Serikali iongee na ACACIA ili kuondoa sintofahamu kwa wafanyakazi

Msolopagazi

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
663
153
Hili la kuzuia mchanga unaozalishwa kwenye migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi kusafirishwa bila kuweka utaratibu mbadala,litatugharimu.

Wafanyakazi zaidi ya 6,000 wameajiriwa kwenye migodi hii na wamepewa notisi ya miezi 2 kuanzia sasa kwamba, kama hakuna kitakachobadilika basi migodi yote miwili itafungwa.

Sababu ni kwamba, mchanga huu unachangia 50% ya mapato ya kampuni, kwa kuzuia usafirishaji wake kampuni inapoteza $350,000 kila siku sawa na $10.5m kwa mwezi. Hakuna kampuni itakayokubali kupoteza kiasi hicho cha pesa kila mwezi kwa kipindi kisichojulikana. Kipindi hakijulikani kwasababu utaafiti uliofanywa na watanzania wenzetu mwaka 2011 ulionyesha kuwa Tanzania haina vigezo vya kujenga mtambo wa kuchenjua mchanga huo, kwasababu uwekezaji wa mtambo huo ni mkubwa no unapaswa kuzalisha angalau Tan 150,000 kwa mwaka lakini Tanzania inazlisha kwa wingi Tan 55 kwa mwaka. Mgodi wa Buzwagi ukifungwa mwishoni mwa mwaka basi kiwango kitashuka hadi Tan 30.

Jambo lingine wanalosema litapelekea kufunga ni kwamba watashindwa ku backfill (kuziba mashing) bila kuziba mashimo hawawezi kuchimba.

Mgodi ukifungwa wafanyakazi takribani 6,000 watakosa ajira, serikali zote zitakosa kodi no mambo mengine.

Mpaka sasa kampuni zimesitisha miradi yote ya maendeleo ya jamii, wameondoa masaa ya kazi ya ziada(overtime) n.k.

Tunaiomba serikali ikae chini no wadau na wataalamu wake kulitazama jambo hili upya kwa masilahi ya Taifa, wawekezaji na wafanyakazi kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom