Serikali iwadhibiti wanaotumbuliwa majipu wasiajiriwe sekta binafsi.

maramia

JF-Expert Member
Jul 17, 2015
2,030
1,345
Kutakuwa hakuna maana kama viongozi na watumishi wa serikali/umma wanaotumbuliwa majipu na kufukuzwa ama kusimamishwa kazi watakuwa haraka haraka wanakimbilia kuajiriwa katika taasisi na sekta binafsi ns kwa hiyo kufukuzwa kwao hakutakuwa kunawaumiza sana.

Serikali iwe kali kwa watu hawa, mbona mwalimu aliweza? Aliweza kuamuru mtu arudi akaishi kijijini kwake na awe anaripoti kwa Dc ktk kipindi fulani au akalime na ikawezekana? Kwa mfano aliwahi kumfanyia hivyo Tuntemeke Sanga.
 
kumbuka nchi yetu si ya kikumunist ! mtu binafsi akiamua kuajiri mtu yeyote yupo huru, kama ni mgeni atafata taratibu ...
 
Kutakuwa hakuna maana kama viongozi na watumishi wa serikali/umma wanaotumbuliwa majipu na kufukuzwa ama kusimamishwa kazi watakuwa haraka haraka wanakimbilia kuajiriwa katika taasisi na sekta binafsi ns kwa hiyo kufukuzwa kwao hakutakuwa kunawaumiza sana.

Serikali iwe kali kwa watu hawa, mbona mwalimu aliweza? Aliweza kuamuru mtu arudi akaishi kijijini kwake na awe anaripoti kwa Dc ktk kipindi fulani au akalime na ikawezekana? Kwa mfano aliwahi kumfanyia hivyo Tuntemeke Sanga.
haya ni mawazo ya kijinga sana, mtu anaweza kuwa hafai kwenye utumishi wa umma akafaa kwenye sekta binafsi, unataka mtu akifukuzwa polisi basi asiajiriwe na kk?
 
Si ya kijinga sana ungesema ni ya kijinga wa kadili maana kuna nchi zina sheria kama hizi, kwa mfano Sweden, Denmark na Finland.

Ndiyo maana utakuta wafanya kazi wana discipline sana ya kazi kwa sababu mtu anajua akiipoteza kazi aliyonayo hataajiriwa popote.
 
Baada ya hapo mtazuia hata wasijiari wenyewe. Tupunguze mawazo ya chuki maisha bado magumu sana.
Wana maisha gani magumu, mijitu ina mijumba mpaka sabini, magari matano ya bei ya 500 milioni kila moja, vituo vya mafuta kila wilaya bado mnasema maisha magumu.

Maisha magumu kwako si kwao. Huruma yenu ndiyo jeuri yao.
 
Si ya kijinga sana ungesema ni ya kijinga wa kadili maana kuna nchi zina sheria kama hizi, kwa mfano Sweden, Denmark na Finland.

Ndiyo maana utakuta wafanya kazi wana discipline sana ya kazi kwa sababu mtu anajua akiipoteza kazi aliyonayo hataajiriwa popote.
Hakuna binadamu yeyote aliyekamilika hata ktk nchi hizo ulizozitaja.acha mawazo ya kishetani hayo
 
Mkuu kama ni Elimu alisoma yy, ujuzi anao yy na vyet ni vya kwake kwann umzuie??

Basi uanze kufuta utalaamu na ujuzi kichwani mwake.
 
Kutakuwa hakuna maana kama viongozi na watumishi wa serikali/umma wanaotumbuliwa majipu na kufukuzwa ama kusimamishwa kazi watakuwa haraka haraka wanakimbilia kuajiriwa katika taasisi na sekta binafsi ns kwa hiyo kufukuzwa kwao hakutakuwa kunawaumiza sana.

Serikali iwe kali kwa watu hawa, mbona mwalimu aliweza? Aliweza kuamuru mtu arudi akaishi kijijini kwake na awe anaripoti kwa Dc ktk kipindi fulani au akalime na ikawezekana? Kwa mfano aliwahi kumfanyia hivyo Tuntemeke Sanga.
Kama wana makosa basi wachukuliwe hatua za kisheria. Mambo yangekuwa ni hivyo unavyotaka wewe basi hata mwinyi asingeupata urais. Na huyo alikuwa mwalimu na wakati haukuwa huu. Na unavyoona wewe vijiji ndio vinavyotakiwa kupokea hao watu?
 
Wana maisha gani magumu, mijitu ina mijumba mpaka sabini, magari matano ya bei ya 500 milioni kila moja, vituo vya mafuta kila wilaya bado mnasema maisha magumu.

Maisha magumu kwako si kwao. Huruma yenu ndiyo jeuri yao.
Acha Ku generalise kwa Hiyo hata wale manesi na walimu waliofukuzwa nao wana utajiri wa aina Hiyo? Hivi kuna kiongozi hata mmoja wa kusiasa ametumbuliwa jipu?
 
Back
Top Bottom