Serikali inavyoibiwa ukusanyaji ushuru magetini wakati wa kusafirisha mazao

NYEKUNDU YA BIBI

JF-Expert Member
Oct 27, 2017
2,300
2,970
Habarini Wakuu

Naomba niende moja kwa moja kwenye lengo langu

Hatimaye msimu wa uuzaji na ununuzi mazao hasa ufuta maeneo ya Mbeya umeelekea tamati au kufikia kikomo. Kumekua na upotevu wa mapato kijanja kwa namna hii hapa chini.....

Mfanyabiashara hatoi hela halali ya ushuru na anapofika getini anahonga hela kila geti kwa makubaliano binafsi na mlinzi wa geti. Mfano kama gunia inabidi lilipiwe 6000 Mfanyabiashara anatoa rushwa ya 3000 kwa kila gunia na hii inaingia moja kwa moja mifukoni mwa walinzi wa geti nakusababisha hasara kubwa kwa kusanyo la Serikali,

Nini kifanyike......
Serikali iongeze macho hasa magetini inapoteza sehemu kubwa ya pato inaende kwa watumishi wasio waaminifu na kama itaweza kufuatilia maongezi nimeshuhudia ubadhirifu unaoumiza Serikali yetu watumishi wanaifanya Serikali yetu kupoteza uaminifu

Hongera za dhati kwa Rais wetu John pombe Magufuli, Kiongozi wa SADC nakutakia utekelezaji mwema wa kazi

TANZANIA YA VIWANDA NA WATUMISHI WAAMINIFU NA WANAOTII AMRI MBELE YA RAIS WETU
 
Back
Top Bottom