Serikali inapowakatili raia wake kodi za kuingiza magari: Nini kifanyike?

KAMBAKO

Member
Dec 18, 2011
11
0
Kuna hawa waheshimiwa wanaotaka kuipeleka Serikali mahakamani kudai kwamba kodi ya magari machakavu ni ya kibaguzi kwa vile iinabagua watu masikini dhidi ya matajiri.

Ukinunua gari lililotumika miaka kumi au zaidi unalipia kodi kama asilimia 20. Ukinunua jipya hulilpi kodi hii. Mimi nawaunga mkono, ila sijui uwezo wa sheria kutusaidia sisi akina yahe.


 
Tanzania kuna sheria against wanyonge tu, ni linchi la ajabu kabisa kabisa! i am ashamed to be a Tanzanian.
 
Inaweza kuonekana ni against wanyonge lakini ukwei ni kwamba lengo la sheria hiyo ni ku discourage dumping. Nadhani tulionununua mf. used japanese cars mtaniunga mkono kuwa mara baada ya kununua lazima ulipeleke gereji na utakuta shock absorbers, ball joints na mfumo mzima wa suspension unahitaji kubadilishwa. Gari ya rafilki yangu mmoja nilliitoa bandarini na wakati naendesha niligundua breki zipo chini sana, kwenda gereji pads kwishnei. Huwezi amini, service yote ilitugharimu almost 1 million.

Vile vile ni kutokana na ubovu wa magari hayo kumekuwa na ongezeko kubwa la ajali na kusababisha vifo na majeruhi wengi ukizingatia mengi ya magari hayo yametengenezwa kwa asbestos na sio chuma,bati na unapopata ajali gari linachakaa utadhani limepondwa mawe.

Naunga mkono hii sheria kwani hata ukitembelea mitandao ya kijapan iuzayo magari online utakuta gari la mwaka 2001 kurudi nyuma lina bei rahisi kuliko 2002 na kuendelea na hata ubora wake upo juu.

USHAURI: Unaponunua gari used hakikisha unapeleka gereji na kufanya service kubwa kabla ya kulitumia na kumbuka kubadili tairi.

Nawahi dinner!
 
Naomba mnijulishe ukiagizia gari kutoka japan lenye umri wa zaidi ya miaka 10 kodi ni kiasi gani kutoa pale bandarini?ahsante.
 
Utalipa kama ifuatavyo

1. Import duty 25%
2. VAT 18%
3. Excise duty 10%
4. Stamp duty 1.4%
5. Destination Inspection fee 1%
6. Dumping fee 25%

Jumla 80% This is the reason why most of us don't drive cars!!!
 
KAMA MTUMISHI WA UMMA UNAWEZA kuaapplya exemption pale hazina
 
Hii ndinga naimaindi sana..........jamaa wanataka $6,500 CIF........kodi zitakuwaje?


Mkuu kwanza fungua www.tra.go.tz halafu angalia CRP (CURRENT RETAIL PRICE) ya hiyo model halafu ukiipata kuna rate ya depriciation ambapo utatoa hiyo value yao inayobaki ndio msingi wa kodi kama post namba 2.
 
Wakati EWURA wanatangaza kupanda kwa gharama ya umeme walielekeza pia kuwa wafanyakazi wa TANESCO walipe ankara za matumizi ya umeme sawa na wateja wa kawaida.

Imekuwa ni kawaida kwa makampuni, mashirika na taasisi nyingi kutoa motisha za huduma ama bidhaa wanazozalisha kwa wafanyakazi wao, mathalani utakuta wafanyakazi wa TBL hupewa kiasi fulani cha bia kila mwezi, wafanyakazi wa ATCL hupewa ticket za kusafiria kila mwaka, wafanyakazi wa serikali na taasisi zake kama EWURA kusamehewa ushuru wa magari waingizapo kutoka nje, n.k.

Msamaha wa ushuru haupunguzi kodi za watanzania? Wafanyakazi wengi wangependa kununua magari lakini ushuru unakuwa mkubwa na hivyo wafanyakazi wa serikali hutamba na magari mazuri na makubwa mitaani.

Je ni haki wafanyakazi wa TANESCO pekee kuondolewa privelege hiyo, wafanyakazi wa serikali pamoja na taasisi zake kama EWURA nao walipe ushuru wa magari yao.
 
Inajulıkana kuwa mıshahara ya Serıkalı nı mıdogo kwahıyo kupunguzıwa kodı nı motısha. Na wengı wao wananunua hayo magarı kwa mıkopo na akıpata msamaha kıdogo ndıyo mtu anapata uwezo na yeye wa kuonekana barabaranı.
 
Kwa hiyo mtmishi wa umma mwenye exemption analipa nini na halipi nini? Tafadhali nipatie maelezo zaidi.

