Serikali inawalinda wanaokashifu dini - Maaskofu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali inawalinda wanaokashifu dini - Maaskofu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bangoo, Jul 2, 2012.

 1. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #1
  Jul 2, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Baraza la maaskofu catolic Tanzania limemetoa taarifa kuwa serikali imekuwa ikiwakumbatia watu wanaokashifu dini za wanzao!

  Akitoa taarifa ya baraza la maaskofu Tanzania jana Raisi wa baraza hilo Thadeus Ruwaichi alisema serikali imeshindwa kuwachukulua hatua watu waliochoma makanisa huko zanzibar.

  Alisema toka 2010 mpaka sasa makanisa 25 yamechomwa zanzibar na hakuna mtu yoyote anayechukuliwa hatua!.
   
 2. A

  Abdalla Khamis Member

  #2
  Jul 2, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 59
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nyinyi viongozi wa Makanisa mnataka Serikali ifanye nini kwa kitu ambacho hata ushahidi haupo?,tokio la kuchomwa kanisa Zanzibar bado ni tete , hajajulikana msababishi, au ndio mwatafuta namna ya kuimrisha serikali ikamate tu watu kama mnavofanya?, kwa Zanzibar tunasema basi tena ,amri zenu toeni Makanisani sio Serikalini, ama kwa serikali yenu ya muungano sio Zanzibar.
   
 3. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #3
  Jul 2, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  BARAZA la Maaskofu Katoliki Tanzania (Tec) limeilaumu Serikali kuwa, inawakingia kifua watu wanaoendesha mihadhara ya kidini inayokashifu dini nyingine.

  Rais wa Tec anayemaliza muda wake, Askofu Mkuu, Yuda Thadeus Ruwa’ichi alisema jana kuwa, licha ya kwamba jambo hilo linaweza* kuleta chuki na vurugu nchini, Serikali haichukui hatua zozote dhidi yake.

  “Serikali na mamlaka za dola zinawakingia kifua wadau wa harakati wanaoendesha mihadhara yenye kukashfu dini nyingine, pamoja na kufahamika lakini hawachuliwi hatua zozote,” alisema.

  Rais huyo ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanza, alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam wakati wa ibada maalumu ya kutangaza uongozi mpya wa baraza hilo.

  Katika uchaguzi huo Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa wa Jimbo la Iringa, alichaguliwa kuwa rais mpya kwa kipindi cha miaka mitatu.

  Askofu Ruwa’ichi aliitaka Serikali kupiga marufuku mihadhara na makongamano ya kidini, kwani ikiendelea baada ya miaka michache nchi itaingia katika machafuko makubwa yatakayoleta maafa.

  Ruwa’ichi* ambaye alikuwa akitoa tamko hilo kwa niaba ya maaskofu wote, alisema wameshangazwa na ukimya wa Serikali katika kushughulikia vurugu za kidini zinazoendelea kutokea hapa nchini na kuwataka wasiogope kuchukua hatua, kwani hiyo ndiyo dhamana waliyopewa na wananchi.

  “ Tunalaani vikali vurugu na vitendo vya uchomaji moto makanisa vilivyotokea huko Zanzibar na kuwafanya wananchi waishi kwa wasiwasi kwa sababu ya kushindwa kupewa ulinzi na vyombo vya dola,” alisema Askofu Ruwa’ichi.

  Alisema maaskofu wanatoa pole kwa waathirika wa vurugu hizo huko Zanzibar ambao wanaendelea kuishi kwa wasiwasi kutokana na vitisho vinavyoendelea kutolewa dhidi yao.

  Alisema Serikali kama inataka kujenga imani mbele ya wananchi wake, inatakiwa kuchukua hatua ili kuhakikisha vurugu za kidini hazipati nafasi.

  “ Watanzania na mamlaka husika za Serikali zinatakiwa kutafakari kwani mwanzo wa makubwa ni madogo, na mdharau mwiba mguu huota tende,” alisema na kuongeza kuwa vurugu hizo zikiachwa ziendelee zitasababisha matatizo makubwa.

  Askofu Ruwa’ichi alisema kati ya mwaka 2001 na sasa jumla ya makanisa 25 yalichomwa moto Zanzibari, lakini hakuna aliyekamatwa wala kuchukuliwa hatua za kisheria.

  “Kama hakuna mtu yeyote aliyechukuliwa hatua kwa uchomaji moto makanisa hayo, unadhani tatizo hili litamalizika,” alihoji.

  Aidha, Askofu Ruwa’ichi* alitaka vyombo vya habari vinavyoeneza uzushi na chuki za kidini vifungiwe vinginevyo ndiyo kitakuwa chanzo cha vurugu.

  “ Baadhi ya vyombo vya habari vinaeneza uzushi na chuki za kidini kama vile hakuna Serikali. Serikali isikae kimya kama vile hakuna linalojiri, ichukue hatua na kutoa ufafanuzi kwa wananchi,” alisema.

