Inawezekana maada hii ilishajadiliwa hapa lakini naomba niianzishe tena.
Tumeshuhudia kilichotokea Samunge,kilichotokea wenye DECI na yanayotokea sasa ambapo watu tofauti wanatangaza biashara ambazo hazijathibishwa wala kusajili.
Nimepanda bus na ndani yake baada ya muda anajitokeza bwana mmoja mwenye briefcase ambayo imejaa dawa aina tofauti na katika matangazo yake anadai kuwa anauwezo wa kutibu kansa ya kizazi.
Unafungulia TV na unamuona "daktari" anayeeleza namna ya kutibu pressure kwa kutumia vitunguu.
Mtaani kuna matangazo hasa katika baadhi ya misikiti kuwa kuna mashine za kusafisha figo na gharama ni kati ya elfu 70 mpaka laki na kitu.
Ukiangalia yote hayo ni utapeli na serikali haichukui hatua wakati wananchi wake wanadhulumiwa na wajanja wachache.Inawezekana baadhi ya watu wakadai ya kuwa mtu kapenda mwenyewe kutapeliwa lakini binafsi naamini ya kuwa serikali ina wajibu wa kutoa miongozo mara kwa mara na kuchukua hatua ili kulinda raia,leo tuangalie walikwenda Samunge,kama bado yuko hai ni kuwa natumia dawa za hospitali na si vinginevyo.
Tujadiliane!!!