nguruka wa kig0ma
JF-Expert Member
- Jan 16, 2020
- 2,943
- 2,934
Saalam!
Ni muda mrefu sasa Watanzania wakilalamikia michango mashuleni bila majibu ya serikali.
Malalamiko yanatoka na kukizana kwa kauli za viongozi wa kuu wa nchi na utendaji wa viongozi wa halmashauri zetu na wakuu wa shule za serikali.
Viongozi wakuu wanasema elimu bure na asiwepo Mwananchi kudaiwa michango.
Viongozi Halmashauri na wakuu wa shule za serikali wanasema matamko ya viongozi wa juu ni siasa tu.
Hali hii inasababisha chuki kati ya wazazi na walimu, kwani mzazi akishasikia hakuna michango, ni lazima amuhoji mwalimu atakayemwambia achangie dawati au ujenzi wa uzio/ madarasa
Chuki hizo huendelea, walimu wakifahamu kuwa mzazi wa mwanafunzi fulani ndiye aliyekuwa anahoji na kupinga michango kwenye vikao, mwanafunzi huyo hatasoma kwa amani, hasira za walimu huamia kwa watoto.
Ni wakati sasa serikali kuweka Jambo hili sawa.
Serikali imeshindwa kutekeleza sera ya elimu bure, irudishe ada mashuleni ili shule ziwezekujiendesha.
Maana ukipiga hesabu utakuta zaidi ya laki tatu mzazi anatoa kwa ajili ya mwanafunzi kwa mwaka.
Dawati
Ujenzi wa madarasa/uzio
Nembo
Faili la mwanafunzi
Rimu nk.
Kwa lugha rahisi shule siyo za serikali Bali ni shule za wananchi
SERIKALI RUDISHA ADA MASHULENI