  Akizungumzia ukosefu wa ajira, Askofu Ruwa’ichi* alisema Serikali inatakiwa kuangalia suala hili kwa umakini, kwani vijana ni rahisi kujiunga na makundi hayo yenye vurugu kwa sababu za kutokuwa na kazi za kufanya.

  Alisema katika mkutano huo wameamua kutenga siku moja kwa ajili sala ya kuliombea taifa na kwamba wataendelea kutumia idara za kanisa hilo kujenga masikilizano* na dini mbalimbali, ili kujenga umoja licha ya tofauti zao za kiimani.

  Madaktari na Serikali
  Askofu Ruwa’ichi* alisema, Watanzania wanaangamia nchini mwao kwa kukosa tiba na ulinzi, jambo ambalo ni hatari na kuiomba Serikali kukaa meza moja na madaktari ili kumaliza mgomo huo.

  Hata hivyo, aliwaonya madaktari kuangalia njia nyingine za kutumia katika kudai haki zao badala ya mgomo ambao unapoteza maisha ya wananchi wasiokuwa na hatia.

  “ Tungependa matatizo haya ya Serikali na madaktari yafikie mwisho kwa kufanya mazungumzo kwani wanaoumia ni wananchi,” alisema.
  mwisho

  Askofu Malasusa
  Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Alex Malasusa amewataka wananchi kuacha tabia ya kujilimbikizia mali,* huku wakishuhudia jamii ikiangamia* kwa kukosa mahitaji muhimu kama elimu na afya.

  “Kuna watu wamejaliwa kuwa na kila kitu hata baadhi ya mali zao hawazifahamu pale zinapopotea, lakini kuna kundi la jamii nyingine kati yao ambalo linaishi maisha magumu ambayo linahitaji msaada wa kutosha,” alisema.

  Askofu Malasusa aliyasema hayo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam *wakati wa harambee ya kuchangia mfuko wa kusomesha wanafunzi wasio na uwezo wa ‘Educate The Children’ wa Shule ya Mtakatifu Joseph’s Mbezi Beach kuwa hivi sasa watu wamekuwa na tabia ya kujilimbikizia fedha nyingi.

  “Hivi sasa watu wanajilimbikizia mabilioni ya fedha, huku wakijua kuna kundi la watu ambao linahitaji msaada wao, lakini wamekuwa hawatambui hilo,” alisema Askofu Malasusa.

  Mwenyezi Mungu ametufundisha kugawana kile unachokipata kwa manufaa ya wengine hususan wasio na uwezo, lakini hivi sasa imekuwa tofauti kwa baadhi ya watu kupenda kumiliki mabilioni ya fedha.

  Kauli hiyo ya Askofu Malasusa *inakuja siku chache ambapo Kitengo cha Polisi wa Kimataifa (Interpol) nchini kinachunguza Sh303.7 bilioni ambazo zinadaiwa kukutwa kwenye akaunti sita za Watanzania, wakiwamo Wanasiasa,katika benki mbalimbali nchini Uswisi.
   
 4. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #4
  Jul 2, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,796
  Trophy Points: 280
  Nani sasa anachoma makanisa na amechukuliwa hatua gani?
   
 5. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #5
  Jul 2, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Wakatoliki hukaa na kutafakari, huwa hawakurupuki! Elimu yao huwafanya wawe na busara sana.
   
 6. rugumisa

  rugumisa Member

  #6
  Jul 2, 2012
  Joined: May 29, 2012
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na hao wanaokashifu dini nyingine wajiulize maswali yafuatayo:(1)Tangu waanze kukashifu wamepata waumini wapya wangapi?(ii)Je kukashifu au kutukana dini ya mtu mwingine ni njia nzuri ya kuoneza dini yako au ni kuonyesha inferiority complex , elimu ndogo uliyonayo ya kujenga hoja,na kuwa roho wa bwana hayuko nawe?(iii)Je na wakristu tukikikashifu dini yao watavumilia-maana tukianza itakuwa noma na tunao ushahidi mwingi wa kimantiki,kihistoria na miujiza kutoka mbinguni yenye ukweli usiotia shaka kuhusu tunaloamini?(iv)Je kuna nabii/mtume wa Mungu aliyeeneza dini au ujumbe wa Mungu kwa lugha ya matusi na kejeli-hapa naongelea manabii wa ukweli wa mungu kama Yohana mbatizaji,paulo,petro,musa?-Ukweli utakuweka Huru.
   
 7. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #7
  Jul 2, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Labda serikali ya JMT inasubiri waanze kutua kwa mabomu makanisani kama walivyofanya huko Kenya Jana ndiyo ijishebedue!
   
