barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,865
SHIMIWI ni mashindano ya michezo ambayo hujumuisha Wafanyakazi wa Serikali Kuu,Idara na Mashirika mbalimbali ya Umma,mashindano haya hujumuisha michezo mingi kama mpira wa miguu,wa pete,mchezo wa bao,kuvuta kamba,karata na mengineyo.
Lengo la kuanzishwa michezo hii, ni kujenga afya,kukuza undugu na kufahamiana miongoni mwa wafanyakazi ndani na nje ya shirika/idara husika.Mwaka huu mashindano hayo yanafanyika mkoani Dodoma.
Miaka ya nyuma SHIMIWI ilikuwa na radha yake,ukienda kutazama mpira wa miguu ni raha tupu, unawakuta wafanyakazi kweli,wenye umri wao...mpira unakuwa burudani,ukienda kwa wakimbiza kuku ni raha tupu achilia mbali hao wacheza netball.
Lakini sasa SHIMIWI si ile tena,Idara nyingi zinakodi "MAMLUKI" toka nje waje kuzichezea timu zao,lengo tena si afya wala kujaamiana kwa wafanyakazi.Malengo ya mashindano hayana maana tena,wafanyakazi wenye haki ya kushiriki mashindano hayo wanakuwa "sidelined"..hawana fursa tena,umuhimu wake haupo tena.
Moja ya chanzo cha "Wafanyakazi Hewa" ni hii SHIMIWI,Idara nyingi za Serikali zimekuwa zikiajili wafanyakazi wa muda kwa ajili ya michezo tu ya SHIMIWI na baada ya michezo kuisha mtu anakuwa hana kazi ya kufanya zaidi ya kusubilia mashindano mengine ya mwaka ujao.
SHIMIWI ni jipu,pesa inayopigwa SHIMIWI kwa muda mrefu ni ufisadi mtupu.Michezo ni Afya,lakini uwepo utaratibu wa wafanyakazi hasa wa serikali kushiriki na sio mamluki.Kila mahali ilikuwa ni "deal" na ufisadi.Waziri Nape na Jenista Mhagama katika pitapita zenu basi mnusenuse na SHIMIWI,mtajionea mkubwa msiyoyajua
WENYE DHAMANA NA MASHINDANO YA SHIMIWI WAJIBIKENI KURUDISHA HESHIMA YA SHIMIWI...WAPENI HAKI WAFANYAKAZI.