Nimesikitika sana kuona wizara ya ujenzi ikiweka mikakati ambayo kwa dhati ya moyo wao ni mambo ambayo hayawezi kutekelezeka labda mpaka Yesu arudi. Nimekuwa nikifuatilia kwa umakini sana bajeti ya wizara ya ujenzi, mawasiliano na uchukuzi kwa vipindi vingi lakini pointi yangu inaanzia bajeti ya 2013/2014. Katika bajeti ya mwaka 2013/2014 serikali iliweka bajeti ya kujenga barabara ya kuanzia pugu kwenda bunju kupitia mbezi mwisho na mpiji magoe. Mwaka huo serikali ikasema inaanza upembuzi yakinifu. Bajeti hiyo ikapita na ikaisha.
Bajeti iliyofuata 2014/2015 ikawekwa pia lakni hakuna kilichofanyika. Bajeti ya 2015/2016 ikawekwa pia lakini mambo yakwa yale yale. Bajeti hii inayoisha yaani 2016/2017 pia iliwekwa na sasa bajeti inaisha.
Kilichonisikitisha ni ubabaishaji uliofanywa na waandaaji wa bajeti ya 2017/2018 kwa kukopi yale yale ya mwaka 2016/2017 na kuyapaste kwenye hii bajeti yanayohusu hii barabara. Naona walichoweza kuedit ni figure tu ambazo zimepunguzwa kutoka zaidi ya 900m mpaka zaidi ya 400m. Je serikali kama haina uwezo si waache kupanga mambo yasiyowezekana? Weka kwenye bajeti yale unayoweza kutekeleza ndani ya mwaka husika lakini si kwa kubabaisha huku. Barabara kila mwaka iko kwenye bajeti lakini hakuna linachofanyika! Mimi naona hii ni kwa sababu ya kutokuwa na hela na ndo maana hela inayopangwa haipelekwi na kila mwaka inapungua. Miaka 5 barabara inapangwa kujengwa inashindikana sasa si muitoe kwenye bajeti?
Alafu nilichokiona bajeti yenyewe ni copy and paste and edit kidogo ndo maana mambo yaliyotakiwa kutekelezwa miaka mitano iliyopita yakashindikana tunaendelea kuyaona mpaka bajeti za mbele yakiwa na uwezekano wa kutokutekelezwa.