SERIKALI ipige marufuku "MESSAGE" ZA KUTENGENEZWA MITANDAONI

SERIKALI ipige marufuku "MESSAGE" ZA KUTENGENEZWA MITANDAONI

genius crazy

Member
Joined
Oct 21, 2012
Posts
6
Reaction score
1
Kwa bahati mbaya mwaka 2012 ulikuwa ni mwaka mchungu sana hasa ktk tasnia ya sanaa,wasanii kadhaa walitutoka na pia wengine kufikishwa mahakamani na wengine kutafutwa na polisi.Nawazungumzia waliokufa ni pamoja na KANUMBA,SHARO na wengine nisiowakumbuka.mara baada ya kifo cha sharo zilitengenezwa message nyingi sana zinazohusiana naye kwa kumuigiza the way alivyokuwa akiongea,watu "wakaforwardiana" sana japo hazikuwa message nzuri kwa maoni yangu.Tumeanza tu mwaka 2012 msanii mwingine katutoka,namzungumzia SAJUKI,MUNGU Ailaze roho ya marehem mahali pema pepon,AMINA.Bila kuchelewa zishatengenezwa message za kukejeri zikihusisha kukutana kwa SAJUKI,KANUMBA NA SHARO,daaah nasikitika kwa sababu hazifariji zaid ya kulenga kuchekesha!! Cha ajabu serikali iko kimya sana kama waheshimiwa hawazipati.SERIKALI INASUBIRI IZUNGUMZIWE VIBAYA NDIPO WAPIGE MARUFUKU,Haipendez hatakidogo wanapaswa kuzuia hate pale mtu mmoja anapozungumziwa vibaya.WAWASISITIZE WATANZANIA KUFANYA/KUANDIKA MAMBO YATAKAYO CHOCHEA KUFANYA KAZI KWA MAFANIKIO!!! TUGENGE TZ YETU BADO TUPO NYUMA SANA!
 
Kwani zinashida gani?? Kama hutaki wewe ikingia kwenye cm yako futa tu..
 
Sasa watafuta sms ngap? Kuna hizo za wasanii, walevi, maisha,utani wa makabila, nyngne za ki ngono zaid! Zote hazifai kwa jamii cha msingi ni kuwakataza wanaokuforwadia hawatarudia kukutumia.,may b unazipenda ndo mana unazipata mkuu..na pia mitandao inatengeneza pesa kwa hzo meseji na serikali ndo inapata kodi.
 
Hilo ni tatizo la Utandawazi, Serikali haihusiki na hizo msg, ila cha kufanya ni jamii kujichunguza namna tunavyoenenda hasa katika matukio muhimu kama hayo. Linapotokea tatizo la kijamii, kama msiba, kiutamaduni, tunaweka tofauti zetu pembeni. (ziwe za dini, siasa, kabila, rangi hata jinsi) tunaomboleza pamoja (hata kama kulikuwa na kuhitilafiana) Hili halihitaji shule. Inapotokea mmoja wetu akaweza mizaha, basi tuliangalie kijamii zaidi na siyo serikali!!!!!
 
Point of correction, SAJUKI amefariki 2013 sio 2012
 
Back
Top Bottom