Tulimumu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 14,395
- 13,266
Wafanyakazi na watu wengi wamekuwa wakidai kupandishwa kwa mishahara kama suluhu la kupunguza au kuondoa ugumu wa maisha. Mimi nina mawazo tofauti na hayo. Kama ingekuwa kupanda kwa mishahara ndio suluhisho la ugumu wa maisha, basi kusingekuwa na tatizo tena.
Mimi nashauri serikali isipandishe mishahara badala yake idhibiti mfumuko wa bei na kushusha kodi katika bidhaa za mafuta na mishahara ya wafanyakazi ili kuleta nafuu ya maisha. Utaratibu huu utawanufaisha hata wasiokuwa na ajira rasmi ya kutegemea mishahara.
Sasa hivi baada ya fununu ya kupandisha mishahara kutoka nauli zimepanda kabla hata ya mshahara mpya. Hii ina maana hata huduma na bidhaa nyingine zitapanda au zimepanda kwa usafiri ndio kiungo cha mahitaji yote. Kupandisha nauli hakuna tofauti na kupandisha bei ya mafuta. Sasa hata mishahara ikipanda faida yake itakuwa ni nini wakati nyongeza itakuwa imemezwa mara mbili au tatu kutokana na kupanda kwa mishahara? Wakati huo huo huduma mbali mbali zitapanda kama kodi za nyumba.
Hapa ndipo ninapomkumbuka Mkapa ambaye hakuwa akipandisha mishahara kila wakati bali alidhibiti mfumuko wa bei na nafuu ilikuwa kubwa kuliko kupandisha mishahara. Hvyo wito wangu kwa wafanyakazi na vyama husika ni kuibana serikali idhibiti mfumuko wa bei na kushusha kodi ya PAYE lakini kuongeza mishahara sio suluhisho! Mishahara ikipanda kila kitu kitapanda kwa kisingizio cha kupanda kwa mishahara na ushahidi wa hili ni kupanda kwa gharama za usafiri kabla ya kupanda kwa mishahara. Sasa ongezeko la mishahara litakuwa na faida gani wakati tayari gharama zimepanda kabla yake.
Kama ingekuwa mishahara ikipanda vitu vinabaki na bei ile ile bila kupanda, maana ya kupanda kwa mishahara ingekuwepo. Balaa la sasa ni kuwa asilimia ya ongezeko la gharama za usafiri inaweza kuwa kubwa kuliko ongezeko la mishahara lililoahidiwa. Hili ni rahisi wala halihitaji digrii kujua. Hivyo kama serikali iko makini isitishe gharama mpya za usafiri, ishushe kodi ya PAYE, idhibiti mfumuko wa bei katika bidhaa za mafuta, umeme na vyakula bila shaka hali itakuwa nzuri. Kumbukeni wakati mdai mishahara mipya tayari Tanesco nao wanataka kuongeza gharama za umeme. Mishahara ikiongezeka watatumia kama sababu ya kuongeza gharama kwakuwa nao itawabidi kulipa mishahara mipya.
Hivyo kwa kutazama hali ya maisha ya Tanzania itakuwa ni kosa kubwa kupandisha mishahara bila kudhiti mfumuko wa bei za vitu na kwa kuwa tayari serikali yenyewe imeshaanza kwa kuongeza gharama za usafiri, itazuia vipi wenginie kuongeza bei za huduma zao. Mkapa bado yupo hebu serikali imtumie kwasababu sisi walipa kodi ndio tunaendelea kugharimia maisha yake mpaka atakapo kufa. Fuateni sera yake ya kudhibiti mfumuko wa bei bila kuongeza mishahara.
Kitu kingine kilicho wazi ni kuwa mishahara ikipanda maana yake na thamani ya shilingi inashuka! Kwa hiyo tutakuwa na hela nyingi zisizoweza kukidhi mahitaji. Tusipokuwa makini tutakuwa kama kisiwa cha Zimbabwe kama Mulugo alivyo alivyosema