Serikali inamkingia nani kifua Kashfa ya Rada? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali inamkingia nani kifua Kashfa ya Rada?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Dec 2, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Dec 2, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,403
  Likes Received: 81,428
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Serikali inamkingia nani kifua Kashfa ya Rada? [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Thursday, 01 December 2011 20:27 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] Mwananchi

  Kashfa ya ununuzi wa Rada kutoka katika Kampuni ya BAE ya Uingereza imeingia katika sura mpya baada ya Bunge la nchi hiyo kuitaka Serikali ya Tanzania iwafikishe mahakamani watu wote walioshiriki katika ununuzi wake na kuiingiza nchi katika hasara ya mabilioni ya fedha.

  Kupitia kamati yake ya Maendeleo ya Kimataifa, Bunge hilo limesema lingependa kuona watu wote walioshiriki katika mchakato wa ununuzi wa rada hiyo wakifikishwa mahakamani kujibu tuhuma za ufisadi. Taarifa ya kamati hiyo iliyonukuliwa na BBC, ilieleza kwamba wajumbe wake ambao ni wabunge kutoka vyama mbalimbali nchini humo walisema watatoa ushirikiano wa dhati kwa Tanzania iwapo itaamua kuwashtaki watuhumiwa hao nchini Tanzania au Uingereza.

  Kwa mujibu wa BBC, wabunge hao wamesema, mbali na kurudishiwa fedha iliyozidi kwenye ununuzi huo unaosemekana ulitawaliwa na rushwa, Serikali ya Tanzania inapaswa kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wote haraka iwezekanavyo ili haki itendeke. Hata hivyo, wakati wabunge hao wakisisitiza jambo hilo, Serikali ya Tanzania imekuwa ikidai kwamba haina ushahidi wa kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wa ufisadi katika ununuzi wa rada hiyo.

  Wito huo wa wabunge wa Uingereza umekuja wakati tayari Kampuni ya BAE Systems iliyoiuzia Tanzania rada hiyo kwa bei ya kuruka, ikikiri kwamba kulikuwa na kasoro katika mchakato mzima wa ununuzi wa rada hiyo, hivyo kuahidi ingeirudishia Tanzania Dola za Marekani 46 milioni kama fidia. Mpaka sasa kampuni hiyo haijarudisha fedha hizo.

  Lakini pia wito huo wa wabunge wa Uingereza unakuja miezi kadhaa tangu Serikali ya Tanzania ipeleke ujumbe wa wabunge wanne nchini Uingereza kufuatilia malipo hayo ukiongozwa na Naibu Spika, Job Ndugai. Katika ripoti iliyotolewa na wabunge hao katika Mkutano wa Nne wa Bunge la Kumi, wabunge hao walisema kwamba waligundua madudu ya kutisha kuhusu ununuzi wa rada hiyo na kupendekeza mambo kadhaa, ikiwamo kushtakiwa kwa wahusika wa kashfa hiyo hapa nchini.

  Wabunge hao pia waliwaeleza waandishi wa habari jinsi madhambi waliyoyagundua katika mchakato mzima wa ununuzi wa rada hiyo yalivyokuwa makubwa kiasi cha kuwa ushahidi wa kutosha kuwatia hatiani iwapo Serikali ingeamua kuwafungulia mashtaka mahakamani. Ingawa wabunge hao hawakuwataja watuhumiwa hao katika mkutano huo, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati wa utiaji saini wa ununuzi wa rada hiyo, Andrew Chenge, ambaye sasa ni Mbunge wa Bariadi Magharibi ni mmoja wa watuhumiwa wakubwa na hakika hali hiyo imempa wakati mgumu katika chama chake cha CCM.

  Jambo la kushangaza ni kwamba, pamoja na msimamo wa wabunge hao kwamba watuhumiwa katika kashfa hiyo washtakiwe kulingana na madudu waliyoyabaini, Serikali iliweka pampa masikioni, huku Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Eliezer Feleshi akidai hapakuwa na ushahidi wa kuwafungulia watu hao mashtaka. Na katika hali ya kushangaza, mkurugenzi huyo alirudia kauli hiyo juzi baada ya wabunge wa Bunge la Uingereza kutaka watuhumiwa hao wafikishwe mahakamani na kwamba wangetoa ushirikiano kwa Serikali ya Tanzania, jambo lililotafsiriwa kwamba wanao ushahidi wa kuwatia hatiani.

  Wakati yote hayo yakitokea, mtandao maarufu wa Wikileaks, ambao umekuwa ukifichua siri nzito katika duru za kiserikali, kidiplomasia na kisiasa katika nchi nyingi duniani ulieleza jana kwamba Serikali ya Tanzania iliamua kutofungua mashtaka dhidi ya watu hao kwa madai kuwa kesi hiyo ingemhusisha Rais mstaafu, Benjamin Mkapa na marafiki wa karibu wa Rais Kikwete na kwamba Mkurugenzi wa Takukuru, Edward Hoseah alizuiwa na kutishwa asiwafungulie mashtaka watuhumiwa wa kashfa hiyo.

  Sisi tunadhani Serikali inajidhalilisha kwa kuendelea kukataa kuwafikisha watuhumiwa mahakamani. Kisingizio cha kutokuwapo ushahidi ni kichekesho kwa sababu Serikali haijawahi kufanya jitihada zozote za kuutafuta ushahidi huo. Litakuwa jambo jema iwapo wananchi wataibana Serikali ili ukweli wa suala hilo ujulikane ili sheria ichukue mkondo wake.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #2
  Dec 2, 2011
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,788
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  mzee wa vijisenti, dr.Idrissa wakuu wa jeshi etc
   
 3. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #3
  Dec 2, 2011
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,788
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  ushahidi gani unakosekana wakati SFO walichunguzi sakata lote na pia serikali ya uingereza ipo tayari kutusaidia ikiwa ni pamoja na kutupa ushahidi na nyaraka mbalimbali mbona basi serikali yetu haijawasiliana na uingereza kuomba huo ushahidi??
   
 4. Chipukizi

  Chipukizi JF-Expert Member

  #4
  Dec 2, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 1,970
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Uwenda mmoja wa watuhumiwa wa apa Tanzania,ni mmoja wa anaetaka gombea ukazi wa pale kwenye jumba,jeupe magogoni,sasa akipelekwa kwa pilato si itakuwa so,mie napita tu
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Dec 2, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,403
  Likes Received: 81,428
  Trophy Points: 280
  Inaudhi na kusikitisha sana kuona wahusika wote wa uchafu chungu nzima uliofanyika wakati wa Mkapa na hata Kikwete bado wakiendelea kukingiwa kifua huku hali ya nchi ikizidi kwenda mrama. wamechota zaidi ya Trillioni moja lakini wote bado wanapeta tu huku wakiwa busy kupigana vibega kuelekea 2015. Katika hali kama hii tusitegemee kabisa kuwa na maendeleo ya aina yoyote ile miaka nenda miaka rudi.
   
 6. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #6
  Dec 2, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,245
  Trophy Points: 280
  Hata issues za dowans na mikataba ya madini iliyosainiwa hotelini jumapili si ilikua haina ushahidi wa kutosha? UN ituundie ICTR yetu, hizi issues zinanyamaziwa lakini zitakuja kutuletea genocide hapa.
   
Loading...