 8. Y

  Ye Nyumbai Senior Member

  #8
  Jul 2, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kuna msikiti hapa arusha unaitwa masjid kuba,hapo kuna kijana anuza kanda na cd za dini yao lakini anachokifanya ni kuweka cd zinazokashifu ukristu wakati wote.ni wazi cd hizo waumini wao wanazipenda na bila hizo hauzi kitu.tunawashangaa viongozi wanalijuwa hili kwamba matokeo yake si mazuri huko tuendako lakini wanakaa kimya.jiulizenu wakristu nao wakaweka mambo hadharani,tanzania itakalika.si kwamba wakristu hawajui habari ya dini zingine ila wakristu wanafundishwa kuvumiliana na kuchukuliana kiubinadamu.pelekeni watoto shule acheni kuwakaririsha mabo wasiyoyaelewa matokeo yake ni kulalamika mnaonewa kila uchao.
   
 9. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #9
  Jul 2, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  UAMSHO ndio waliochoma makanisa hata polisi wanajua hilo
   
 10. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #10
  Jul 2, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  UAMSHO ndio walichoma
   
 11. Lyceum

  Lyceum JF-Expert Member

  #11
  Jul 2, 2012
  Joined: Oct 1, 2009
  Messages: 915
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 80
  kuna redio inaitwa Imani kule Morogoro. Jamaa wanakashifu balaa. Nina mpango wa kuanzisha kikanisa changu cha kujibu mpigo. LIWALO MA LIWE BANA
   
 12. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #12
  Jul 2, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,903
  Likes Received: 5,365
  Trophy Points: 280
  mihadhara ya waislam kuitupia madongo dini ya kikristo ilianza mara mwinyi alipoingia madarakani,makanisa kuchomwa moto ni baada ya jk kuwa rais...kuna connection flani hapa..
   
 13. S

  SAGANKA JF-Expert Member

  #13
  Jul 2, 2012
  Joined: Jun 9, 2012
  Messages: 313
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Intelijensia ambayo kila kukicha polisiccm wanahubiri iko wapi.Mbona haijatuletea majibu juu ya uchomaji wa makanisa.Au intelijensia imewekewa king'amuzi kwa ajili ya habari za cdm tu.Halafu wewe kila siku nakukataza tabia zako hizo za kuwaambia viongozi wa dini eti wasivuke maji kuzungumzia habari za znz,mbona wewe unavuka maji na kuwajibu maaskofu wa bara,au una jini mahaba,sikuelewi.
   
 14. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #14
  Jul 2, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Wazee wa kununua maspika na kubesha kwenye malori kueleza kuwa Yesu c Mungu na watabakia hvy hvy wenzao wanajenga mashule,vyuo,hospitali na wakiumwa makoo kwa kupayuka kweny maspika watatibiwa kwny hizo hosp kwa kulipia
   
 15. mikonomiwili

  mikonomiwili JF-Expert Member

  #15
  Jul 2, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 274
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  An_nuur na Radio IMani vitazua Vurugu nchini sijui TCRA wanafanya nini ama hawa wamepata Baraka za serikali . Zamani tulizoea kila kitu kinacho Tangazwa kikakua kina angaliwa yaani monitor lakini leo watu wanajitangazia na kuaharibu dini wawengine tu .Nasis tuanze kuwakashfu ili na wao wajisikie vibaya.

  hivi hawawezi kuhubiri kutokana na msaafu bila kugusa ukristo kila kukicha lazima wa seme dini ya wenzao inawahusu nini ?
   
 16. G

  Gulwa JF-Expert Member

  #16
  Jul 2, 2012
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 2,796
  Likes Received: 1,971
  Trophy Points: 280
  "Religion and violence do not go together but religion and reson do" Benedict XVI
   
 17. Y

  Ye Nyumbai Senior Member

  #17
  Jul 2, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Napenda niwafahimishe wale wote wanaukashifu Ukristo kwamba Wakristo si wajinga kunyamaza,nikwasababu Wakristo ni watu wanaopenda amani na utulivu uwepo siku zote.

  Lazima watu wote wafahamu (Waislamu) kwamba hata Wakristu wanaijua Quran vizuri na wanajuwa kuichambua kwa kina pia,watakapoanza akina Simbaulanga na wenzake ndani ya miaka michache misikiti yote itageuka makanisa.

  Narudia tena ndugu zangu ninyi wafwata upepo, pelekeni watoto shule wakaelimike si vinginevyo na haya malalamiko ati Wakristo wanapendelewa yataisha.

  Endelea kusema Yesu si Mungu na nguruwe haramu,mimi namkazania mwanangu asome aje amtume mwanao!!!
   
 18. M

  Makupa JF-Expert Member

  #18
  Jul 2, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Satanic Verses hivi ni nini
   
 19. m

  mzaire JF-Expert Member

  #19
  Jul 2, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  Kwani ni kwenu huko znz nyinyi maaskofu, whts kanisa in znz???

  wakristo wenyewe ni 0.2%, msituletee fujo hapa Tz. Nani atawasikiliza huko znzbar.
   
 20. m

  mzaire JF-Expert Member

  #20
  Jul 2, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nenda kanyolewe huko na hzo pumba zako, nendeni mkawakamate si mshawajui, zogo la nini tena???
   
Loading...