Hivi tuna tume ya kudhibiti bei ya bidhaa hasa za chakula? kama ipo ina fanya kazi yake sawasawa? maana issue kama unga,mchele,ngano na maharage ambayo ndio chakula kikubwa cha mtz kinapokuwa uncontrolled ndio tunapoumizana ,issue ya mafuta sio kiviiiile maana kuna watu kule vijijini hawategemei mafuta kwa saana,ie mbongo anatumia kuni kutoka porini,mboga anachuma shambani,chumvi anatumiia magadi (kutoka manyara),maji anachota dimbwini,kiangazi anaenda mtoni,taa wakati wa usiku pia sio lazima maana atawasha moto wa kuni...ingawa influence ya kupanda kwa bei za mafuta pia ipo Kama ndo ningekuwa kubwa yao cha kwanza ningeanza kudeal na control of food prices,kwamba bei elekezi iwe affordable kwa kila mwananchi. Lkn pial wachumi wetu nao mbwembwe tu,mm nahisi hawamshauri mkuu accordingly zaidi ya kumpamba na kumsifia au wanasoma upepo wa mkuu anachopenda kusikia huku asilimia kubwa ya watz wakishindia mlo mmoja tena usio kamili.