David Goliath
JF-Expert Member
- May 16, 2018
- 928
- 1,799
Niende Moja Kwa Moja kwenye mada, Serikali kupitia wizara ya afya na TCRA kupitia makampuni ya simu toeni elimu au tahadhari Kwa watanzania kutojifungia ndani wakiwa wamewasha majiko ya mkaa au kuni ndani ya nyumba.
Mara Kwa mara kumekuwa na matukio ya vifo vya watanzania wenzetu wakipoteza maisha kutokana na kujifungia ndani na majiko ya mkaa hasa kipindi cha baridi na mvua Ili kujipatia joto, ni wachache sana wanajua madhara yake na kati ya hao wachache wapo pia wanaopuuzia.
Naamini kupitia matangazo kwenye vyombo vya habari na makampuni ya simu na vipeperushii tunaweza kuokoa maisha ya watanzania wengi.