Serikali itumie njia hii kuboresha elimu hasa ya chuo

FPT

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2017
Posts
1,224
Reaction score
1,851
Kwa kipindi kirefu, elimu nchini Tanzania hasa elimu ya chuo kikuu imegubikwa na changamoto nyingi ambazo zinaifanya ionekane ni ya ovyo. Wanafunzi wa vyuo hawajitumi kusoma kwa kutegemea alama nzuri kutoka kwa wahadhiri wao. Pia, wanafunzi wanategemea” madesa” na “ vinondo” ili waweze kufaulu. Wanafunzi wanatumia muda mwingi kufanya yasiyofaa badala ya kusoma. Wengi wa wanafunzi wanategemea njia za mkato kufaulu na kujigamba kwamba kahitimu na GPA kubwa ambazo kwa hakika si za kwako. Haya ni mambo ambayo yanafanya elimu yetu hasa ya chuo kuonekana haifai.
Kwa kuonelea hili, nimeona nije na mapendekezo yafuatayo ili walau kuboresha elimu ya Tanzania hasa ya chuo ambayo kimsingi ndio elimu ya ujuzi na taaluma. Mapendezo na ushauri wangu kwa serikali ni kama ifuatavyo
  • Kuundwa kwa bodi za mitihani Napendekeza serikali iunde bodi za mitihani ya kitaaluma kama ilivyo kwa wahasibu ambao wana bodi inayoitwa NBAA. Mwanafunzi anayesomea uhasibu chuoni si kigezo cha yeye kuwa mhasibu bali mpaka aidhinishwe na bodi ya wahasibu(NBAA) kwa kufanya mitihani ya bodi na kuifaulu. Uwepo wa NBAA kunaifanya kozi za uhasibu ziheshimike na wanafunzi kujituma kusoma kwa ajili ya hiyo mitihani. Uhasibu ni taaluma inayoheshimika kutokana na uwepo wa bodi nzuri za kuisimamia. Kutokana na uwepo wa wahadhiri wasio waaminifu, wanaofaulisha wanafunzi pasipo mwanafunzi kutoa jasho katika kusoma, napendekeza serikali iunde bodi za mitihani kama ilivyo NBAA. Hii itapunguza uzembe kwa wanafunzi kuamini katika vinondo na madesa badala ya kusoma vitabu. Hii, pia itapunguza malalamiko ya rushwa ya ngono vyuoni kwa wanafunzi kwa sababu mwanafunzi ataonesha bidii ili aje kufaulu mitihani ya bodi na hivyo kufanya asome kwa bidii na kufaulu hata mitihani yake ya chuo.
  • Mishahara ipangwe kutokana na ufaulu wako wa mitihani ya chuo na bodi Hii pia itawafanya wanafunzi wajitahidi kusoma kwa bidii ili wafaulu vizuri na hivyo kupelekea kulipwa mshahara mzuri. Wanafunzi wanakuwa wavivu kusoma kwa kuamini kwamba hata nikisoma vipi nitapata mshahara sawa na Yule aliyepata first class GPA. Mishahara inatakiwa ipangwe kutokana na jasho mtu analolitumia katika kusoma. Hii itasaidia kuwafanya wanafunzi hawa wafaulu vizuri kwa kusoma kwa bidii kwa mategemeo ya kuja kulipwa vizuri na sio kufungua fungua vitabu na kufunika. Tofauti ya mtu aliyepata GPA ya 3 na mtu aliyepata GPA ya 4.8 ionekane pia katika mishahara yao hata kama wanafanya kazi iliyo sawa ama wana cheo kinachofana.
FPT 2040.​
 
Hili ni wazo ambalo wanaweza kuwa nalo wenye akiri tu kama wewe naunga mkono hoja kwa asilimia zaidi ya mia jamani kama kuna mhusika anaeweza ona huu uzi naomba ikiwezekan Auprint haraka kabla haujafutwa hili ni wazo kubwa mno tena sana
 
Umeongea vitu visivyoeleweka... That's not how to improve education
 
wataboreshaje elimu wakati hao wenyewe hawakuboreshewa elimu..?
hii ishu ya kuboresha elimu hawa viongozi wetu kama vile wamepigwa upofu.
 
Mkuu, kwa uzi wako ulivyo na maelezo yake, hii ya mishahara umeitafakari vizuri?
 
Njia bora ni kuanza kufundisha kwa kutumia kiswahili hadi chuo kikuu.
 
Back
Top Bottom