Ray waniache
JF-Expert Member
- Jan 25, 2017
- 737
- 507
Kwanza kabisa niseme huwa sinaga chama, Kila ninaechat au kuzungumza naye analalamika hali kuwa ngumu
Nawaonea huruma vijana wenzangu.ambao wamesoma wanazo degree zao wapo tu nyumbani kila siku wimbo wa ajira umekua ni ule ule
Ingekua hata serikali imewatengezea mazingira ya kujiajiri hata isingekua nongwa
Vijana wa nchi wana moyo wa uvumilivu sana
Wanapitia kipindi kigumu cha maisha kuliko chochote kile tanzania hii
Naumia sana pale napowakuta vijana wenzangu hususani kaka zangu na dada zangu wa kitanzania. wamesomeshwa kwa shida na wazazi hizo degree au wamesoma kwa mkopo halafu leo hawana ajira halafu hapo body ya mikopo inawajia juu walipe watalipaje sasa?
Serikali ya kidemokrasia ni utawala wa watu ulowekwa na watu na kwa manufaa ya watu kwanini vijana ambao wengi ndo wapiga kura wakose ajira katka nchi yao
Tuache utani kwenye hili jambo halihitaji mzaha kabisa
Cha msingi serikali itoe ajira kwa vijana kuliko kinyume chake
Kama hutoi ajira kuna haja gani ya kutenga mabilioni kila mwaka ya mikopo na kujenga au kukarabati vyuo ilhali watu hawaajiriwi?