Serikali itafute kiini cha wanafunzi hewa nchini


drclark

drclark

Member
Joined
Feb 10, 2016
Messages
57
Likes
12
Points
15
Age
49
drclark

drclark

Member
Joined Feb 10, 2016
57 12 15
Elimu bora yenye sera zinazotekelezeka, dira, mfumo na utaratibu mzuri hutoa kizazi bora cha elimu ambacho ndicho hutumika kama chachu ya maendeleo katika taifa lolote.

Msingi wa maendeleo ni elimu, taifa lisilo na mfumo imara wa elimu, hujikuta likitumbukia katika malumbano, maradhi, ujinga, umaskini, kupoteza mwelekeo na matatizo sugu yanayotokana na udhaifu huo.

Uvumbuzi wa changamoto za elimu utatokana na viongozi bora wa elimu ambao wataweza kuchora ramani ya mfumo, kutunga sera, dira ya elimu na kuwa na taswira halisi ya elimu ya baadaye.

Kwa bahati mbaya elimu yetu ya Tanzania imekuwa ikukumbana na ombwe la viongozi ambao hufanya sekta ya elimu kuwa mithili ya kinyozi anayejifunza kunyoa.

Mawaziri wengi hawajengi misingi ya elimu kwa kufanya utafiti, kushirikisha wadau wa elimu au kuitisha mijadala kabla ya kufikia maamuzi.

Ni jambo la kawaida kuona tamko la kiongozi likipingwa hata kabla halijaingizwa katika utekelezaji. Tafsiri yake ni kuwa hakuna ushirikishwaji wa wadau wala mijadala kuanzia ngazi za chini.

Mtitiriko huu wa matamko yanayoleta ukakasi katika sekta ya elimu, haujaanza kwa waziri wa sasa, Profesa Joyce Ndalichako.

Wengi hivi sasa tunashangazwa na kauli zake za kutaka wanafunzi kuhakikisha wanatumia njia moja ya kufika chuo kikuu bila kutumia njia mbadala. Yaani kidato cha nne halafu cha sita kabla ya kujiunga na elimu ya juu.

Tunachosahau ni kuwa kumewahi kutolewa maamuzi mengi, yakiwamo yasiyokuwa na mantiki kabisa. Mtakumbuka waziri aliyeamrisha kuchanganya masomo ya sayansi (kemia na fikizia) na kufuta masomo ya biashara. Serikali ikaingia gharama za kuandaa vitendea kazi, lakini baada ya muda mfumo huo ukafutwa.

Ukaja utaratibu wa ukokotoaji na upangaji wa matokeo kwa kuongeza madaraja ya ufaulu kwa kutumia mfumo wa GPA, nao ukaondolewa.

Ukawa usiku, ukawa mchana, Profesa Ndalikacho naye ameingia katika mtego na makosa ya watangulizi wake. Yumkini ana nia njema lakini kwa nini matamko haya anayatoa bila kushirikisha au kufanya utafiti wa kitu gani kinahitajika?

Mimi binafsi huwa nayachukulia matamko ya aina hii sawa na kuwasha taa na kuiweka katika nuru ya jua. Huku ni kufanya kazi isiyo na tija.

Matatizo ya mfumo wa elimu tuliyo nayo hayataondolewa na matamko bali na viongozi walio tayari kushirikisha njia za kutatua changamoto hizo. Viongozi wana jukumu la kuandaa mwongozo, mfumo na mwelekeo wa elimu yetu, lakini isiwe wao ndiyo rejea ya kila kitu.

Naamini wanafunzi wanaoshindwa kuingia chuo kikuu moja kwa moja si kwamba hawana uwezo bali kuna changamoto za kifamilia, kiuchumi na kimazingira ambazo wanakabalina nazo.

Sijajua kama waziri analijua hili au ndiyo ule mtindo wa kupanda kwa kutumia ngazi ukishafika, ama unaondoa ngazi, mwingine asitumie kupanda au unamuambia atumie kamba kupanda.

Mfumo anaotaka kuuondoa una tija kwa jamii kwani ulishawekewa misingi na umezalisha wasomi, wataalamu, wabobezi wa kada mbalimbali na viongozi wa ngazi za juu nchini.

Rai yangu kwa waziri ni kuwa apitie sheria ya elimu ya 1978 iliyofanyiwa marekebishao 1995, inayomtaka aunde baraza la ushauri ambalo litamsaidia katika mambo mbalimbali kabla ya kutolewa uamuzi.


Chanzo: Mwananchi
 

Forum statistics

Threads 1,272,321
Members 489,918
Posts 30,447,379