Serikali ipitie upya viwango vya kujiunga na Elimu ya juu.

Serikali ipitie upya viwango vya kujiunga na Elimu ya juu.

Void ab initio

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2015
Posts
5,740
Reaction score
5,703
Serikali kupitia Wizara Ya elimu ilibadili viwango vya kujiunga na elimu ya juu kwa Advanced level kutoka minimum point 2 hadi 4, na kwa diploma kutoka GPA ya 2.7 hadi 3.5 ,na sasa imebadili tena kutoka GPA 3.5 hadi GPA 3 kujiunga na chuo kikuu. Umefika wakati sasa Serikali ifanye utafiti yakinifu na kuangalia athari zinazoweza kujitokeza za kubadilisha badilisha viwango. Na ikiwezekana irejeshe viwango vya zamani yaani point mbili kwa Sekondari ya juu na GPA ya 2.7 kwa diploma, wakati huo utafiti yakinifu ukiendelea kufanyika ili kuonyesha je kuongeza viwango kuna matokeo chanya katika elimu? .
 
Mtazamo chanya.
Sekta ya elimu inahitaji weledi na utulivu ili kufanya maamuzi yenye kuleta tija. Sio kukurupuka na mwisho wa siku unakuja kugundua kuna negative results tofauti na ulivyotegemea.
Utafiti yakinifu ufanyike kabla ya kufanya maamuzi ya mabadiliko yoyote.
[HASHTAG]#naunga[/HASHTAG] mkono hoja.
 
Kwa sasa kaona vyuo vya private havina wanafunzi kaamua kuachia wa diploma waingie je wa form six je unawafanyaje
 
Serikali kupitia Wizara Ya elimu ilibadili viwango vya kujiunga na elimu ya juu kwa Advanced level kutoka minimum point 2 hadi 4, na kwa diploma kutoka GPA ya 2.7 hadi 3.5 ,na sasa imebadili tena kutoka GPA 3.5 hadi GPA 3 kujiunga na chuo kikuu. Umefika wakati sasa Serikali ifanye utafiti yakinifu na kuangalia athari zinazoweza kujitokeza za kubadilisha badilisha viwango. Na ikiwezekana irejeshe viwango vya zamani yaani point mbili kwa Sekondari ya juu na GPA ya 2.7 kwa diploma, wakati huo utafiti yakinifu ukiendelea kufanyika ili kuonyesha je kuongeza viwango kuna matokeo chanya katika elimu? .
Ina maana GPA wameishusha tena kutoka 3.5 mpaka 3 tena au ni mm sjakuelewa?
 
Kwani jamani mnadhani hata hiyo 3.0 ni mchezo hasa kwa walimu wa diploma waliofanya mtihani wa necta
 
Bora hata hiyo 3.0 maana kidogo ninafuu lakini sasa tufike mahali tuwe na maamuzi ambayo yameshajadiliwa kwa kina na sio mtu kwa kuwa ww ndo msemaji wa mwisho basi unaamua tu unavyoona ww...ila bado wizara ya elimu inashida inatakiwa ijapange kwa watakaojiunga na chuo mwakani
 
Back
Top Bottom