Serikali inasahau inachosema kwa wananchi

Wilderness Voice

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2016
Posts
921
Reaction score
1,651
Nakumbuka wakati serikali ikipigia chapuo tozo walisema, tozo itawezesha nchi, na nchi itaondokana na mikopo ambayo mingi mashariti yake si rafiki. Haya yalisemwa na kusisitizwa na Mhe. Rais akiwa anapita maeneo ya Tegeta akiwa safarini kutengeneza Movie ya Utalii Tanzania.
Cha ajabu serikali hii ikabadili gia, ikakopa 1.3 trillion kujengea madarasa. Yaani nchi yetu kujenga madarasa wenyewe hatuwezi tunaenda kukopa. Nchi ya maajabu. Hapo hatukuambiwa fedha ya tozo inaenda wapi kama wamebadili gia.

Katika hotuba ya Rais kusaini mkataba wa ujenzi wa kipande cha reli ya SGR Makutupora - Tabora, Rais katamka wazi na kusisitiza kukopa ni lazima. Na miradi yote itamalizwa kwa kukopa. Hivyo nchi itaendeshwa kwa mikopo. Tena Rais akasisitiza Fedha ya tozo haitahusika katika miradi.

Nachojiuliza hii tozo fedha yake inatumika wapi sasa? Make kwenye madarasa haijatumika tumekopa. Rais kasisitiza kuwa kwenye miradi fedha itakopwa, fedha ya tozo haitatumika! Sasa tuelezwe fedha ya tozo inaelekezwa wapi? Na kwanini Mwanzo serikali ilidanganya kuwa tozo ndo itakuwa suluhisho. Na Rais akakandia mikopo kuwa si mizuri? Cha ajabu leo Rais anasisitiza kuwa mikopo ni mizuri? Na nchi itakopa?

Serikali haina muelekeo, inajiendesha kwa kubahatisha! Hivi huyu waziri wetu wa kupanga uchumi wa nchi na fedha anaushauri mzuri kweli kwa Rais wetu? Makusanyo ya ndani imekuwa siri, hakuna msisitizo mkubwa kwa makusanyo ya ndani. Kama nchi itaendelea kuendeshwa kwa mikopo. Hakuna ubunifu wa mapato zaidi ya tozo. Basi maendeleo ya Tanzania ni ndoto.
 
Je hawa nao walisahau maneno yao au waliamua kuwaona wanachama wao ni misukule isiyojua kutofautisha uongo na ukweli? Mwaka 2008 hadi July 2015 Lowasa ni fisadi, afu October 2015 hadi 2018. Lowasa sio fisadi.

images (7).jpeg

images (10).jpeg
 
Je hawa nao walisahau maneno yao au waliamua kuwaona wanachama wao ni misukule isiyojua kutofautisha uongo na ukweli? Mwaka 2008 hadi July 2015 Lowasa ni fisadi, afu October 2015 hadi 2018. Lowasa sio fisadi.

View attachment 2060544

View attachment 2060545
Kosa halitetewi kwa kosa. Nimekuwa naona mijadala mingi haijibiwi kwa hoja bali mbona fulani alifanya hivi. Jibu hoja iliyopo si kurukia mambo yalopita hata Chadema wao walijisahihisha na hatimae uchaguzi uliofuata waliweka mtu wao ndani ya Chadema kugombea.
Nchi haiendeshwi kisa fulani mbona nae alikosea!
 
Back
Top Bottom