Danken Mbombo
JF-Expert Member
- May 30, 2015
- 651
- 339
Asilimia kubwa ya silaha zinazokamatwa kwenye matukio ya ujambazi ni zile za kivita SMG, AK47, mabomu n.k ambazo hazimilikishwi kwa raia isipokuwa kwa vyombo vya usalama tu (jeshi la polisi, JWTZ n.k).
Vilevile bastola nyingi zinazokamatwa kwenye matukio ya uhalifu hazijamilikishwa kisheria. Lakini cha kushangaza kila uhalifu unaposhamiri serikali kupitia jeshi la polisi wanakimbilia kuhakiki silaha walizomilikishwa watu kisheria.
Nashauri serikali isifanye kazi kwa mazoea bali ihakiki pia silaha kwenye maghala ya vyombo vyake vya usalama, tuache kudhani wao ni malaika