Serikali isisubiri maafa Mbagala

Serikali isisubiri maafa Mbagala

Mwendabure

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2011
Posts
2,138
Reaction score
1,045
Salam Wakuu!

Ni wazi kutokana msukumo wa maisha inalazimu watu kubuni njia mbalimbali ili kukabiliana na hali halisi kwaajili ya kupata riziki.

Hali ilivyo pale maeneo ya Mbagala kuanzia Zakhem hadi Rangitatu hasa nyakati za jioni na usiku ni hatari mno kwa wafanyanya biashara ndogondogo na watumiaji wa barabara kwa ujumla. Msongamano wa wachuuzi na bidhaa zao tena kiholela hadi kando kabisa ya eneo ambalo ni maalum kwa kupita magari. Ni hatari mno!

Sitaki kuamini kuwa mamlaka zinazohusika hazijaona kile kinachoendelea pale na sehemu zingine za hapa Dar. Hivyo nashauri Serikali na mamlaka walione na hatimaye kukabiliana na tishio la usalama kwa wachuuzi na watumiaji wa barabara na mali zao bila kusubiri maafa yatokee ndipo hatua zichukuliwe.

Nawasilisha.
 
MKUU HALI HII NI KERO MNO.KAMA UNATOKA TOWN KUANZIA MIDA YA SAA MOJA KUNA FOLENI MJINGA KUANZIA KIZUIANI HATA RANGI 3.
Hii inasababishwa na hao wafanyabiashara wanaopanga bidhaa barabarani
 
Hawataki lawama,acha tu msongamane mpaka mtakapoamua wenyewe vinginevyo.Khaa!kila siku kuombeana mabaya nani anataka.
 
Hata Kama walikingiwa kifua na mh rais kwamba wasibuguziwe, now imekua to much, nadhani wamejisahau, hiyo kauli ya mh rais inawapa kiburi utakuta kupanga bidhaa zake mpaka kavuka msitali unao onyesha mwisho wa bara bara, na wakati huo hana hata Plesha.
 
Yaaani na hii mvua ya leo, mifereji imeziba, maji yametapakaa barabarani. Wanasogea kukwepa maji wanaziba barabara kabisaa, hakupenyeki.
Kuna foleni leo ya kufa mtu.
 
Hilo jimbo hadi leo sielewi mbunge alipatikana vipi
 
Hilo jimbo hadi leo sielewi mbunge alipatikana vipi
Yani Mkuu. Usifukue makaburi ya pale Shule ya Msingi Majimatitu kilipokuwa kituo cha kuhesabia kura. Tulishuhudia Dola ikipiga tikitaka huku imevaa msuli.. Toba!
 
Back
Top Bottom