Aman Ng'oma
JF-Expert Member
- Nov 8, 2011
- 966
- 537
Hali ya maisha kwa wafanyakazi wa kada za chini ni duni sana.Hali hii inatokana na viwango vya mishahara visivyokidhi mahitaji yao.Hakuna uwiano sawa wa viwango vya mishahara kati ya wafanyakazi wa kada fulani na nyingine.
Maisha ya sasa hivi ni magumu na kwa viwango hivi vya mishahara vinawakatisha tamaa wafanyakazi wengi matokeo yake ari ya utendaji wa kazi unapungua.Tusitarajie maendeleo kutoka kwa wafanyakazi waliokata tamaa ndio maana kila siku mambo yatazidi kuharibika tu,mfano mzuri tazama secta ya elimu,namna ambayo wanafunzi walivyofeli.
Tutaunda tume nyingi sana,lakini kama stahiki za wafanyakazi hazitatazamwa tutarajie mambo kwenda kombo zaidi kila leo.Hii nchi yakwetu sote na lazima matunda yake yaliwe na wote.
Viongozi wetu wamekuwa wabinafsi wanaojijali zaidi wenyewe .Kama tukihitaji ufanisi lazima tukubali wafanyakazi wanapata stahiki zao za mishara inayokidhi mahitaji yao.Mfanyakazi anayelia njaa hawezi akafanya kazi kwa moyo,hivyo nchi itaendelea kuwa masikini.
Kama serikali itaamua, ina uwezo mkubwa sana wa kuwaondolea manung'uniko wafanyakazi.
Pia serikali iangalie namna bora ya malipo ya mishahara,kama inafuata viwango vya TGS,basi iwe kwa ngazi zote bila kujali huyu mbunge,waziri ,hakimu au mwalimu.Mfanyakazi alipwe mshahara kulinana na elimu yake. Hapo nadhani manung'uniko kwa wafanyakazi yataisha.