Kang kin
Senior Member
- Mar 21, 2017
- 154
- 122
Salaam
Kama kichwa kinavyoeleza ni mwaka wa pili sasa serikali haijatoa ajira wala kupandisha mishahara na vyeo kwa watumishi kwa kigezo kwamba bado inafanya uhakiki wa watumishi hewa hakuna anayepinga kwamba zoezi hili si jema.
Baada ya Mhe. Rais kukabidhiwa ripoti ya watumishi hewa watanzania wengi walipata matumaini kwamba zoezi hili limefikia ukomo badala yake hivi karibuni mawaziri wanasimama majukwaani na kuuambia umma kwamba uhakiki bado unaendelea, madhalani kauli zao zimekuwa zikibadilika mara kwa mara,
Wakati Mhe. Simbachawene akijibu swali bungeni kuhusu upungufu wa watumishi uliojitokeza baada ya uhakiki aliahidi kwamba mwez june ajira zingetangazwa kuziba pengo kwa watumishi waliokutwa na vyeti feki lakini kauli ya mhe.Angela kairuki ya hivi karibuni ajira hizo ni mwezi august sasa swali la kujiuliza serikali moja lugha tofauti kuna nn?.
Bila shaka japo jambo hili la ajira na kupandisha mishahara na vyeo halijapewa kipaumbele watanzania wengi wanayo maswali kadhaa mioyoni mwao.
1.Je, kwa mwaka wa fedha ulipoita 2016/2017 serikali ilipanga kuajiri na ikatenga fungu kwa ajili ya watumishi wapya na badala yake haikuajiri kama ilivyo kusudia kwa kigezo cha uhakiki hizo hilo fungu lilienda wapi?
2. Ikiwa Rais alikabidhiwa ripoti ya watumishi hewa kauli za mawaziri kwamba uhakiki bado unaendelea ripoti iliyotolewa na yenyewe ni feki tusubiri original?
3. Ikiwa watanzania wanalipa kodi na bado kuna upungufu wa watumishi zahanati, mashuleni n.k na kwann hawapati huduma stahiki kwa sababu niwalipa kodi?
4. Je, kwanini serikali isitangaze kufuta baadhi ya Degree, Diploma na certificate programme kwa sababu hakina mpango wa kuajili mfano Ualimu wa sanaa?.
Mtazamo wangu.
1. Mawaziri wenye dhamana na masuala ya ajira na utumishi ni vizuri wakae kimya kuliko kutoa matamko tata kila itwapo leo.
2. Serikali itamke wazi kwamba haina mpango wa kuajiri kwa kipindi cha miaka kadhaa kuliko kuja na siasa za danganya toto kila kukicha.
3. Serikali itangaze mwisho wa zoezi la uhakiki ni lini.
4. Serikali iache kujificha kwenye koti la uhakiki itamke wazi nini kinasibu mpaka isitoe ajira mpya.
5. Serikali itoe mikopo isiyo na riba kwa wahitimu wenye uhitaji wa mikopo ili waweze kujiajiri wao wenyewe kuliko kuwaambia wajiajiri na wakati hawana mitaji na yule anayesisitiza wajiajiri ili hali yeye ameajiriwa
Karibuni kwa maoni wadau