimia 99% ya viongozi makao makuu, baraza la uuguzi, mikoani, wilayani, n.k ni wale wenye elimu za kuungaunga tu na digrii za miaka 2. Hii inaikosesha nursing viongozi wenye vipaji na damu changa ya kuongoza na kufikiri.
6. Michango miingi: Pamoja na kuwa na kipato kidogo, lakini manesi wanaandamwa na michango mingi sana ya ziada. Michangango hii ni pamoja na kulipia LESENI na adhabu za leseni, vyama vya kitaaluma (TANNA, TAMA), PAYE, NIHF, NSSF/LAPF, UNIFORM, USAFIRI, NYUMBA, n.k. Viongozi wao hawajali kipato cha muuguzi wakati wanapopanga nini cha kuwalipisha wauguzi wao. Viongozi wanaiga mambo kutoka nje ya nchi bila kuzingatia context na supportive environment ya ufanikishaji wa jambo hilo hapa nchini.
Yote haya yanasababisha wauguzi wajiunge na uuguzi na wafanye uuguzi kwa shingo upande. Ushahidi wa haya unaweza kuuthibitisha kwa mambo yafuatayo:
1. Wanafunzi wenye alama hafifu tu ndo wanajiunga na uuguzi (Hakuna division 1 na two nyingi huko)
2. Wanafunzi wengi wanaojiunga na Uuguzi kwa njia ya CAS ya TCU wanaomba kuhamia kozi ya udaktari
3. Wanafunzi wengi wanaomaliza uuguzi hawapendi kwenda wodini kufanyakazi za kiuguzi, wengi wao wanatafuta kazi nyingine au kusoma kozi nyingine kabisa.
4. Ni rahisi kusikia nesi kala rushwa au amehudumia mgonjwa vibaya
5. Kuchelewa kulipia michango mingi wanayodaiwa kulipa.
6. Wauguzi wengi hawataki watoto wao wawe wauguzi (fanya utafiti utagundua)
7. Wauguzi wengi wako ulaya, USA, Botswana, S. Afrika, nk ambako uuguzi una ahueni.
Waziri mwenye dhamana huu sio mzaha tafadhali saidia jeshi lako hili kulipangia namna ya kuenenda, la sivyo kelele kwa wananchi dhidi ya wauguzi hazitakwisha kuhusu huduma mbovu. Pamoja na ukweli kwamba wauguzi hawatoshi kwenye vituo, lakini hao hao wachache waliopo wanazuiwa kuwahudumia wagonjwa eti kwa kosa la kutolipia hela za leseni ya kufanya uuguzi na kusababisha kazi ya uuguzi kufanywa na "Wauguzi" wasiosoma kabisaa yaani nurse assistants au health attendants. Unamzuia muuguzi asihudumie wagonjwa eti kwa kosa la kutolipa hela za leseni lakini unamruhusu mtu asiyekuwa muuguzi (ward attendant) kuhudumia wagonjwa, hii ni akili?