UFAFANUZI KUHUSU MSAMAHA WA KODI KWA WATUMISHI WA
UMMA.
1.0 Utangulizi
Watumishi wengi wa Serikali na Mashirika na taasisi za Umma wamekuwa wakiuliza
mara kwa mara kuhusu msamaha wa kodi katika ununuzi wa magari yao kwa ajili ya
kuwasaidia usafiri wa kwenda kutekeleza majukumu yao ofisini na kuwasaidia nyumbani
katika shughuli zao mbalimbali za kijamii. Yafuatayo ni maelezo ya utaratibu wa kupata
msamaha wa kodi kwa magari yatakayoingizwa au kununuliwa hapa nchini na watumishi
wa umma au Serikali.
2.0 Sheria husika
Msamaha huu unatolewa kwa mujibu wa GN. Na. 520 na 522 za mwaka 1995
3.0 Wanaostahili kupata msamaha
Mtumishi wa umma ambaye kwa mujibu wa sheria anafaidika na msamaha wa ushuru
katika vyombo vya usafiri ni mwenye ngazi ya mshahara ya TGS D au zaidi kwa upande
wa serikali au inayolingana na hiyo kwa upande wa Taasisi zingine za serikali na
mashirika ya umma.
Mtumishi wa umma ambaye anaendelea na masomo yake hapa nchini au nje
ya nchi haruhusiwi kupewa msamaha wa ushuru hadi pale atakapomaliza
masomo yake na akaendelea na utumishi wa umma.
4.0 Aina ya vyombo vya usafiri vinavyohusika na msamaha
(a) Magari
Magari madogo aina ya saloon
Magari aina ya pick – up yenye uwezo wa kubeba mzigo usiozidi uzito wa
tani mbili
Magari mengine ambayo hayabebi zaidi ya abiria tisa.
(b) Pikipiki za aina zote.
5.0 Aina ya Ushuru unaosamehewa
Ushuru wa forodha (Import duty)
Ushuru wa bidhaa (Excise duty)
6.0 Aina ya kodi/ada zinazotakiwa kulipwa (Hakuna Msamaha)
Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT)
Ada za usajili
Pia ushuru wa bidhaa maalumu kwa magari yenye umri wa miaka kumi au zaidi
toka kutengenezwa
Gharama za bandari
7.0 Taratibu muhimu za kufuata
7.1 Kujaza fomu ya maombi (Nakala nne) ambayo ni lazima iambatane na:-
(i) Uthibitisho wa mwajiri
(ii) Nakala ya kitambulisho cha kazi
(iii)Kumbukumbu za ununuzi au uingizaji wa chombo husika cha usafiri hapa
(iv) Picha nne (4) za "passport size " kwenye fomu ya maombi.
7.2 Baada ya kupata fomu za maombi TRA inatakiwa kuzifanyia uhakiki na
iwapo ni sahihi hupelekwa Hazina kwa kwa ajili ya kuandika hundi kwa kiasi cha
ushuru uliosamehewa na kuwasilisha TRA
7.3 Baada ya TRA kupata hundi toka Hazina taratibu zingine zitaendelea za kuruhusu
chombo cha usafiri kutolewa kwa mwenye nacho baada ya kulipa kodi zingine na ada
kama vile Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na ada ya usajili wa gari
8.0 TAHADHARI!
8.1 Kwa wale ambao wanaagiza vyombo vya usafiri toka nje wanashauriwa
kufanyautaratibu wa kupata msamaha wa ushuru kabla ya chombo husika hakijafika
hapa nchini.
8.2 Ni kosa kisheria kuuza chombo cha usafiri kwa mtu mwingine ambaye hastahili
msamaha bila kwanza kulipa Ushuru/kodi iliyokuwa imesamehewa. Pia ni kosa
kutumia kwa shughuli za biashara.
8.3 Epukana na matapeli wakati wote wa kushughulikia msamaha unashauriwa kutumia
mawakala wa forodha wanaotambuliwa na TRA
Kwa maelezo zaidi wasiliana na :
Mkurugenzi,
Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi
SIMU 2119343
Barua pepe info@tra.go.tz
 
Kodi hizi kwenye magari ya abiria anabebeshwa malalahoi.

Road Licence,
Fire,
Bima,
Ewura,
Summatra,
Mapato ya halmashauri,
Kulipia Stand,
Wapiga debe,
Wiki ya nenda kwa usalama,

Katika bajeti hii serikali ionyeshe ni jinsi gani itaanza kuzipunguza kodi hizi maana sasa kila idara ya serikali inataka kubuni mapato toka kwenye magari si ya abiria tu bali hata ya binafsi.
 

Tofautisha KODI, USHURU, TOZO n.k.
 
MIONGONI MWA KILIO KIKUBWA KWA BAJETI ILIYOPITISHWA MWAKA JANA ILIKUWA NI KODI KUBWA YA KUTOA MAGARI BANDARINI.

REFER TO THE ATTACHMENT: View attachment proposed tax rates_2.pdf

Je bajeti hii itatuangalia walalahoi ili angalau kusiwe na mlolongo wa kodi katika kutoa gari na kulisajiri??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…