Serikali inawaogopa wakwepa Kodi? Kwa mfumo huu hawataacha kukwepa kodi

Mtini

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
1,491
2,355
Katika taarifa ya habari ya saa 2 usiku ITV kwa mara nyingine tena serikali imewasamehe wakwepa kodi wa makontena bandarini kwa kuwapa muda wakalipe kodi walizokwepa. Kwa mfumo huu watu hawataacha kukwepa kodi kwani wanajua wakikamatwa wataamriwa kulipa na wasipokamatwa basi wamecheza bingo, pia kwa upande wangu naona ni udhaifu ambao JPM hana budi kuufanyia kazi
 
Nimeiona hii taarifa. Kwa kweli hii nchi itanifanya nife kwa kuvimba hasira. Sielewi ni kwa nini wakwepa kodi hawafunguliwi kesi na kupelekwa mahakamani na hatimaye kupigwa mvua. Nchi kama USA ukikwepa kulipa kodi (Tax evasion or tax fraud) na ikabainika kuwa ni kweli ulikwepa kodi, utahitajika kulipa hiyo kodi na kuangushiwa miaka pia kufuatana na hukumu itakayotolewa. Kitu ambacho hawafanyi ni kuomba mtu alipe halafu aendelee na mambo yake. Huo upuuzi wenzetu hawana na ndiyo maana wanafuata sheria. Ukija hapa kwetu hawa mbwa wanaachwa tu.
 
Nimeiona hii taarifa. Kwa kweli hii nchi itanifanya nife kwa kuvimba hasira. Sielewi ni kwa nini wakwepa kodi hawafunguliwi kesi na kupelekwa mahakamani na hatimaye kupigwa mvua. Nchi kama USA ukikwepa kulipa kodi (Tax evasion or tax fraud) na ikabainika kuwa ni kweli ulikwepa kodi, utahitajika kulipa hiyo kodi na kuangushiwa miaka pia kufuatana na hujumu itakayotolewa. Kitu ambacho hawafanyi ni kuomba mtu alipe halafu aendelee na mambo yake. Huo upuuzi wenzetu hawana na ndiyo maana wanafuata sheria. Ukija hapa kwetu hawa mbwa wanaachwa tu.
Binafsi napata mashaka sana maana nahisi kuna jipu kubwa nyuma yao ambalo liko sehemu za siri haliwezi kukamuliwa
 
Hivi ni kwamba sheria za kuwashitaki hazipo au? mbona utani sasa
 
Back
Top Bottom