Serikali isituingize tena mkenge.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali isituingize tena mkenge....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mohammed Shossi, Feb 11, 2011.

 1. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #1
  Feb 11, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Nimesoma taarifa ya bwana Felichesmi Mramba kaimu Mkurugenzi mkuu wa Tanesco na ninamnukuu
  Napenda kuchukua fursa hii adhimu kuishauri Serikali kuwa hili swala la umeme ni nyeti sana na limeongelewa sana watu wametoa ushauri lakini Serikali imetia pamba masikioni. Sote tunakumbuka Mwakyembe aliwapa ushauri Serikali hasa Tanesco kuwa na mipango ya muda mrefu kutatua hili suala la umeme na sio kusubiri hali inakuwa mbaya then wanakimbilia mipango ya dharura. Nadhani Serikali haikulifanyia kazi pendekezo la kina Mwakyembe na sasa I can smell another RICHMOND/DOWANS. Sitaki tufike huko na CCM na Serikali yake lazima wajue kuwa hata wakereketwa na wanaCCM kindakindaki wanaumia na hii hali labda huyo mkereketwa awe "majinuni" asihisi machungu ya huu mgao.

  Nina imani watu wamechoka na Tanesco wanatamani ibinafsishwe au Serikali iruhusu umeme uwe kama secta ya mawasiliano iruhusu kampuni nyingi kuendesha hii biashara kama ilivyoruhusu makampuni ya simu.

  Mwisho kabisa napenda kumalizia TUMECHOKA tunataka UMEME isifike wakati tukakosa uvumilivu!
   
Loading...