Ngho
Senior Member
- Jun 2, 2015
- 121
- 192
Karibuni kwenye symposium wajumbe,
Nimeona kuna baadhi ya vitu SERIKALI inafanya ambavyo vinamuumiza moja kwa moja mwananchi. Mathalani suala la Tozo za simu, Kodi ya nyumba kupitia LUKU, na baadhi ambavyo yanapangwa yenye lengo la kujinufaisha YENYEWE huwa hawazingatii au kuhofia Mzigo kwa wananchi. Wananchi ambao wamekuwa wakikaa kwa muda kusubiri nani wa kuwasaidia lakini HAWAIONI kesho yao.
Mnamo tarehe 27 July BoT walitoa mapendekezo katika kipindi hiki baada ya mdororo wa uchumi uliosababishwa na COVID-19 yaliyolenga kupunguza ukali wa maisha, miongoni mwa vitu ambavyo walikuwa wamevilalamikia ni suala la RIBA kwenye mikopo ya Banks ambayo ni 17%. BoT ilizitaka Banks kushusha RIBA kutoka 17% mpaka 10% agizo ambalo halijatekelezwa mpaka leo na wamelisahau au LINA MOTO.
HOJA YANGU:
Serikali ijikite katika mizani katika kuhudumia umma kwa sababu vyovyote inavyoshindwa kusimamia WELEDI katika malengo yake kwenye baadhi ya TAASISI inatoa taswira ambayo ni sio nzuri kwa wananchi.
Suala la Tozo za miamala ya simu wananchi walioshirikishwa ni wale DARAJA la kwanza (MPs) wakatutika kuwa hatuna shida, suala la Kodi ya nyumba nalo kupitia WALE WALE, tumepokea na maumivu tunayavumilia.
Ila ni vipi SECTA ZINGINE ambazo zinashindwa kusimama kwenye utekelezaji wa maagizo ya SERIKALI? Au wameshindwa kukubaliana au dhana ya ushirikishwaji?
SERIKALI itende haki.