Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu.
Nimetafakari sana juu ya hii tabia ya baadhi ya wafanyabiashara kuficha sukari kwa lengo la kutengeneza uhaba bandia ili wauze kwa bei ya kuwaumiza wananchi. Binafsi nimebaini kuwa sukari ni bidhaa muhimu ambayo naamini kuwa kila mtu anaitumia bidhaa hii kila siku kwa namna moja ama nyingine. Hivyo kukosekana kwa bidhaa hii kunaleta sintofahamu katika taifa na kwa kweli huhatarisha usalama wa taifa.
Haya yanayotokea kwenye sukari yaliwahi pia kujitokeza kwenye mafuta na hasa petroli ambapo wafanyabiashara wasio waaminifu walikuwa wanaficha bidhaa hiyo kwa lengo la kutengeneza uhaba bandia na hivyo kufanikisha malengo yao. Kwa sasa hili tatizo kwenye mafuta naona kama limepungia hasa baada ya uamuzi wa serikali kuagiza mafuta kwa pamoja (bulk purchase) ambapo kwa sasa mfanyabiashara mmoja mmoja hana mamlaka ya kuagiza mafuta nje ya nchi isipokuwa kwa kibali maalum kwani jukumu hilo limechukuliwa na serikali.
Kosa walilofanya serikali kwenye sukari ni kuiachia sekta binafsi jukumu la kuagiza sukari nje ya nchi na pia sekta binafsi ndiyo yenye dhamana ya kununua sukari kwenye viwanda vyetu vya ndani. Hawa akina Mohamed Dewji ndio wanaagiza sukari nje ya nchi na ndio hao hao wanaonunua sukari kwenye viwanda vyetu vya Kagera, Mtibwa, Kilombero nk. Kwa hali hii, wafanyabiashara hawa wamekuwa wakijipangia bei kiasi ambacho unashindwa kutofautisha ni wakati gani sukari inazalishwa kwenye viwanda vyetu na wakati gani haizalishwi. Siku zote bei ya sukari imekuwa ikipanda bila ya maelezo yoyote. Sina hakika kama Bodi ya Sukari ina mamlaka ya kudhibiti hali hiyo kama wanavyofanya wenzao EWURA kwenye mafuta
Kutokana na hali hii, naishauri serikali yangu kutumia hii changamoto iliyojitokeza kurekebisha makosa. Ni wakati sasa wa serikali kubeba dhamana kwa asilimia 100 ya kuagiza sukari nje ya nchi. Kww kufanya hivyo, sukari itauzwa kwa bei nafuu na tutalinda pia viwanda vyetu kwani sukari haitaagizwa kiholela tu bali serikali itafanya hivyo ili tu kuziba pengo ambalo viwanda vyetu vimeshindwa kuliziba. Pia uamuzi huo utalinda afya zetu kwani sukari itakayoagizwa itakuwa na ubora tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo baadhi ya wafanyabiashara huingiza nchini hata sukari iliyopita muda wake wa matumizi